WAZIRI MKUU MAJALIWA NA NAIBU SPIKA ZUNGU WAWASIFU REA NA TANESCO

Mkurugenzi Mkuu REA, Mhandisi Hassan Said (kulia), akimweleza Naibu Spika Azan Zungu jinsi walivyojipanga kufika umeme katika vijiji vyote nchini, baada ya kutembelea banda lake lililokuwa katika wiki ya Maonyesho ya Majukumu ya Wizara ya Nishati yaliyomalizika leo jijini Dodoma na kutia fola ambapo wabunge zaidi ya 100 waliyatembelea na kusifu ubunifu huo. Wengi wamemsifu Waziri January Makamba na wasaidizi wake  kwa kukata kiu ya wabunge kutaka kufahamu ni lini majimbo yao yatakuwa na umeme wa uhakika hadi vijijini.

Waziri Makamba, akimweleza Naibu Spika jinsi walivyojipanga kukata kiu ya siku nyingi ya wnaanchi  kuwa na umeme wa uhakika
Naibu Spika, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa REA baada ya kumaliza kutembelea banda hilo

Naibu Spika akiagana na Mkurugenzi Mkuu REA, Mhandisi Hassan Said
Waziri Makamba, akimwongoza Naibu SpikaZungu , kutembelea mabanda yaliyopo katika maonyesho
Naibu Spika akimsikiliza Mwakilishi wa TPDC Mhandisi Baltazari Thomas Mroso, jinsi walivyojipanga kutengeneza mifumo ya magari kutumia Gesi asili ili waanze kujiepusha na mafuta ambayo yanadaiwa kuwa adui wa mazingira
Naibu Spika, akisaini vitabu vya wageni ofisini kwa Waziri


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo, akimweleza jambo Naibu Spika baada ya kufika katika banda lake



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mwakilishi wa TPDC Mhandisi Baltazari Thomas Mroso,baada ya kutembelea banda hilo
Mkurugenzi Mkuu Tanesco Mhandisi Maharage Chande (kushoto), akimweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, walivyojipanga kufuta ndoto za kukatika katika kwa umeme nchini na hakutakuwa na mgao tena, alisema mkurugenzi huyo. Amewataka mawaziri wengine kiuga mfano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimmiminia sifa Waziri January Makamba, kwa ubunifu wake na kuweza kukata kiu ya wabunge baada ya kutembelea maonyesho hayo na kulidhika na maneno ya mameneja wa mikoa jinsi wanavyotekeleza majukumu yao majimbo.


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, akizungumza na  mmojaa wa wananchi walitembelea maonyesho hayo
Naibu Waziri wa Nishat Byabato akizungumzia jinsi wizara hiyo na watendaji wake walivyojipangakuwatumikia wananchi wa Tanzania



Waziri Janujary Makamba, akiagana na watendaji wa wizara hiyo waliohudhulia maonyesho hayo na kuwasifu jinsi walivyojitahidi kukata kiu ya wabunge waliowatembelea katika mabanda yao
 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA