Ubalozi wa Libya wavunja ukimya biashara ya utumwa
Naibu Balozi wa Libya nchini, Saleh Kosa, akizungumza na waandishi wa habari, akikanusha nchi yake kufanya biashara ya binadamu na kudai kwamba kinachofanyika ni utozaji wa fedha za ajili ya kuwasafirisha binadamu waliokimbia katika nchi zao ili wavuke kwenda nchi za Ulaya na Marekani. Mazunghumzo hayo yalifanyika Ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Na MWANDISHI WETU SERIKALI ya Libya imekanusha taarifa iliyosambaa katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari kuwa mamia ya watu wanauzwa kama mnada katika soko la utumwa nchini humo kwa kiasi kidogo cha chini ya dola 400. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Balozi wa Libya, Saleh Kosa alisema mapatano yale yalikuwa ni gharama za kuwasafirisha na wala si gharama za kuuza uhuru wao ili wawe watumwa. “Serikali ya Libya, mara tu baada ya kupata taarifa hizo ilivituma vyombo husika kufanya uchunguzi jumuishi na wa kina kuhusu madai hayo ambayo ni makosa kwa mujibu wa sheria za Libya na baadaye isambaze kwa