*JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA*
*JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA*
AINA ZA WASUKUMA NA KISUKUMA
Lugha ya kisukuma ina lahaja kuu nne; *ginantuzu,* *ginang'weli,* *ginangw'agala* na *gidakama*. Vivyo hivyo, Wasukuma wamegawanyika katika *misingi ya lahaja za lugha ya kisukuma.*
1.
*Bhadakama*. Hawa wanapatikana sehemu za mji wa Shinyanga, sehemu za Gahama na sehemu za Igunga na Nzega. Kwa idadi, hawa ndiyo Wasukuma wachache sana. Ni watu wenye aibu, wakimya mno... wana muingiliano na utamaduni wa Wanyamwezi. Pengine hawa ndiyo Wasukuma masikini kuliko aina yoyote ya Wasukuma!
2.
*Bhanang'weli.*
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa mikoa ya Mwanza, Geita, na kusini - Magharibi mwa Mkoa wa SIMIYU. Kiidadi, hawa ndiyo Wasukuma wengi sana... katika ongea yao, wana matumizi mengi ya 'shi' kwa mfano, shikolo, shiliwa. Pia hawatumii 'ng'wadila' katika salamu za jioni. Wao hutumia 'gawiza' au 'dillo gawiza' Kwa sababu wanaishi katika strategic areas, wana muingiliano na watu wa makabila mbalimbali. Au tuseme wamemezwa na watu wa kuja. Ukienda Geita wenyeji hawaonekani, labda kukimbiza daladala za baiskeli. Mwanza ndiyo usiseme kabisa.
3.
*Bhanang'wagalla*.
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa Wilaya za Meatu, Kishapu na Maswa na sehemu za Igunga. Ukikutana nao ni rahisi mno kuwasikia wakisema, 'yombaga bhahebhu', ong'wawiya, kaaa, aghayaa... ni nadra sana kuwasikia wakisalimia, 'ng'wadila' Wao hufupisha, 'dilla mayu' au dilla bhabha. Majina ya maeneo mengi huanza na Ng'wa. Kwa mfano, ng'wabagimu, ng'wajidalala, ng'wanhuzi... Utajiri wao uko kwenye mifugo.
Vijana wa huko hulizika mapema. Kwa mfano, kama mavuno ya matobholwa, karanga, alizeti na pamba ni mazuri, vijana wa maeneo haya hushinda kwenye ngoma za jadi. Hawajui kusaka ridhiki nje ya maeneo yao, utafikiri wako kisiwani. Wanaotoka nje ya maeneo yao ni wafugaji tu. Wanawake wa huko hupenda kuvaa shanga kiunoni na shingoni ingawa sio wajuzi wa mambo ya Tanga. Wavulana nao huvaa miguuni. Soko la wasichana liko juu sana. Pengine huu ukanda, hasa Meatu, ndiyo unaongoza kwa kutoa mahari kubwa Tanzania nzima.
4.
*Bhanantuzu /Wanyantuzu*
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa Wilaya za Bariadi na Itilima. Hawa ndiyo Wasukuma waliotapakaa kila kona ya nchi hii. Na pengine bila ya hawa kabila la Wasukuma
lisingejulikana kwa namna hii. Kisukuma chao hakina 'shi' bali hutumia 'si' kwa mfano, sikolo, siliwa....Jamaa hawa wanajua kuchakalika kutafuta mali. Hawaogopi kitu, hawaogopi mtu. Jamaa hawa ndiyo Wasukuma pekee wanaothubutu kwenda kupora ng'ombe za Wamasaai. Ni Wasukuma wenye dharau na mikogo mingi. Kama unasikia watu wanaopenda utani na masihara, basi hawa ni kiboko. Si unamjua Danni Makanga? Mambo ya ujanja ujanja na upigaji dili, hapa ndipo penyewe. We mwangalie Chenge tu, au hata Cheyo au hata Mbunge Njaru. Utanipa jibu. Wanaume wa huko hupenda kuoa wake weupe. Kama sio mweupe basi awe na sifa za ziada. Michepuko kwa mwanaume ni kitu cha kawaida
*Ngwabeja bakoi* Asanteni.
Comments
Post a Comment