TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI INAHITAJI WAFANYAKAZI 170O---- MNDOLWA


Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji nchini  Raymond Mndolwa, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dododma leo., akielezea utekelezaji wa  Majukumu ya Tume hiyo na  Mwelekeo wa Ujenzi wa Miradi ya Umwagiliaji mwaka wa Fedha 2023 na 24
MKURUGENZI MKUU WA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI, RAYMOND MNDOLWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TUME YA UMWAGILIAJI NA MWELEKEO WAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA HABARI - MAELEZO JIJINI DODOMA* #Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanzishwa kwa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Sura 435 kama Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara inayohusika na Umwagiliaji.

# Majukumu makuu ya Tume ni kuratibu, kuendeleza na kusimamia Maendeleo ya kilimo cha Umwagiliaji nchini.

#Mafanikio ya Tume kwa mwaka wa fedha 2022/23. Hadi kufikia Juni 2023, Tume imesaini mikataba 48 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 234.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa skimu na mabwawa yaumwagiliaji;

#Mikataba 22 yenye thamani ya shilingi Bilioni 25 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Mikataba mitatu (3) yenye thamani ya Shilingi Bilioni 23.9 kwa ajili ya ununuzi wa magari na mitambo;

#Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni mbili (2) kutoka nchi za Italia na Uispania kwa ajili ya kufanya mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa miradi ya Bonde la Mto Mara na mradi wa Kisegese uliopo katika Bonde la Kilombero.

#Tume imefanikiwa kununua mitambo 15 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji;

#Tume imenunua magari 53 kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya umwagiliaji. Tume pia imefanikiwa kupata fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa PFoR ambapo utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2023/2024; Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 70 kwa miaka mitano; na

#Aidha, Tume imefanikiwa kupata fedha kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kupitia mradi wa “Irrigation Development Advisory”. Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

#Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, mwelekeo wa Tume ni kuendelea kutekeleza miradi itakayoongeza eneo la umwagiliaji lenye ukubwa hekta 256,185.46 ili kufikia hekta milioni 1,200,000 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2020),

#Awamu ya Tatu ya Mpango Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III; 2021/2022-2025/2026) na Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II) na kufikia hekta milioni 8.5 ifikapo 2030 (Agenda 10/30).

#Ili kufikia malengo hayo Tume imepanga kutekeleza jumla ya miradi 822, ambapo miradi 114 ni ya ujenzi wa mabwawa na 103 ni ya ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji.

#Maeneo ya kipaumbele katika Mwaka wa Fedha 2023/2024. Kukamilisha ujenzi wa skimu mpya 25 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023, kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu 30 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023;

#Kukamilisha ujenzi wa mabwawa 14 yenye mita za ujazo 131,535,000 yaliyoanza kujengwa Mwaka 2022/2023, kukamilisha usanifu wa mabonde 22 ya Umwagiliaji ulioanza Mwaka 2022/2023;

#Kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye mabonde 22 yenye jumla ya hekta 306,361, kuanza ujenzi wa skimu mpya 35 zenye jumla ya hekta 111,390;

#Kukarabati miundombinu ya umwagiliaji katika Skimu 24 zenye jumla ya hekta 32,092; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa mapya 100 yenye wastani wa mita za ujazo 936,535,700 na kuanza ujenzi wa mabwawa hayo.

#Kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya pamoja (Block farms) yenye jumla ya hekta 79,518.46 katika Mikoa ya Kigoma, Njombe, Mbeya, Kagera na Dodoma kupitia programu ya Building Better Tomorrow (BBT);

#Kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa skimu mpya za umwagiliaji 236 zenye ukubwa wa hekta 415,811, kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa skimu 255 za ukarabati zenye ukubwa wa hekta 291,095 na kuanza kuchimba visima vya umwagiliaji 150 kwa kila halmashauri.

#Ili kutekeleza maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa hapo juu, Tume imeidhinishiwa na Bunge kiasi cha Shilingi 373,511,998,000/= kwa ajili ya mwaka wa fedha 2023/2024.

#Kati ya Fedha hizo, miradi ya maendeleo Shilingi 299,964,223,000 /= (80.3%) na, matumizi ya Kawaida Shilingi 73,547,775,000 (19.7%).

*Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO*









Wanahabari wakiwajibika



Mkurugenzi Reymond Mndolwa, akiwasikiliza wanahabari wakitoa ushauri
 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA