UHAMIAJI WAFANYA USAFI NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO HOSPITALI YA TEMEKE
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makalala ametoa zawadi kwa
akina mama na watoto waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Temeke
sambamba na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka eneo hilo.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jhn Pombe Magufuli la kufanya usafi kila mwisho wa
mwezi.
Kamishna
Jenerali Anna alimkabidhi kijarida chenye masuala mbalimbali yanayohusu
uhamiaji kwa mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na kumtaka kushirikiana
nao kwenye kutoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo pale pindi wapatapo
muda.
Mganga
Mkuu wa hospitali ya Temeke Dr Amani Malima amewashukuru sana kwa kuja
kufanya usafi kwenye hospitali hiyo na kutoa zawadi kwa wakina mama na
watoto huku akiwahakikishia kuwa watatoa elimu kwa wagonjwa wanaofika
hapo kuhusiana na masuala ya uhamiaji.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akifanya usafi
katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi
kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa
Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya emeke Felix Lyaviva wakifanya usafi katika Hosptali ya
Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa
mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar
es Salaam Oktoba 28, 2017.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akijadiliana
jambo na mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva baada ya kuwasili katika
Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi
kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe
Mafuguli.
Kamishna
Jeenerali akitoa zawadi ya pampers na sabuni kwa wakina mama
waliojifungua watoto walio chini ya muda wake (njiti) walipowatembelea
kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa
mwezi.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akitoa zawadi
kwa wakina mama walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda
kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kumaliza kufanya usafi katika hospitali ya
Temeke sambamba na kutoa zawadi kwa watoto na wakina mama waliokuwa
wamelazwa kwenye hospitali hiyo, hilo ni katika kutilia mkazo agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya
usafi kila mwisho wa mwezi. Kushoto ni Mganga mKuu wa Hospitali ya
Temeke Dr Amani Malima.
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala akimkabishi
jarida la Uhamiaji navifaa vya usafi kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Temeke Dr Amani Malima ikiwa ni siku ya usafi wa kila mwisho katika
kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Mafuguli, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa
Uhamiaji
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala akisaini katika kitabu cha wageni.
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala akijadiliana
jambo na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dr Amani Malima pamoja na
kufurahi pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi,
Wafanyakazi wa uhamiaji wakiwa wanafanya usafi.
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala na Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Temeke Dr Amani Malima wakiwa wanaelekea katika wodi za
kina mama na watoto baada ya kumalizika kwa usafi.
Kamishna wa Uhamiaji- Pasi na Uraia, Gerald Kihinga akitoa zawadi kwa
watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi
wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Samwel Magweiga kitoa
zawadi kwa watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda
kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna
wa Sheria Hanerole Manyanga akitoa pole na zawadi kwa mama aliyetoka
kujifugua walipotembelea Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi
wa kila mwisho wa mwezi.Picha zote na Zainab Nyamka.
NELLY KAZIKAZI ATWAA TAJI LA MISS HIGHER LEARNING 2017
Miss
Higher Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha akiwa
na washindi wenzake baada ya kutangazwa rasmi na kuvishwa Taji katika
shindano la Miss Vyuo Vikuu lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye
Ukumbi wa King Solomon Namanga Dar es Salaam. Kulia ni mshindi wa pili,
Queen Elizabeth Makune (kushoto) ni mshindi wa tatu, Melody Thomas.
Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Shindano hilo pia lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii tofauti kama JK Comedian Jukwaani, Msaga sumu na Barnaba Boy.
Sehemu ya wageni waliofika kushuhudia shindano hilo wakiwa katika meza za VIP
Shoo ilianza kama hivi kwa kufungua na shoo ya pamoja
Hatimaye warembo walianza kupita jukwaani na vazi la ubunifu....
Msaga Sumu akitoa burdani
Hatimaye Warembo walianza kupita jukwaani wakia na vazi la Ufukweni
Majaji wakijadiliana jambo
Dj John Dilinga naye akionyesha shoo, kuigiza umiss
Miss Talent akinyesha jinsi alivyochukua taji hilo.
Hatimaye ukafika muda wa Warembo kupita jukwaani na vazi la usiku.
Ulifika muda wa Barnaba Boy kuwarusha wadau wa urembo ukumbini hapo
Dj Denso kutoka Mafoto City Sound akiwarusha kwa ngoma za Barnaba alipopanda jukwaani
Huku ni nyumba ya Stage warembo wakishoo love
Barnaba Boy akiwachezesha warembo kwa ngoma zake
Warembo wakiwa nyuma ya stage nao wakifuatilia shoo ya Barnaba Boy
Hawa ndiyo warembo wote walioshiriki shindano hilo
Mkurugenzi na mratibu wa shindano hilo, Joseph Musendo akizungumza jukwaani, akiwa na msaidizi wake
Ilipoanza kutangazwa tatu bora
Miss Highlearning 2016, Laura Kway, akimvisha Taji Miss Highlearning 2017, Nelly Kazikazi, baada ya kutangazwa mshindi.
Miss Higher Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi.
Comments
Post a Comment