HUDUMA ZA MAJI SAFI NA MAJI TAKA TUMEZIBORESHA SANA JIJINI DODOMA--MHANDISI ARON

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo alipokuwa akizungumza uboreshaji wa huduma zinazotolewa na mamlaka hiyi kuwahudumia wananchi wa jiji hili ambalo ndilo makao makuu ya nchi. Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba Jukumu la msingi la DUWASA ni kutoa huduma ya majisafi na uondoaji majitaka
kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na miji ya Chamwino, Kongwa na Bahi. Kwa sasa Jiji la Dodoma lina wakazi 765,179 (Sensa.2022) ambapo takribani
91% wanapata huduma ya Majisafi na salama (Kwa Mgao) na 20% huduma ya
uondoshaji Majitaka. Mahitaji ya Maji ya Jiji la Dodoma kwa sasa
ni lita 133,400,000 kwa siku, na yataongezeka hadi lita 417,308,000 kwa
siku (Mwaka 2051)., HEBU FUATANA NA MIMI HAPO CHINI UJIONEE VIZURI HABARI YAKE KWA WANADODOMA



Mhandisi Aron akiwafafanulia mambo wanahabari


Wanahabari wakiwajibika wakati wakimsikiliza mkurugenzi


@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 Jukumu la msingi la DUWASA ni kutoa
huduma ya majisafi na uondoaji majitaka
kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na miji ya
Chamwino, Kongwa na Bahi. Kwa sasa Jiji la Dodoma lina wakazi
765,179 (Sensa.2022) ambapo takribani
91% wanapata huduma ya Majisafi na
salama (Kwa Mgao) na 20% huduma ya
uondoshaji Majitaka. Mahitaji ya Maji ya Jiji la Dodoma kwa sasa
ni lita 133,400,000 kwa siku, na
yataongezeka hadi lita 417,308,000 kwa
siku (Mwaka 2051).

 Uwezo wa vyanzo vyote vya maji vya
DUWASA ni lita 67,100,00 kwa siku Upungufu wa mahitaji ya maji ni lita
66,300,000 kwa siku (50%) Mahitaji ya mfumo wa kutibu Majitaka
ni lita 20,000,000 kwa siku Uwezo wa mfumo wa kutibu Majitaka
ni lita 350,000 kwa siku Upungufu wa uwezo wa kutibu
Majitaka ni lita 19,650,000 kwa siku

Majisafi Katika kukabiliana na ongezeko kubwa la
mahitaji ya Maji jijini Dodoma, Serikali
kupitia Wizara ya Maji na DUWASA
imewekeza kiasi cha Tsh. 9.14bilioni kwa
hatua za muda mfupi za kupunguza uhaba
wa maji;
Hatua za muda mfupi (Kazi zilizofanyika) Uchimbaji na uendelezaji wa visima (32)
sehemu mbalimbali za huduma, ufungaji wa
pumpu, ulazaji wa kilometa 208.86 za
mtandao wa kusafirishia na kusambazia
maji, ujenzi wa Matenki yenye ujazo wa lita
3,035,000, n.k
Matokeo ya hatua za muda Mfupi Dodoma:Uzalishaji umeongezeka kutoka
Lita Mil. 61.5 na kufika 67.1 kwa siku. Chamwino:Upatikanaji wa maji
Umeongezeka kutoka 42% mpaka 87% Kongwa:Upatikanaji wa maji
Umeongezeka kutoka 44% hadi 88% Bahi: Upatikanaji wa maji
Umeongezeka kutoka 37%
hadi 95%
2.0 MAFANIKIO KATIKA HUDUMA...
(b) Majitaka Serikali imetenga kiasi cha 4.9bn kwaajili
ya kukarabati wa mtandao wa majitaka
eneo la Area D na C;  Kubadili kilomita 19 za mtandao
chakavu  Ujenzi wa Chamba 1,005  Kuhamishia wateja wote kwenye
mtandao mpya Hadi sasa, mradi huo umefikia asilimia
86 ya utekelezaji.
2.0 MAFANIKIO KATIKA HUDUMA...
3.0 MIPANGO YA KUBORESHA HUDUMA
(a) Majisafi
✓ Serikali imetenga kiasi cha 23.8Bilion kuendeleza hatua
za muda mfupi ili kupunguza adha ya upatikanaji wa
maji Dodoma kwa kuchimba visima maeneo ya; Nzuguni,
Bihawana na Zuzu. Kazi zitakazofanyika ni;  Nzuguni: Tsh. 5.8bn na itaongeza uzalishaji kwa
11.3%  Zuzu-Nala: Tsh. 7.8bn na itaongeza uzalishaji kwa
10%  Bihawana: Tsh. 10.2bn na itaongeza uzalishaji kwa
15.2%  Kongwa: Tsh. 68Mil. Kuongeza uwezo wa Chemchem,  Chamwino: Mradi wa Miji 28
✓ Muda wa Kati & Mrefu  Bwawa la Farkwa
• Mradi unakadiriwa kugharimu kiasi cha
$ 793.31 Milion
• Tayari Serikali imetenga Dola 125.3
kwa ajili ya kujenga Bwawa na Mtambo
wa Kutibu Maji kupitia AfDB.
• Mradi huu utaongeza kiasi cha Maji lita
Milioni 128 kwa Siku.
• Mradi upo katika hatua za kuwapata
wahandisi washauri wa mradi.
3.0 MIPANGO YA KUBORESHA HUDUMA...
✓ Muda wa Kati & Mrefu....  Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria
• Upembuzi wa awali (Pre-Feasibility
Study) ulifanyika na kukamilika mwezi
Desemba, 2019 umeonesha uwezekano
mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria kufika
Dodoma.
• Mradi huu unalenga kuhudumia Mji wa
Dodoma na Singida.
• Mradi upo katika hatua za kumpata
mhandisi Mshauri.
3.0 MIPANGO YA KUBORESHA HUDUMA...
✓ Mpango wa Dharula  Mradi wa Maji kutoka Bwawa la Mtera
• Unatarajiwa kuleta maji Lita Mil. 130 kwa
Siku.
• Mhandisi mshauri kampuni ya M/S Khatib &
Alami Consulting tayari yupo site anaendelea
kufanya upembuzi na tayari amewasilisha
inception report October 2022.
• Jumla ya Tsh. 326 Bilioni zitatumika na benki
ya Dunia imeonesha nia kufadhili mradi huu.
• Mhandisi mshauri atawasilisha taarifa yake
ya mwisho Mwezi Machi 2023.
• Mradi huu unaweza kujengwa ndani ya
kipindi cha miaka 2.
3.0 MIPANGO YA KUBORESHA HUDUMA...

(b) Majitaka  Mradi wa Ujenzi wa uboreshaji wa
huduma ya majitaka Jijini Dodoma (EDCF-
Korea);
• Una gharama ya Dola Mil. 70
• Utajenga mabwawa mapya 16
• Utatibu majitaka lita mil. 20 kwa siku
• Mtandao wa mabomba 250km
• Kuunganisha wateja wapya takribani
6,000
• Tathmini (Evaluation) ya kumpata
mhandisi mshauri imekamilika Mwezi
Oktoba 2022 na imetumwa EDCF-Korea
kwa ajili ya Kibali (No Objection).
3.0 MIPANGO YA KUBORESHA HUDUMA...
(b) Majitaka...  Ujenzi wa mtandao wa majisafi na majitaka
Mji wa Serikali – Mtumba
• Unahusisha ujenzi wa mtandao wa majisafi
(8.5km) na majitaka (~52km) katika mji wa
Serikali
• Ujenzi wa mabwawa ya kutibia majitaka
eneo la chang’ombe – Buigiri
• Mhandisi mshauri ameshafanya mapitio ya
usanifu na kuwasilisha Draft design ya mradi.
• DUWASA inaendelea kupitia usanifu huu kwa
ajili ya kutoa maoni kwa mhandisi mshauri.
• Mradi huu unatarajiwa kugharimu Tsh. 95
Bilioni mpaka kukamilika kwake.
3.0 MIPANGO YA KUBORESHA HUDUMA...

4.0 HITIMISHO
DUWASA inaendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kuitazama Dodoma kwa umuhimu wake na kuiwezesha katika
uwekezaji wa miradi mbalimbali.
ASANTENI SANA
“Kazi iendelee




Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA