NMB YAWATAKA WENYE ULEMAVU KUJIAMINI
Afisa Mkuu wa Rasilimali watu benki ya NMB, Emmanuel Akonaay akiwasilisha mada kwenye mkutano mkuu wa Kitaifa wa Wafanyakazi wenye ulemavu nchini uliofanyika Jijini Dodoma. NMB ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo uliolenga kujadili upatikanaji wa stahiki bora haki ya kuajiriwa na mazingira rafiki ya kazi kwa watu wenye ulemavu.Na Mpigapicha Wetu
Mwandishi Wetu
Dodoma.Sababu kuu tatu zimetajwa kuwa changamoto ya kuwakosesha ajira watu wenye ulemavu nchini licha ya kuwa wanakuwa na sifa zinazotastahili.
Sababu hizo zilitolewa jana Jijini Dodoma na Afisa Mkuu wa Rasilimali watu katika benki ya NMB Emmanuel Akonaay kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa wafanyakazi wenye ulemavu ulioitishwa na taasisi ya Ikupa Trust huku NMB wakiwa moja ya wadhamini.
Akonaay alitoa kauli hiyo alipozungumza kwa niaba ya waajiri juu ya changamoto wanazokutana nazo wakati wa kuajiri kwani wenye ulemavu huwa wachache ingawa alisema ndani ya NMB wenye ulemavu wapo.
Afisa Mkuu wa Rasilimali watu katika benki ya NMB Emmanuel Akonaay alizitaja baadhi ya changamoto hizo ni kutojiamini hivyo kushindwa kutuma maombi ya kazi.
Nyingine ni wenye ulemavu kutokuwa na ari ya kujitolea na kukosekana kwa kanzi data ya wenye ulemavu ili kuwatambua katika uwezo wao.
Afisa huyo alisema NMB tangu mwaka jana walianzisha program ya kuwasaidia watu 200 kwa ajili ya masomo kutoka kaya za wasiojiweza wakiwemo wenye ulemavu lakini mwaka huu benki itadhamini vijana 50 kwenye masomo ya vyuo vikuu moja kwa moja.
“Lakini pia nitoe Rai kwenu nanyi wenye ulemavu, nashauri muwe na udhubutu, tujiamini na tufanye kazi kwa bidiiiii. Ila msiishie hapo tu...jengeni utamaduni wa kuwa washauri wa vijana mashuleni na vyuoni ili muweze kuwajengea uwezo wa kujiamini wanapomaliza masomo,”alisema Akonaay.
NMB tunao watu wenye ulemavu na wanajituma sana. Kutokana na uwezo wao wameza kupanda vyeo ndani ya benki Na tumefanikiwa kuweka mazingira mazuri kufanya KAZI zao vizuri. Na ndio maana tumeshiriki kikamilifu kwenye mtukano huu wenye kauli mbiu inayosema "Stahiki bora haki ya kuajiriwa na mazingira rafiki ya kazi kwa watu wenye ulemavu."
Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi aliziomba taasisi za fedha kuendelea kuwaamini wenye ulemavu na kutimiza matakwa yao si kwa kuomba bali kwa haki.
Katambi aliagiza kwa Serikali, taasisi na mashirika yote kuanzia sasa kutopitisha ramani zote za majengo kama hazitakuwa na ujenzi wa miundombinu rafiki kwa wenye ulemavu.
Kuhusu asilimia tatu katika nafasi za ajira, alisema kuanzia sasa Wizara hiyo itafuatilia kila mahali kuona kama takwa hilo linatekelezwa na itakapobidi hatua zitachukuliwa ili kuziba nafasi hizo kwani wenye ulemavu wenye sifa wapo.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Ikupa Trust, Stella Ikupa alisema kundi hilo linakutana na changamoto nyingi lakini wanalilia utekelezaji wa sheria ambayo inasema kila walipo watumishi 20, lazima asilimia tatu yao iwe ni wenye ulemavu.
Ikupa alisema tatizo la miundombinu ni kubwa hasa katika majengo ya Serikali ikiwemo vyoo ambapo huwafanya baadhi ya wenye ulemavu kulazimika kushinda njaa au kutokunywa maji kutwa nzima wakiwepo kazini wakiogopa kwenda vyooni kwani mazingira si rafiki.
Kwa upande mwingine Ikupa alizishukuru taasisi za fedha ikiwemo NMB kwamba wamekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wenye ulemavu ikiwemo Tasisi ya Ikupa Trust.
Mwisho,…..
Comments
Post a Comment