SIMBA CEMENT YATOA MIFUKO 3000 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI MKOANI SINGIDA
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi leo katika anayeshughudia ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Mashariki leo katika anayeshughudia ni kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akimkabidhi Msaidizi wake,Abdallah Salimu mifuko hiyo mara baada ya kukabidhiwa anayeshughudia katikati nyuma ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea sehemu ya mifuko ya Saruji 3000 kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi katika kulia anaye shughudia ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akieleza mikakati ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambaye hayupo pichani ambaye alikwenda kiwanda hapo kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya Elimu Jimboni kwake Iramba Magharibi
aziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na vyombo vya habari mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya saruji ambapo alikishukuru kiwanda cha Simba Cement kwa kusaidia sekta ya Elimu Jimboni kwake kuli ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swat
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya Saruji kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya Elimu Jimboni Kwake
Sehemu ya Saruji mifuko 3000 aliyokabidhiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Simba Cement Reinhardt Swat wakitembelea kiwanda hicho kabla ya kukabidhiwa mifuko 3000 ya Saruji Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat kulia akimuonyesha eneo ambalo wanalotumia kwa shughuli za kiwanda Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchema katika ambaye alitembelea kushoto ni Meneja wa kiwanda hicho,Beny Lema Meneja wa Kiwanda cha Simba Cement Beny Lema akimuogoza Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kushuka ngazi mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kulia akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa ajili ya kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu kwenye Jimbo lake la Iramba Magharibi
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Jijini Tanga wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema kushoto akiwa na wafanyakazi wengine wa kiwanda hicho wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba katika akiwa na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia kushoto ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim wakiongia ukumbini kwa ajili ya kupata taarifa.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga ambao nao waliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani katika makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdalla(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI
Mkandarasi
kutoka kampuni ya CHICO kutoka China, Bw. li, akitoa maelezo kwa Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu
hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye
urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiwaonesha
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi na Mbunge wa Jimbo la Igalula
ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, eneo
ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa
kiwango cha lami itajengwa, mkoani Tabora.
Tingatinga
likikata miti kwa ajili ya kusafisha eneo ambapo ujenzi wa barabara ya
Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami utaanza, mkoani
Tabora.
Serikali
imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4
inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO
kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya
katavi na kigoma.
Amesema
hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,
wakati aliposimamishwa na wakazi wa kijiji cha Tura, wilaya ya Uyui,
mkoani Tabora, alipokuwa akikagua kambi ya mkandarasi na kuangalia hatua
za awali za matayarisho ya ujenzi wa barabara hiyo.
Prof.
Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi
bilioni 117.9 na utachukua miezi 24 mpaka kukamilika kwake."Serikali
imeanza rasmi ujenzi wa barabara hii na sasa ni jukumu lenu kuhakikisha
mnampa ushirikiano mkandarasi huyu ili mradi uwahi kukamilika mapema",
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza
biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi
jirani. Ameongeza
kuwa sasa Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya
kutoka daraja la Kikwete mpaka Uvinza, mkoani Kigoma na hivyo itasaidia
wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi kutoka mkoa wa Dar es Salaam mpaka
mikoa ya katavi na Kigoma kupita kwenye lami njia nzima.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Igalula mkoani Tabora ambaye pia ni mjumbe wa kamati
ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa
yeye na timu yake watajitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu
kutohujumu vifaa vya mkandarasi huyo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi, ameishukuru
Serikali kwa mradi unaoendelea katika wilaya hiyo na kumuahidi Waziri
kuwa yeye na kamati ya usalama itahakikisha mkandarasi hahujumiwi.
Awali
akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS),
mkoa wa Tabora Mhandisi DamianNdibalinze, amemueleza Waziri kuwa kazi
imeanza kwani Mkandarasi ameshaanza kuleta vifaa eneo la kazi na ujenzi
wa kambi unaendelea.
Waziri
Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Tabora ikiwa ni
lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea
mkoani humo .
WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.
Pia
Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali
yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua
kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.
Alizindua
kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya
Sekou Toure akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani
Mwanza.
“Serikali
imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo
nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na
kuuza.”
Pia
aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na
Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.
Kwa
upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na
Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga aliishukuru Serikali kwa kutambua
madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.
Bw.
Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya
kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu
yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni
miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha,
aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara
hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile alisema dawa za kulevya
zinasababisha madhara makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa yanachangia
kusambaa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ukimwi na kifua kikuu.
Pia
alisema kwa sasa dawa za methadone zinazotolewa kwa waathirika wa dawa
za kulevya wanazipata kutoka kwa wahisani mbalimbali. Hata hivyo,
Serikali imepanga kuingiza suala hilo katika bajeti ijayo ili ianze
kuagiza yenyewe.
Baadhi
ya vijana waliokuwa wanatumia dawa za kulevya mkoani Mwanza akiwemo,
Nyamizi Sospeter na Abdul Abdallah, waliishukuru Serikali kwa kuanzisha
vituo vya methadone.
Nyamizi
alitumia dawa za kulevya kwa muda wa miaka saba na muda wote huo
alikuwa akiisumbua familia yake kutokana na matukio mbalimbali ya
kihalifu aliyokuwa akiyafanya ili apate fedha za kununulia dawa hizo.
Naye
Abdul Abdallah alisema alitumia dawa za kulevya aina ya heroine kwa
takribani miaka 20 na muda wote huo alikuwa anakaba watu ili apate fedha
za kununulia dawa hizo.
“Naishukuru
Serikali kwa kuanzisha kliniki ya methadone na sasa nimeacha mimi
pamoja na mke wangu. Najiona binadamu maana nilikuwa mwizi, mchafu kwani
nilikuwa nakaa mwezi bila kuoga na hata kutengwa na jamii.”
Kwa
pamoja waathirika hao wa dawa za kulevya waliiomba Serikali kuwasaidia
kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha
kufanya kazi na kupata kipato kitakachowasaidia kuendesha maisha yao.
Awali,
Waziri Mkuu alizindua muongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa
dawa za kulevya (Soba Houses) ambao unalenga kuwawezesha wamiliki wa
nyumba hizo kuziendesha vizuri na kuwasaidia ipasavyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.
RAIS MAGUFULI AWASILI UGANDA, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVEN
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni
mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa
Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini
Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla
ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na ujumbe wake katika Mazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa
Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisaini Kitaabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya
Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya
mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja
na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda.
Kikundi
cha ngoma za Asili cha Masters of ground kutoka Wilaya ya Kyotera,
Masaka nchini Uganda wakitumbuiza baada ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda. PICHA NA IKULU
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA
JESHI
la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.
Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo.
Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed
Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma
mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya
madaraka.
Kamanda
Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe
amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana
na TAKUKURU.Naye
Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema
Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika
akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.
Alisema
Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017
wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya
Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi
ya Mwenyekiti huyo. Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa
kubaini kilipo.
Februari
19, 2019 akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi Waziri Mkuu Kassim
Majaliwaalimsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya
Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.Alichukua
hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake
ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo
na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.
Amesema
Mwanasheria huyo Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya
ukurugenzi aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti
binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.
Waziri
Mkuu alisema Bw. Bahebe aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa
fedha kwa ajili ya kazi ya ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa
na kampuni ya ukandarasi ya Seekevim. Alisema
mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo
aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi
ilikuwa imekwisha tangu Desemba 2015.
Alisema
Mwanasheria alimlipa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na
Halmashauri jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.Hivyo
alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili
ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
DCC LUSHOTO YASITISHA MPANGO WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI
Kamati
ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC) imeamua kusitisha mpango wa
ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lilokuwa lijengwe kwenye eneo
jipya la Kwehangala hadi hapo suluhu ya mgogoro baina ya viongozi wa
halmashauri hiyo itakapopatikana.
Mwenyekiti
wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika
(Pichani Juu) alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuwepo
sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu
ya suala hilo. .
Hivi
karibuni kumekuwepo na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao juu ya wapi
pajengwe majango ya makao makuu ya Halmashauri hiyo. Baadhi
ya viongozi wanadai utaratibu wa fedha za manunuzi haukufuatwa katika
kufikia maamuzi ya kujenga jengo la Halmashauri katika eneo la
Kwehangala na kuacha majengo yaliyokwisha jengwa Bumbuli kwa gharama ya
Sh. milioni 700.
Kutokana na mvutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kikao kiliafiki kisitishe zoezi hilo mpaka maelewano yatakapopatikana."
Wajumbe wameshauri suala la kuhamisha makao makuu lisitishwe hadi hapo
utakapopatikana utangamano,kwani tayari imeonekana kuna mgogoro ambao
umeleta utengano kwa viongozi" Alisema Lugangika .
Mbunge
wa jimbo hilo, January Makamba alikiri kuwepo kwa mvutano huo ambao
alisema hauna tija katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Bumbuli.Makamba
alisema ni vyema kama viongozi wakazungumzia suala la maendeleo
mfano;maji,barabara,umeme,nyumba za watumishi badala ya kila siku
kuzungumzia wapi kujengwe jengo la halmashauri.
Alishauri
kuwa wananchi washirikishwe katika suala hilo, ikiwa ni pamoja na
kuwapa elimu ya kutosha juu ya hoja ya kuhamisha halmashauri kwa kuwa
ndio wenye chombo chao badala ya viongozi kuamua wao pekee.
"Suala
hilo nakubaliana na maoni wa kikao cha DCC tulisitishe kwani kwa sasa
hatuna shida na majengo ya halmashauri kwa sababu majengo tunayo ambayo
hatulipii kodi ya pango. Sasa hivi tuzungumzie maendeleo kwani wananchi
mwaka 2020 hawatatudai majengo ya halmashauri bali watatudai maendeleo
juu ya huduma muhimu za jamii alisema Makamba.
Hivi
karibuni baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo walipiga kura ya
kupitisha azimio la kujenga jengo hilo la halmashauri huku Madiwani nane
wakigoma kupiga kura kwa madai kuwa hawawezi kupiga kura wakati kuna
ukiukwaji wa kanuni na utaratibu ktk kitengo cha manunuzi.
Madiwani
hao nane ambao waligoma kupiga kura kupitisha azimio hilo mnamo January
18 mwaka huu walimuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuingilia
kati mgogoro na kuzuia walichokiita ukiukwaji wa utaratibu wa manunuzi
pamoja na maelekezo mbalimbali ya viongozi juu ya mpango huo.
Pia
walimuomba aingilie kati na kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa fedha
za umma na ukiukwaji wa utaratibu wa uendeshaji wa halmashauri na
kudharau kwa makusudi maelekezo yaliyotolewa na viongozi mbalimbali wa
serikali kuu.
WAMILIKI WA LESENI ZA MADINI WAASWA UONGEZAJI THAMANI YA MADINI
Na Mathias Canal, Mbeya
Wamiliki
wa leseni za madini ya dhababu, vito na mengineyo kote nchini
wametakiwa kuiga mfano wa Ndg Salim Jesa mmiliki wa kiwanda cha Marmo E.
Granite Mines (T) Ltd kinachojishughulisha na kukata, Kusaga na kuuza
mawe kwa kufanya mchakato mzima mpaka bidhaa kukamilika hapa hapa
nchini.
Kauli
hiyo kwa wamiliki wa leseni za madini nchini imetolewa leo 20 Februari
2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati
akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara ya
kikazi Mkoani Mbeya.
Alisema
kuwa kiu ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ni kuona rasilimali
za nchi zinaongezwa thamani zikiwa ndani ya nchi jambo ambalo linaakisi
umakini wa utendaji na ulipaji kodi ya serikali pasina kukwepa ama
kutorosha rasilimali madini yakiwa ghafi.
Aliseama
kuwa faida ya kuongeza thamani ya madini nchini ndio muarobaini wa
sekta ya madini kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa
hatimaye kufikia asilimia 10% kama ulivyo mpango wa wizara kuongeza
kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa.
“Nchi
nyingi ambazo zimejua siri hii kwa kiasi kikubwa zimefanikiwa lakini
sisi Tanzania tulichelewa sana, na kama tungeendelea kuchelewa ingefika
kipindi ambacho madini yasingekuwepo kamwe na kama Taifa tungeambulia
mashimo makubwa na kusalia katika wimbi la umasikini” Alisema Mhe Biteko
Aidha,
amemuhikishia mmiliki wa kiwanda hicho kuwa serikali itazungumza na
taasisi zinazofanya kazi za ujenzi nchini kuunga mkono juhudi za umahiri
wa kiwanda hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hususani wakati huu
ambao serikali inaendelea na mchakato wake wa kuhamia Mjini Dodoma.
Sambamba
na hayo pia uongozi wa kiwanda hicho umempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka sera nzuri
hususani kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya madini na juhudi zake
za kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na serikali kwa ujumla wake.
Kampuni
ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd iliyopo mkoani Mbeya ilianzishwa
mradi wa kukata, kusaga na kuuza mawe Januari 2004 baada ya kukidhi
masharti ya usajili wa makampuni.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mawe yaliyo
katwa, Kusagwa na kuongezewa thamani katika kiwanda cha Marmo E. Granite
Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20
Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili katika
kiwanda kinachoshughulika na kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E.
Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya,
Jana 20 Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Katikati)
akisikiliza maelezo kutoka kwa Ndg Salim Jesa Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kuhusu usafirishaji wa mawe
baada ya kuyaongezea thamani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani
Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua utendaji
kazi wa kiwanda cha kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite
Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana
Comments
Post a Comment