*JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA*
Vijana wa Kisukuma wakichunga mifugo yao *JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA* AINA ZA WASUKUMA NA KISUKUMA Lugha ya kisukuma ina lahaja kuu nne; *ginantuzu,* *ginang'weli,* *ginangw'agala* na *gidakama*. Vivyo hivyo, Wasukuma wamegawanyika katika *misingi ya lahaja za lugha ya kisukuma.* 1. *Bhadakama*. Hawa wanapatikana sehemu za mji wa Shinyanga, sehemu za Gahama na sehemu za Igunga na Nzega. Kwa idadi, hawa ndiyo Wasukuma wachache sana. Ni watu wenye aibu, wakimya mno... wana muingiliano na utamaduni wa Wanyamwezi. Pengine hawa ndiyo Wasukuma masikini kuliko aina yoyote ya Wasukuma! 2. *Bhanang'weli.* Hawa ni Wasukuma wenyeji wa mikoa ya Mwanza, Geita, na kusini - Magharibi mwa Mkoa wa SIMIYU. Kiidadi, hawa ndiyo Wasukuma wengi sana... katika ongea yao, wana matumizi mengi ya 'shi' kwa mfano, shikolo, shiliwa. Pia hawatumii 'ng'wadila' katika salamu za jioni. Wao hutumia 'gawiza' au 'dillo gawiza' Kwa sababu wanaishi katika strat