HAKUNA UHABA WA DAMU SALAMA UNAOITESA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA -BOMBO

Na Mwandishi Wetu, TANGA.

UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo umesema hakuna uhaba wa damu kama ilivyoandikwa na mmoja ya gazeti kwamba unaitesa kutokana na uwepo wa jitihada mbalimbali

Jitihada hizo ni pamoja na kutumia taasisi mbalimbali za kiserikali na kidini kuhamasishaji wa kuchangia kwa hiari jambo ambalo limekuwa likifanyika kwa nyakati tofauti tofauti na limekuwa na mwamko mzuri wa wananchi kuchangia

Pia katika taarifa hiyo iliyotoka kwenye chombo hicho cha habari ilionekana kuwa na mapungufu kwa kukosa mikakati iliyoelezewa wakati wa halfa hiyo.

Akizungumza leo na waandishi wa Habari Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo-Dkt Naima Yusuf alisema kwamba uhaba upo lakini hospitali imeweka mchakato wa upatikanaji wa damu kwa wakati kupitia uchangishaji katika halfa mbalimbali.

 Alisema sio kwamba uhaba wa damu unaitesa hapana bali kuna mpango ambao upo kwa upatikanaji wa damu kwa mwaka na bado wanasisitiza wananchi kujitokeza kuja kuchangia kwa hiari.

 “Sio kwamba uhaba wa damu unaitesa Hospitali ya Rufaa ya Bombo Lakini pia wagonjwa wanapohitaji damu wanapata kwa wakati”Alisema

Awali akizungumza Mkuu wa Idara ya Maabara katika Hospitali hiyo Sinde Mtobu alisema kwamba wastani wa matumizi kwa mwezi ni chupa za damu 500 mpaka 600 na wanakusanya kwa wananchi chupa 300 mpaka 400.

Katika kukabiliana na uhaba huo wakati mwengine kituo cha damu salama kutoka Kanda ya Kaskazini wanapopewa taarifa wanakuwa tayari kusaidia kwa ajili ya kutosheleza mahitaji kwa wakati husika.

 Alisema hivyo wanapungukiwa chupa 200 na sio kila mwezi kuna wakati mwengine wanakuwa na damu nzuri inatosheleza hivyo ni wastani tu huku jitihada ya Taasisi na wadau kwa kuzunguka kwenye Taasisi za Umma kuchangisha damu kwenye shule za Sekondari za Umma na Serikali.

Aidha alisema wananchi wanafika kuchangia damu kwenye kituo chao cha bombo ikiwemo baadhi ya jamii ndugu zikiwemo taasisi za dini,Jai  na Bilali Muslim ambazo wanashirikiana na viongozi wa kisiasa kutafuta njia ya kuweza kuwasaidia kupata damu muda wote.

“Taasisi zipo nyingi Tanga kila taasisi yenye watu kila mwaka mara moja inaweza kutuunga mkono kuchangia damu kwa kutoa kalenda yao nasi tutashirikiana nao kuhakikisha tunakwenda kuendesha zoezi la kuchangia damu”Alisema Mtobu.

Hata hivyo alisema kwamba wanawashukuru Tanga Uwasa kwa kuchangia damu ikiwemo Kanisa la Wasabato na KKKT huku akiendelea kuisa taasisi nyengine kwa niaba ya hospitali zikiwa na matukio mengine zitusaidie ili waweze kuendelea kuwahudumia wagonjwa.
Imetolewa na Kitengo cha Habari cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo

 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA