Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii kwenye Mahafali ya 52 ya Duru ya Tano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada
ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City
tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa
Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia
na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa
Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na
mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika
kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja
na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya
Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa
katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30,
Novemba, 2022.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya
Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi
wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizungumza katika
Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30,
Novemba, 2022.
Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Balozi Mwanaidi Sinare
Maajar akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya
Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye
akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City
tarehe 30, Novemba, 2022.
Wahitimu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika Mahafali ya Hamsini na
mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika
kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wahitimu mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye pamoja na Wahitimu wengine wakiwa kwenye Maandamano ya kuelekea ndani ya ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika tarehe 30, Novemba, 2022.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amevitaka Vyuo Vikuu nchini kutimiza wajibu wake wa kutoa mchango katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Juu ya Heshima ya Udaktari (Doctor of Letters Honoris Causa) ya Chuo Kikuu cha Dar es katika Mahafali ya 52 ya Chuo hicho yaliyofanyika Novemba 30, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais ameongeza kuwa jukumu la Taasisi za elimu ya juu katika kuleta maendeleo ni kutoa elimu stahiki, kufanya tafiti na kutoa maoni katika mwenendo wa kulikuza na kuimarisha Taifa.
“Tangu kuingia madarakani Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikisisitiza kuwa elimu inayotolewa inapaswa kukidhi mahitaji ya jamii katika karne ya 21,”amesema Rais Samia
Ameongeza kuwa mbali ya kuongeza maarifa elimu inayotolewa katika Taasisi za elimu inapaswa kuwawezesha wahitimu kuwa na stadi zitakazowawezesha kujiajiri, kuajiriwa ama kuwa wajasiliamali na kuwa tayari kuchangia maendeleo ya Taifa wanapohitimu masomo.
Akizungumza katika Mahafali hayo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema kuwa tayari Wizara imekamilisha Mapitio ya Sera na Mitaala na kwa sasa hatua inayofuata ni kuyawasilisha kwenye vikao vya ndani vya Serikali kabla ya mjadala wa wazi wa kitaifa kuhusu maoni na mapendekezo hayo.
Kuhusu uboreshaji wa elimu ya juu Prof. Mkenda amesema katika kujenga mazingira mazuri ya utoaji wa elimu ya juu, Serikali kupitia mradi wa HEET itatumia Dola za Kimarekani 425 sawa na fedha za kitanzania Bilioni 972 kupanua na kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika fani za kipaumbele cha Taifa.
Ameongeza kuwa Mradi unatekelezwa katika Vyuo Vikuu 14 vya Serikali,Taasisi 3 za Wizara zinazoshughulikia Elimu ya Juu na Taasisi 5 za Elimu ya Juu zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Aidha, Prof. Mkenda amesema utekelezaji wa Mradi huo utaongeza udahili katika Fani za kipaumbele cha Taifa kutoka 40,000 mwaka 2020 hadi kufikia 100,600 mwaka 2026.
Kuhusu ufadhili wa masomo ya Elimu ya Juu, Waziri huyo amesema Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu mfululizo kila mwaka ambapo bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/18 ilikuwa shilingi bilioni 427 lakini kwa Mwaka wa fedha 2022/23 bajeti hiyo imefikia Shilingi bilioni 654.
Ameongeza kuwa na kama hiyo haitoshi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanzisha ufadhili ujulikanao Samia Scholarship kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi na kwamba jumla ya shilingi Bilioni tatu zimetengwa kwa mwaka wa 2022/2023 kwa ajili ya wanafunzi 640.
Comments
Post a Comment