MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI NGOGWA -KITWANA KAHAMA

 



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akimtwisha Ndoo ya Maji Mwanamke, mara baada ya kumaliza kuzindua Mradi wa Majisafi na Salama kutoka Ziwa Victoria wa Ngogwa-Kitwana katika Manispaa ya Kahama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amezindua Mradi wa Majisafi na Salama kutoka Ziwa Victoria wa Ngogwa-Kitwana Manispaa ya Kahama, ambao umewaondolea adha wananchi ya kutumia Maji yasiyofaa kiafya.

Mradi huo wa Majisafi na salama umezinduliwa leo Julai 30, 2022 na Mwenge wa Uhuru, Mradi ambao ulikuwa ukitekelezwa na Mamlaka mbili za Maji (SHUWASA), (KUWASA) pamoja na Wakala wa Maji vijijini (RUWASA) wilayani Kahama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi huo wa Maji,Sahili  amewapongeza (SHUWASA) na kubainisha kuwa Mradi huo ni mzuri ambao umewaondolea adha wananchi ya matumizi ya Maji yasiyo salama.


“Mradi huu wa Maji nimeukagua ni mzuri, naomba wananchi muitunze miundombinu yake ili na nyie uwatunze na kuendelea kupata huduma ya Majisafi na salama kwa muda mrefu,” amesema Geraruma.

Amewataka pia wananchi ili kutekeleza dhamira ya kumtua Ndoo kichwani ya Maji Mwanamke, wanapaswa kuvuta Maji hayo majumbani mwao, na kuachana na dhana ya kuchota Maji kwenye vituo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, amesema mradi huo umetekelezwa katika muda muafaka, ambapo kwa sasa kuna hali ya ukame, na kuwaomba wananchi waupokee mradi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, amesema mradi huo ulianza mwaka 2020 na umekamilika Mei mwaka huu.

Amesema mradi huo wa Maji utanufaisha wananchi 44,618 na umegharimu kiasi cha fedha Sh. bilioni 2.9.

Nao baadhi ya wananchi walionufaika na mradi huo wa Maji wameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo na kuwaondolea adha ambayo walikuwa wakiipata kutokana na ukosefu wa Majisafi na salama maeneo hayo.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa (2022)Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa majisafi na Salama wa Ngogwa-Kitwana Manispaa ya Kahama.

Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa Majisafi na Salama wa Ngogwa-Kitwana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa Maji Ngogwa-Kitwana.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa (2022)Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata utepe kuzindua Mradi wa Majisafi na salama wa Ngogwa-Kitwana Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa (2022)Sahili Nyanzabara Geraruma, akizindua mradi wa Majisafi na salama wa Ngogwa-Kitwana Manispaa ya Kahama.

Jiwe la uzinduzi wa mradi wa Majisafi na salama wa Ngongwa-Kitwana Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa (2022)Sahili Nyanzabara Geraruma, akifungua bomba la maji ili kuhakikisha kama maji yanatoka kwenye mradi huo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akimtwisha Ndoo ya Maji Mwanamke mara baada ya kumaliza kuzindua mradi wa Majisafi na Salama kutoka Ziwa Victoria wa Ngogwa-Kitwana katika Manispaa ya Kahama.

Bango la kuukaribisha Mwenge wa Uhuru kuzindua Mradi wa Majisafi na Salama wa Ngogwa-Kitwana Manispaa ya

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA