Kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote yapata washindi 51
Mshindi wa Kampeni ya matumizi ya NMB Mastercard (Master bata kotekote) Bernard Matiku(kulia) akipokea funguo wa pikipiki kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Baraka ladislaus wakati wa hafla ya kukabidhiwa iliyofanyika jana, kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya kadi NMB Filbert Casmir.Na Mpigapicha Wetu
Mshindi wa Kampeni ya matumizi ya Masrercard(Master bata kotekote) Bernard Matiku(wa pili kushoto) akibonyeza kitufe ili kuwapata washindi wengine wa kampeni hiyo, wakati wa kukabidhiwa pikipiki yake, kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB Filbert Casmir Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Baraka Ladislaus(wa tatu kushoto) na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Erick Mremi(kulia) wakishuhudia.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Na Mwandishi Wetu
Msimu wa nne wa promosheni ya NMB MastaBata kwa ajili ya kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za kidijitali umezidi kunoga baada ya kundi la kwanza la washindi 51 wa kila Mwezi kupatikana wiki hii.
Washindi hao ambao 49 walishinda pesa taslimu TZS 1,000,000 kila mmoja na wawili wakishinda pikipiki aina ya Boxer walipatikana Jumatano katika droo iliyofanyika kwenye tawi la NMB Kenyatta mkoani Mwanza.
Zoezi hilo lililosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubashiri Tanzania limepelekea idadi ya washindi wa kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote kufikia 225 hadi sasa. Zawadi walizoshinda wateja hao kwa siku hii zina thamani ya zaidi ya TZS milioni 55 huku shindano zima likiwa na thamani ya zaidi ya TZS milioni 300.
“Ninafuraha Sana kushinda pilipili nzuri ya boxer. Nimehamasika Sana kutumia kadi za NMB Mastercard na NMB Mastercard QR kufanya miamala kitu ambacho mimi nakifanya mara kwa mara sasa hivi na mumeweza shinda mara ya pili,”Bw Bonnard Lucas Matiku mkazi Bunda huko Mara ambaye amechukua pikipiki moja inayotolewa kila wiki.
Mkazi huyo wa Bunda alijibu hivyo na kuonyesha thamani ya promosheni ya MastaBata baada ya kuulizwa na meneja wa Kanda ya Ziwa, Bw Baraka Ladisluas wakati WA makabidhiano.
“Lengo la kampeni hii ya MastaBata, Kote-Kote! kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake ni kuhamasisha matumizi ya kadi za malipo za benki yetu za NMB Mastercard na NMB Mastercard QR kila wateja wetu wanapofanya malipo na manunuzi,” Meneja Baraka alibainisha kabla ya kuchezesha droo ya tatu.
Droo ya kwanza ilifanyika kwenye tawi la NMB la Mlimani City jijini Dar es Salaam, ya pili huko Iringa na ya Tatu Kibaha. Katika droo zote tatu, benki hiyo iliwazawadia wateja 75 wa kila droo kiasi cha TZS 100,000 kwa kila mshindi. Pia kila wiki kuna mshindi wa Boxer moja yenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 3.
Zawadi za kila mwezi zitakuwerpo mara mbili ambapo jumla ya washindi 98 watanyakua pesa taslimu TZS milioni moja kila mmoja huku kila mwezi kukiwepo zawadi ya Boxer mbili. Zawadi ya droo ya mwisho ni safari ya siku nne huko Dubai kwa washindi saba na wenza wao.
“Promosheni hii itaendelea hadi mwezi Januari mwakani kwa hiyo fursa na nafasi ya kujinyakulia zawadi mbalimbali bado ipo kwa wateja wetu ambao wanafanya miamala yao kwa kutumia kadi za malipo za NMB Mastercard na NMB Mastaercard QR,” Mkuu wa Biashara ya Kadi wa benki hiyo, Bw Philbert Casmir alisema.
Mbali ya kuhamasisha kufanya malipo kidijitali, alibainisha, kampeni ya MastaBata imekuwa sehemu ya utamaduni wa NMB kuwazawadia wateja wake kila mwisho wa mwaka. Promosheni hiyo ilianzishwa mwaka 2018.
Bw Casmir aliwasihi Watanzania kuacha matumizi ya pesa taslimu kwenye malipo na kufanya hivyo kidijitali zaidi, kama inavyoelekezwa kwenye ajenda ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kisasa wa kidijitali.
Comments
Post a Comment