Ubalozi wa Libya wavunja ukimya biashara ya utumwa
Naibu
Balozi wa Libya nchini, Saleh Kosa, akizungumza na waandishi wa habari,
akikanusha nchi yake kufanya biashara ya binadamu na kudai kwamba
kinachofanyika ni utozaji wa fedha za ajili ya kuwasafirisha binadamu
waliokimbia katika nchi zao ili wavuke kwenda nchi za Ulaya na Marekani.
Mazunghumzo hayo yalifanyika Ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana
Akisisitiza ajambo kwa waandishi wa habari
Na MWANDISHI
WETU
SERIKALI ya
Libya imekanusha taarifa iliyosambaa katika mitandao na vyombo mbalimbali vya
habari kuwa mamia ya watu wanauzwa kama mnada katika soko la utumwa nchini humo
kwa kiasi kidogo cha chini ya dola 400.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kaimu Balozi wa Libya, Saleh Kosa alisema mapatano yale
yalikuwa ni gharama za kuwasafirisha na wala si gharama za kuuza uhuru wao ili
wawe watumwa.
“Serikali ya
Libya, mara tu baada ya kupata taarifa hizo ilivituma vyombo husika kufanya
uchunguzi jumuishi na wa kina kuhusu madai hayo ambayo ni makosa kwa mujibu wa
sheria za Libya na baadaye isambaze kwa watu wote na pia kuwachukulia hatua za
kisheria wote wanaohusika bila ya kujali kama makosa yenyewe yamefanywa kwa
lengo la kuvukisha wahamiaji au utumwa,”alisema Kosa.
Alisema
Libya inaamini kwamba mambo kama hayo, huwa ni sehemu yanayofungamana na
uhamiaji haramu ambao Libya ndiyo nchi iliyodhurika zaidi na kwamba imekataa
kuwajibika peke yake kubeba jukumu la kukomesha uhamiaji haramu.
“Libya
inapenda kuhakikisha kwamba katika kukomesha suala la uhamiaji haramu na mambo
yanayohusiana nayo inalazimu kuwapo kwa juhudi za pamoja za kimataifa na
zilizoratibiwa ili kupambana na hali hiyo.
“Kwa kigezo
hiki, Libya inaomba kuwepo na mikakati kivitendo na yenye athari kubwa baina ya
nchi wanazotoka wahamiaji haramu, nchi wapitiazo na waendazo na pia
kushirikisha taasisi husika za kimataifa na za kikanda,”alisema kaimu balozi
huyo.
Kosa alisema
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya inaweka upya msisitizo wake kuiunga mkono
serikali ya nchi hiyo, kwa kuipa uwezo wa kiufundi na kilojistiki ili kuisaidia
katika kudhibiti mipaka yake.
“Kuuhimiza
Umoja wa nchi za Ulaya na jumuiya ya kimataifa kushirikiana na nchi watokazo
wahamiaji ili kufanya miradi ya maendeleo ya kudumu kwa lengo la kukomesha
suala hili na athari zake hatari.
“Pia
kutekeleza vifungu vya tamko la pamoja kuhusu uhamiaji na maendeleo
lililokubaliwa katika vikao vya Novemba 22 na 23 mwaka 2006 mjini Tripoli,
Libya.
“Kuisaidia
Libya kumudu gharama za kujenga na kuendesa vituo vya kuwaweka wahamiaji na
kutoa misaada kusaidia maeneo yote yaliyodhurika na uhamiaji nchini Libya na
pia kuvisaidia vyombo vya usalama vya Libya kuwa na uwezo unaohitajika,”alisema.
Aidha
alisema kwa mara nyingine serikali ya Libya inalaani biashara ovu ya uuzaji na
usafirishaji binadamu ikiwa ni ya kimataifa au ya kikanda.
Alisema
endapo kuna lililotokea kuhusu hilo la wahamiaji basi itakuwa jambo
alilolitenda mtu binafsi na wala si suala la kuratibiwa.
“Sisi
tunalikana na kulilaani vikali kwa imani kwamba kushughulikia suala la
wahamiaji ni lazima kuwe ni kwa kuzingatia heshima yao kama wanadamu.
“Serikali ya
Umoja wa Kitaifa inawahakikishia kuwapo kwa mahusiano ya kindugu baina ya
walibya na ndugu zao waafrika ambao kwa karne nenda rudi wamekuwa
wakiunganishwa na mashikamano ya urafiki na kuwa malengo yanayofanana,”alisema.
Akisisitiza ajambo kwa waandishi wa habari
Comments
Post a Comment