URA SACCOS YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI ZA JESHI LA POLISI
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani
akizungumza kabla ya kupokea Vifaa Tiba kwa ajili ya Hospitali za jeshi
la Polisi vilivyotolewa na Chama cha kuweka akiba na Kukopa cha URA
Saccos katika Hospitali ya Kilwa Road Jijini Dar es Salaam
Kamanda wa kikosi cha Afya nchini, Paul Kasabago akizungumza juu ya hali ya Vituo vya Afya vya Jeshi la Polisi nchini.
Kikosi cha Bendi cha Jeshila Polisi nchini kikitoa Burudani kwa watu waliofika katika hafla ya kupokea vifaa tiba kutoka URA Saccos
Naibu Kamishna Azizi Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa cha URA Saccos akizungumz akatika hafala hiyo yamakabidhiano ya vifaa Tiba iliyofanyiak Kilwa Road Jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani, akikata utepe kuashiria uzinduzi na kupokea Vifaa Tiba kutoka URA Saccos
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akifanyiwa kipimo cha Presha na Sukari kutoka kwa Afisa Muuguzi PC Stella Sizya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Polisi Kilwa Road.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akionyeshwa baadhi ya Vifaa tiba vilivyotolewa na URA Saccos
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akisaini karatasi za makabidhiano ya Vifaaa na Naibu Kamishna Azizi Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa cha URA Saccos
Kikundi cha Ngoma cha Jeshi la Polisi nchini kikitoa Burudani
Picha ya Pmoja ya viongozi wa meza kuu na wakuu mwa vikosi mbalimbali
Kamanda wa kikosi cha Afya nchini, Paul Kasabago akizungumza juu ya hali ya Vituo vya Afya vya Jeshi la Polisi nchini.
Kikosi cha Bendi cha Jeshila Polisi nchini kikitoa Burudani kwa watu waliofika katika hafla ya kupokea vifaa tiba kutoka URA Saccos
Naibu Kamishna Azizi Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa cha URA Saccos akizungumz akatika hafala hiyo yamakabidhiano ya vifaa Tiba iliyofanyiak Kilwa Road Jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani, akikata utepe kuashiria uzinduzi na kupokea Vifaa Tiba kutoka URA Saccos
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akifanyiwa kipimo cha Presha na Sukari kutoka kwa Afisa Muuguzi PC Stella Sizya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Polisi Kilwa Road.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akionyeshwa baadhi ya Vifaa tiba vilivyotolewa na URA Saccos
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini, NsatoMarijani akisaini karatasi za makabidhiano ya Vifaaa na Naibu Kamishna Azizi Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa cha URA Saccos
Kikundi cha Ngoma cha Jeshi la Polisi nchini kikitoa Burudani
Picha ya Pmoja ya viongozi wa meza kuu na wakuu mwa vikosi mbalimbali
KUBENEA ATOA MILIONI 14 ZA MFUKO WA JIMBO KUJENGA VIVUKO VIWILI MABIBO
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akikabidhi fedha kwa ajili ya
kulipia kivuko kilichokuwa watu wakilipishwa 200 kwa kila wakipita.
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa Mabibo
wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero
za wananchi, ambapo aliweza kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 14 kwa
ajili ya ujenzi wa madaraja na kuamua kununua kivuko cha mtu Binafsi ili
watu waweze kupita bure kuliko awali ambapo walikuwa wakilipishwa
shilingi 200.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa
Mabibo wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza
kero za wananchi
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa katika mitaa ya Mabibo
wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero
za wananchi
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitembea na wakazi wa Mabibo
wakati alipokwa akifanya ziara ya kutembelea miradi na kusikiliza kero
za wananchi
Mmoja
ya wakazi wa mabibo akiwasilisha hoja yake kwa mbunge wa jimbo la
Ubungo Saed Kubenea wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za
Wananchi
Mmoja
ya wakazi wa mabibo akiwasilisha hoja yake kwa mbunge wa jimbo la
Ubungo Saed Kubenea wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za
Wananchi
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WADAU WA SEKTA YA UWINDAJI WA KITALII NCHINI, YAONGEZEA MIAKA MIWILI YA UMILIKI WA LESENI ZA VITALU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake
mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta
hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa
utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu,
Dk. Aloyce Nzuki (kulia).
Na Hamza Temba, Dodoma
...............................................................
Serikali imesikia kilio cha wadau wa sekta ya uwindaji wa
kitalii nchini na kuamua kuongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu
95 vya uwindaji wa kitalii ambazo zilikuwa ziishe muda wake tarehe 31 Desemba
mwaka huu (2017).
Uamuzi huo umefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla wakati wa kikao cha majumuisho na watendaji wa Wizara hiyo
muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkuano wa wadau wa sekta hiyo ulioandaliwa
na Wizara hiyo mjini Dodoma jana.
Akizungumzia uamuzi huo Dk. Kigwangalla alisema, lengo ni kuwapa
muda wawekezaji hao ili waweze kujiandaa na mabadiliko ya mfumo mpya wa utowaji
wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada ikiwemo kurudisha
baadhi ya gharama za uwekezaji walizoweka katika vitalu hivyo.
Awali akizungumza katika mkutano huo wa wadau Mwenyekiti wa
Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini, Michael Mantheakis
alimuomba Waziri Kigwangalla kuwaongezea muda wa umiliki wa leseni zao kuanzia
miaka mitano au mitatu na nusu ili waweze kurudisha gharama za uwekezaji walizowekeza
katika vitalu hivyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, makambi na vifaa vyake
pamoja na maji.
Hata hivyo, Waziri Kigwangalla aliweka wazi msimamo wa Serikali
wa kutimiza azma yake ya kuingia kwenye utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu
vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada na kusema kuwa kamwe haitorudi nyuma
na kwamba utekelezaji wa zoezi hilo hauwezi kusubiri muda mrefu kiasi hicho.
Akizungumzia kuhusu hatua ya utekelezaji wa utaratibu huo,
Waziri Kigwangalla alisema kwa sasa taratibu za kuandaa Sheria za usimamizi zinaendelea
na zinatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2018 pamoja na kanuni zake
zinazotarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2018.
Aidha, alisema mfumo maalumu wa kielektroniki unaandaliwa ambapo
maombi yote ya leseni za umiliki wa vitalu vya uwindaji kwa njia ya mnada yatafanyika
kwa uwazi kwa njia ya mtandao.
Alisema baada ya kukamilika kwa taratibu zote na mfumo huo mpya
wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada na
maombi kuwasilishwa, mnada wa kwanza utaanza tarehe 1 Julai, 2018 kwa kuanza
kunadi vitalu 61 ambavyo kwa sasa havina wawekezaji.
Mnada wa pili utafanyika mwaka 2020 baada ya kuisha kwa muda huo
wa nyongeza wa miaka miwili ukihusisha vitalu 95 vilivyoongezewa muda wa
umiliki wa leseni pamoja na vitalu vingine endapo vitabaki katika mnada huo wa
kwanza kwa sababu mbalimbali.
Alisema sheria na kanuni zinazoandaliwa hivi sasa zitazingatia mambo
muhimu ikiwemo kuwapa nafasi watanzania wenye mitaji midogo kuweza kuingia
kwenye biashara hiyo pamoja na kuweka adhabu kali dhidi ya wafanyabiashara
watakaohujumu biashara hiyo kwa makusudi.
Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce
Nzuki, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya
wizara hiyo na waandhishi wa habari.
Oktoba 22 mwaka huu (2017) wakati akiongoza kikao cha wadau wa sekta ya
Maliasili na Utalii mjini Dodoma, Waziri Kigwangalla alitangaza
kufuta leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii zilizokuwa zianze mwezi
Januari, 2018 ili kupisha utarartibu mpya wa utoaji wa leseni hizo kwa njia ya
mnada ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuimarisha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake
mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta
hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa
utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto
ni Naibu Katibu Mkuu,
Dk. Aloyce Nzuki.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini,
Michael Mantheakis (kulia) akiwasilisha mapendekezo yake katika mkutano wa wadau
wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali
ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha
utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya
mnada.
Mdau wa sekta ya uwindaji wa kitalii, Dk. Licky Abdallah
akizungumza katika mkutano huo.
Mdau wa sekta ya uwindaji wa kitalii ambaye pia ni mmilikia wa
kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Bushman Hunting Safaris, Talal Abood
akiwasilisha mapendekezo yake katika mkutano huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisikiliza kwa
makini mapendekezo ya wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano
uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa
sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake
mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya
kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya
kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa
kitalii kwa njia ya mnada. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki
(kushoto kwake).
KAMPUNI YA PiMAK YAFUNGUA DUKA KUBWA LA KUUZA VYOMBO VYA MAHOTELINI JIJINI ARUSHA
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo katikati akifungua duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK ambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hiyo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez ( Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi akiingia katika duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAKambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hizo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,kulia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
Kulia ni Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na Mkurugenzi wa hoteli ya Gold Crest ya Mwanza na Arusha Mathias Manga mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK
Meneja Mkuu wa kampuni ya PiMAK ya kimataifa inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mapishai kwenye mahoteli akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea duka hilo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akimuonyesha bidhaa za kampuni ya PiMAK mtaja aliyetembelea duka hilo siku ya uzinduzi Bi.Mary Mbajo
Wahudumu wa duka hilo wakiwa na vepeperushi vya kampuni hiyo
Muonekano ndani ya duka hilo
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo akizungumza mara baada ya kukata utepe,kushoto ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha ,Milance Kinabo
Naibu Meya wa jiji la Arusha,Viola Likindikok akiangalia baadhi ya vyombo vinavyopatikana dukani hapo anayefatia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
Kulia Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akipozi na wadau katikati ni Maya wa jiji Kalist Lazaro
Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akitoa maelezo kwa mteja
Wageni waliofika katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo
Na Pamela Mollel,Arusha
KAMPUNI ya kimataifa ya PiMAK inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli , imefungua duka kubwa jijini Arusha kwaajili ya kuwarahisishia watumiaji wa vyombo hivyo kuvipata kwa wakati
Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo la kisasa Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwepo kwa duka hilo hapa Tanzania tayari ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa mahoteli
Kimambo alisema kuwa kampuni ya PiMAK kuja kuwekeza nchini itasaidia ajira lakini pia kuwainua wajasiriamali wadogo wenye ndoto ya kufika mbali.“Kuna hawa wajasiriamali wadogo ambao wanajihusisha na maswala ya upishi watapata fursa ya kutanua biashara zao kwa kuwa tayari vifaa vinapatikana kiurahisi”alisema Kimambo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez alisema, kampuni hiyo yenye makao yake Uturuki imeamua kufungua maduka hapa Nchini Tanzania kwaajili ya kuwarahisishia wateja wake ambao walikuwa wakiagiza vyombo hivyo nje ya nchi.
Akizungumzia kuhusiana na bidhaa hizo, alisema kuwa ni bidhaa kwa ajili ya matumizi ya hoteli, migahawa na huduma kubwa za mapishi vikiwamo vya kukatia nyama, kuhokea mikate, kuoshea vyombo, kupikia na huduma nyingine za kihoteli4
Comments
Post a Comment