Posts

Showing posts from August, 2023

WAOKOTA VYUMA CHAKAVU HATARINI KUPATWA NA MIONZI

Image
Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, Profesa. Lazaro Busagala (kulia), akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Austria, Naimi Aziz, alipotembelea ofisi za Tume hiyo leo jijini Dodoma na kuzungumza na wafanyakazi wa Tume Baalozi Naimi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili hapo Mkurugenzi Busagala, akimuonyesha Maabara za Tume hiyo Mkurugenzi akimweleza jambo kwa msisitizo Balozi Wafanyakazi na wanahabari wakiwa katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Habari wa Tume hiyo akiwakalibisha  wanahabari na balozi katika mkutano huo Mkuu wa Tume hiyo Kanda ya Kati, Machibya Matulanga,akitoa maelezo kuhusu kazi za Tume hiyo Picha zikionyesha miili ya binadamu iliyopata madhara kutokana na kukusanya vyuma chakavu Balozi na Mkjurgenzi wakisikiliza kwa makini maelezo ya tume hiyo Mkurugenzi wa Nguvu za Atomu nchini Profesa Lazaro Busagala, amesema wakusanya vyuma chakavu wapo katika hatari kubwa ya kupata maradhi ya mionzi kama hawatakuwa makini wakati wakifanya kazi hiyo, Mkurugenzi

RAIS DKT. SAMIA KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi mbalimbali vya Sanaa vikitumbuiza kwenye Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) katika viwanja vya Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023. Viongozi, Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa kwenye viwanja vya Paje kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) lililofanyika Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Simba wakati akikagua mabanda mbalimbali yaliyopo kwenye viwanja vya Paje katika Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AZINDUA MPANGO WA USAFIRISHAJI WA DHARURA KWA MAMA NA MTOTO.

Image
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa  Mpango wa usafirishaji dharura mama na mtoto ( m-Mama) Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma Dkt.Edson Fransis akizungumzia mpango wa usafirishaji dharura  m-mama utakavyosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto. Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Jumanne Mwankhoo akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Usafirishaji wa dharura m-mama kwenye viwanja vya hospitali ya Rufaa mjini Songea. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezindua Mpango wa Usafirishaji wa Dharura kwa akinamama wajawazito,waliojifungua na Watoto wachanga (m-mama). Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Mkoa mjini Songea,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo,amesema mfumo huo utahakikisha vituo vya kutolea huduma za afya na wenye d

MBIBO AWAOMBA MABALOZI KUISAIDIA WIZARA KUTIMIZA NDOTO ZA WAASISI SEKTA YA MADINI

Image
  *Kamishna wa Madini awaeleza Mabalozi  kuweka Msukumo kwenye Madini Mkakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewaomba Mabalozi Wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwezesha Sekta ya Madini kutimiza Ndoto za Waasisi wa Taifa kwa kuendeleza jitihada za Wizara za kuhakikisha rasilimali madini zinatumika kujenga uchumi imara, maendeleo ya nchi na watu. Ili kutimiza ndoto hizo, Mbibo amewaomba kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kwenye Sekta ya Madini na kuvutia uwekezaji nchini kwa lengo la kuongeza mchango wake kiuchumi na kimaendeleo. Mbibo ameyasema hayo Agosti 30, 2023 jijini Dodoma katika kikao kilicholenga kuwajengea uwezo kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya Madini ikiwemo maeneo muhimu ya kipaumbele na yanayopaswa kupewa msukumo kiuwekezaji ikiwemo kuimarisha na kujenga ushirikiano na nchi wanazokwenda. Mabalozi waliotembelea wizara ya madini ni Balozi Joseph Sokoine anayekwenda nchi ya Canada, Balozi Fatma Rajabu a