SHEIN AANZISHA MJADALA WA KUHUSU MASUALA YA WAZEE NCHINI LEO DODOMA

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt, Ally Mohamed Shein, leo jijini Dodoma amefungua mjadala wa wazee nchini , akisema hakuna aseti kubwa katika Taifa lolote bila wazee,  na nchi bila wazee ni kama taifa la wafu, amewataka vijana wale kuwapenda wazee wao kwani hata wao wakumbuke ni wazee wa kesho. Aidha amelaani tabia ya kuwashambulia wazee na wengine kuwashambulia na kuwasababishia mauti kwa kisingizio ni wachawi na sababu mbalimbali ambazo yeye ameziita hazina sababu  za msingi. Wazee wengi wa vijiji hasa katika nchi zetu za kiafrika hukumbwa na masahibu mengi baadhi kutokana na kutokuwa na nishati ya kueleweka hupikia kuni katika maisha yao yote na kusababisha baadhi kuwa na macho mekundu , mzee anapoonekana anamacho mekundu hudhaniwa ni mchawi kibaya zaidi hata katika familia yake hudhaniwa hivyo na baadhi kukimbia makazi yao kwenda kusikojulikana.. Rais huyo msaatu amesema muda umefika sasa kuwa na majadala wazee watunzweje  ili kuondokana na manyanyaso hayo katika nchi zao. Mjadala huo ambao unahudhuliwa na washiriki kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Tanzania bara na Visiwani imedhaminiwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Help Age na Taasisi ya Mwalimu Nyerere









Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku,akimpongeza Rais Mstaafu Dkt. Ali Mohamed Shein, baada ya kuhutubia








Baadhi ya wazee waliohudhulia

Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashiriki ya  kuhudumia Wazee Tanzania Clotilda Kokupima, akizungumza akitoa shukurani zakw kwa Rais Mstaafu kwa utawala wake huko Zanizbar kwa kufanikisha kuwajengea makazi bora wazee na kuwapa penshini nzuri.



Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, akizungumza katika mjadala huo





Butiku na Sheini wakiteta

Picha ya pamoja na watoa mada

Picha na Wabunge waliohudhulia






















Wabunge waliohudhulia wakibadilishana mawazo, Nyongo, Kikoyo na Makamba

Mtoa mada Jenerali Ulimwengu, akibadilisha mawazo na wenzake


 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA