Kituo cha Mabasi Ubungo kuzalisha ajira 20,000
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka
Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali yamaendeleo
jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa kituo cha Mabasi Ubungo.
Ugeni
huo uliambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang ambayo
ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo
hicho.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya
kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo
umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kituo cha mabasi
ubungo.
Alifafanua
kuwa jiji la Dar es Salaam linakaribia kunza kwa ujenzi wa mradi mkubwa
wa kubadilisha kituo cha mabasi ubungo na kwamba hatua mbalimbli
zimeshakamilika ili kupisha mradai huo.Alisema kuwa mara baada ya
kukamilika kwa mradi huo jumla ya watanzania 20,000 watapata ajira jambo
ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwezesha
vijana kuondokana kwenye makundi ambayo sio salama.
Alisema
kufanikisha kwa mradi huo, utasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha
jijini hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.“ Leo
nimekutana na ugeni ambapo kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa
wamekuwa na urafiki mkubwa katika nchini yetu, tumejadiliana mambo mengi
ambayo yote ni yakuleta maendeleo katika jiji letu.
“
Lakini kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi Ubungo, ambapo
hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia
watajulisha, nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa jiji linafuata
utaratibu katika kutekeleza mradi huo” alisema Meya Mwita.
“
Fursa hii ni kubwa ambayo tumeipata, watanzania watapata ajira,
mzunguko wa fedha kwenye jiji letu utaongezeka, kama Meya wa jiji hili
nimewakaribisha tufanye kazi pamoja, lengo likiwa nikuweka jiji kwenye
muonekano mzuri” aliongeza.Kwaupande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Linghang Cathy Wang alimpongeza Meya Mwita kutokana na aina ya utendaji
wake wa kazi nakuahidi kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi
huo.
Alisema
kuwa Meya Mwita ni kiongozi anayefanya kazi kwa bidii na umakini na
kwamba kutokana na jitihada hizo za kulijenga jiji , kampuni yao
itafanya kazi na kumuhakikisha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA MAKUMBUSHO MAPYA YA OLDUVAI NA ONESHO LA CHIMBUKO LA MWANADAMU
Morogoro, Septemba 28, 2017.
Serikali
ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana
na Umoja wa Ulaya imekamilisha ujenzi wa Makumbusho mapya ya Olduvai
ambayo yanaonesha Chimbuko la Binadamu (The Cradle of Humankind) katika Bara la Afrika.
Makumbusho
hayo mapya pamoja na Onesho la Chimbuko la Binadamu, yatafunguliwa
rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan tarehe 03 Oktoba, 2017 katika eneo la Olduvai, ndani
ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Onesho
hilo ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu uliofanyika katika Bonde la
Olduvai na Laetoli katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Wananchi,
viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mabalozi wanatarajiwa kuhudhuria
kwenye hafla hiyo.
Idadi
kubwa ya vioneshwa katika Makumbusho hiyo, vilipatikana katika bonde la
Olduvai na Laetoli nchini Tanzania kupitia utafiti wa kisayansi wa muda
mrefu na vilikuwa vimehifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar
es Salaam. Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana za mawe
na masalia ya wanyama walioishi takribani miaka milioni 4 iliyopita.
Makumbusho hayo yamepangwa
kuonesha sehemu kuu nne zinazowiana. Sehemu ya kwanza inahusu ushahidi
wa nyayo za zamadamu zilizongunduliwa huko Laetoli mwaka 1978 na
mtafiti Dr. Mary D. Leakey. Nyayo hizi ziliachwa na zamadamu anayeiitwa
Australopithecus afarensis na ndio ushaidi usiopingika wa zamadamu
kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopita.
Sehemu
ya pili inahusu hadithi ya kusisimua ya kuwa binadamu (Genus Homo);
ambapo kutakuwa na masalia ya zamadamu wanaoitwa Zinjanthropus au
Paranthropus boisei na Homo habilis, zana za mawe za mwanzo zilizotumika
(Oldowan) katika kujipatia chakula na ushahidi wa kale wa ulaji wa
nyama katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million
2 iliyopita.
Sehemu
ya tatu inahusu maisha ya jamii ya Homo erectus. Jamii hii ilikuwa
inafanana zaidi na binadamu wa sasa kuliko jamii zilizotangulia.
Kutakuwa na masalia zamadamu Homo erectus, zana za mawe (Acheulian) na
ushahidi wa ulaji wa wanyama wakubwa kama vile Nyati na tembo katika
historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 1.7
iliyopita.
Sehemu
ya nne inaonesha kipindi cha mwanzo cha binadamu wa sasa (Homo sapiens)
walioanza kutokea hapa Afrika miaka laki 2 iliyopita. Sehemu hii pia
itaonesha mila na utamaduni wa makabila mbalimbali kama vile Wahadzabe,
wamasai na Datoga. Kutakuwa na mavazi ya asili ya jamii hizo, zana za
kuwinda na vifaa mbalimbali wanavyovitumia katika maisha yao ya kila
siku.
Wizara
ya Maliasili na Utalii inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria ufunguzi
huo ambapo watapata pia fursa ya kutembelea vivutio vingine vilivyopo
ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kujifunza na kufurahia urithi huu wa
asili na kiutamaduni wa Taifa letu.
Imetolewa na;
Prof. Jumanne Maghembe
Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe
Waziri wa Maliasili na Utalii
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari
jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na
Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba,
2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai
wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari
jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na
Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba,
2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai
wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha na Hamza Temba - WMU).
KIITEC LAUNCHED SOLAR POWER PLANT AND SOLAR LABORATORY
Excellency
Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania (C) cuts a ribbon to
officiate the launch of Solar Power plant and laboratory at KIITEC in
Arusha, others in photo are senior officials from the partners
institutions supporting the Institute.
FTE President Fransis Bronchon,(R) briefing invited guests on Solar Project at KITEEK during the launch event at Arusha.
Excellency
Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania(C) got briefing on
project from, Albert Mtana, (R)-Teacher of Electrical and Solar
Photovoltaic System (L) is Michel Ramser-VP Strategic Marketing and
Sponsorship (ADEI).
Solar
panel installed at the centre. The Kilimanjaro International Institute
for Telecommunications, Electronics and Computers (KIITEC) has launched
30KW solar power plant and solar laboratory at its training centre in
Arusha recently. The Guest of Honour at launch event was Her Excellency
Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania, also the event brought
together the partners that have supported KIITEC for many years.
These
are: Schneider Electric East Africa, the Schneider Electric Foundation,
ADEI, EDF Help and the Foundation for Technical Education (FTE).
Speaking during the event, KIITEC Director of studies, Mr. Daniel Mtana,
said the opening of this solar power plant speaks to the accomplishment
of institute’s vision to become the centre of training excellence for
renewable energy, particularly solar photovoltaic systems in East
Africa.
“Committed
to true hands-on experience, KIITEC has now invested heavily in
photovoltaic solutions and strives to be recognized as the premier
provider of quality technical education in a student-centered
community.” General manager at Schneider Electric East Africa, Mr. Mr.
Edouard Heripret, said in most sub-Saharan countries, the rate of
enrolment in formal secondary technical and vocational training and
education (TVET) does not exceed 5%.
“Vocational
training has always been at the heart of Schneider Electric’s DNA. In
East Africa, we have been committed to support technical training since
2009. Kiitec was one of our first training partners and I am pleased
today to participate in the inauguration of the solar plant and
laboratory, as these new components will allow students to have a full
set of competencies to enter the labour market and will support access
to energy for everyone.” Mr.
Heripret
added “At Schneider Electric, we are building sustainable communities
through energy knowledge and leadership, thanks to the Schneider
Electric Foundation. Its aim is to contribute to the development of
people and societies through education, innovation, awareness-raising
and vocational training related to energy.
It
acts, anywhere in the world where the company is present, through its
three programmes. KIITEC is an international technical institution, was
founded in 2004 by French engineers and has produced some of the most
competent technicians in the country. Two NGOs, the Foundation for
Technical Education (FTE-Swiss) and Action Development Education
International (ADEI-French), support the institution. Schneider Electric
assists ADEI in its support of KIITEC.
The
institute is a pilot centre, with the goal of transposing and exporting
its model from Tanzania, to Kenya. It provides its students with the
basic skills in telecommunications, electronics, information science,
networks and industrial automation systems.
The
training lasts over two years. It comprises lectures complemented by
practical training, project design, and a three-month outplacement in a
company. As of today, 350 young people, comprising 90% of the students,
have obtained their diploma, the ‘National Technical Award’, which is
recognized by the local government, and have all found jobs, mainly in
the industrial maintenance sector.
Serikali Kuzichukulia Hatua Taasisi Zilizokiuka Taratibu za Manunuzi 2016/2017
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma
(PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga (kushoto) akiongea wakati
wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya
Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma, Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo Prof. Sufian Bukurura.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
Balozi Dkt. Matern Lumbanga wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini
ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma
(PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea
Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na
wajumbe wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) baada ya kupokea
Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma ambapo ameahidi kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka
taratibu za manunuzi zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt. Laurent
Shirima akiongea, wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali
imesema itazichukulia hatua Taasisi zote zilizokiuka sheria na kanuni
za manunuzi ya Umma pamoja na zile zenye viashiria vya rushwa ambazo
zimebainika katika ripoti ya tathmini ya utendaji iliyotolewa na Mamlaka
ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
Hayo
yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango alipokuwa akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za
Serikali katika sekta ya Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha
2016/17.
“Tutazichukulia
hatua na kuziwajibisha taasisi zote ambazo zimebainika katika ripoti
hii kuwa na viashiria vya rushwa au kufanya malipo yenye utata katika
manunuzi yao,” alisema Dkt. Mpango.
Dkt.
Mpango amesema kuwa, zaidi ya 70% ya fedha za Umma zinatumika kununua
vifaa na huduma mbalimbali hivyo Serikali haitavumilia kuona fedha hizo
zinatumika bila kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga
amezitaja taasisi ambazo zimekiuka sheria na taratibu za manunuzi kwa
mwaka 2016/2017 kuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya
Mifupa (MOI) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taasisi
nyingine ni Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Anga (TCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na
Halmashauri ya Wilaya Kondoa.
Balozi
Lumbanga amesema kuwa uchunguzi wa zabuni mbili zenye thamani ya
shilingi bilioni 160.5 ambazo zilikuwa zinatekelezwa na Wizara ya Fedha
na Mipango pamoja TCAA haukubainika mapungufu ya msingi na PPRA
ilipendekeza utekelezaji wa miradi hiyo uendelee kama ilivyopangwa.
“Uchunguzi
uliofanywa katika taasisi sita zilizobaki ulibaini kuwa Serikali
ilipata hasara ya takribani shilingi milioni 12.15 kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi
uliosababisha ongezeko la riba pamoja na faini zilizotokana na ukiukwaji
wa taratibu za kijamii na mazingira kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa
kazi za ujenzi,” alisema Balozi Lumbanga.
Balozi
Lumbanga amezitaja Taasisi zilizobainika na malipo yenye utata kuwa ni
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) na Halmashauri ya Kwimba. Ukaguzi wa kupima upatikanaji wa
thamani ya fedha ulibaini malipo yenye utata katika taasisi hizo tatu
ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 483.44 zililipwa kwa wakandarasi
kwa kazi ambazo hazikuwa zimefanyika.
Vile
vile amesema kuwa, miradi 33 katika taasisi 17 ilibainika kuwa na
kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa. Taasisi hizo ni Mamlaka za
Maji Safi na Maji Taka za Moshi (Muwasa), Mwanza (Mwauwasa) na Arusha
(Auwasa) pamoja na Halmashauri ya Wilaya za Wilaya za Msalala, Kibondo
na Moshi.
Taasisi
byingine ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Wizara
ya Maji na Umwagiliaji, Chuo cha Ufundi Arusha, Halmashauri ya Mjia wa
Kahama, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Uhasibu Arusha
(IAA), Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Mji wa MAsasi
pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Ripoti hiyo ni ripoti ya 11 kuwasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango tangu PPRA ilipoanzishwa.
MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR
Muakilishi
wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa wapili kushoto akifuatana na
Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Maandamano ya maadhimisho
ya Siku ya Moyo Duniani yaliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu
wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
Maandamano
yalioongozwa na Bend ya Chipukizi yakielekea katika Ofisi ya Jumuia ya
watu wenye maradhi yasioambukiza katika maadhimisho ya Siku ya moyo
Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
Vikundi
mbalimbali vya mazoezi vikishajiisha suala zima la ufanyaji mazoezi ili
kulinda afya na maradhi mbalimbali, katika siku ya maadhimisho ya Siku
ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Makamo
mwenyekiti wa ZNCDA Ali Zubeir Juma akitoa hotuba ya makaribisho kwa
mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani
29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Mgeni
rasmi katika maadimisho ya siku ya Moyo Duniani Mwakilishi wa Jimbo la
Mpendae Said Mohd Dimwa akitoa hotuba kuhusiana na kujikinga na maradhi
mbalimbali yanayotokana na Ulaji,Unywaji wa Pombe na Uvutaji wa Tumbaku
katika maadhimisho hayo yliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu
wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Wananchi
mbalimbali waliojitokeza kupimwa afya zao katika maadhimisho ya Siku ya
moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF
SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar
Kampuni
yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya
Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu
katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama
Manispaa ya Kinondoni.
Mafunzo
hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa
mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za
msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na
kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application
mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia
kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara
kwa kutumia technologia za kisasa.
Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo
awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini
tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze
kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa
mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule
zingine.
Waalimu
wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo.
Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila
Mtanzania, aliongeza Matinde.
Hata
hivyo, Matinde alisema kuwa mafunzo kwa wanafunzo ambao walikuwa
washaanza yataendelea vile vile. ‘Utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wale
wanafunzi ambao walikuwa washaanza utaendelea vile vile. Kilichofanyika
ni chukua hatua ya ziada ya kuwapa walimu mafunzo ya Tehama ili nao
waweze kuwa kwenye nafasi ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa’ alisema
Matinde.
Matinde
aliongeza kuwa bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa
vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara
kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii hususani
vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama
kwa ujumla.
Kwa
upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “
Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama.
Tuhahakisha kuwa walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao
waanze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi.
Jengela
alisema mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji
kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”
msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali.
Bado tunapokea maombi, Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia www.teknohama.or.tz na www.a irtelfursa.com au kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama
MBUNGE AZZA HILAL AWAPIGA JEKI WANAFUNZI WENYE ULEMAVU SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA SHINYANGA
Mbunge
wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi
baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika
shule ya msingi Tinde-Picha na Said Nassor-Malunde1 blog Tinde
Mbunge
wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM)
ametembelea shule ya msingi aliyosoma Tinde iliyopo katika kata ya Tinde
wilaya ya Shinyanga kisha kutoa msaada kwa wanafunzi nane wenye ulemavu
wa viungo akiwemo kijana ambaye hawezi kuongea wala kutembea. Mbunge huyo ametembelea shule hiyo jana Jumatano Septemba 27,2017.
Mheshimiwa
Hilal ametoa msaada wa baiskeli kwa kijana ambaye hawezi kutembea wala
kuongea anayesoma katika shule hiyo huku akijitolea kuwanunulia
wanafunzi hao nane mahitaji yao yote ya shule mpaka watakapomaliza
masomo yao ya shule ya msingi.
“Hii
shule nimesoma,baada ya kufika hapa nimeambiwa kuna watoto wenye
ulemavu,baada kumuona kijana huyu nimempatia baiskeli lakini pia
nimejitolea kuwahudumia wanafunzi hawa wanane ambao wana ulemavu wa
viungo,nitawanunulia mahitaji yao ya shule na watakuwa wanakunywa uji
kila siku kwa gharama zangu”,ameeleza Mbunge huyo.
Mbali
na kutoa msaada huo Mheshimiwa Azza Hilal ameshiriki zoezi la Upandaji
miti katika wilaya ya Shinyanga lililoanzishwa na Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro lenye kauli mbiu ya "Shinyanga Mpya, Mti
Kwanza".
Akiwa
katika kata ya Tinde,mbunge huyo aliungana na mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro kupanda miti katika shule ya msingi Tinde,pia
katika barabara kuu ya kutoka Tinde kwenda Kahama na barabara ya kutoka
Tinde kwenda Nzega mkoani Tabora.
Mbunge
wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi
baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi
Tinde,aliyeshikilia kipaza sauti ni mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akiwa na mwanafunzi
aliyepata msaada wa baiskeli kutoka kwa Mheshimiwa Azza Hilal
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akipanda mti katika shule ya msingi Tinde.
PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NCHI 21 DUNIANI KWA AJILI YA KUJADILI UKUKUZAJI WA SEKTA YA UPANDAJI WA MITI KIBIASHARA
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha
upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani
Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21
duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji
na upatikanaji wa masoko. Aliwataka wajumbe hao kujadili namna ya
kuwawezesha wakulima wa miti wakati wanasubiri kuvuna mazao yao waweze
kujishuulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi kwa kutumia mbinu bora
za kisayansi ili waweze kujikimu kimapato.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha
upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani
Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21
duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji
na upatikanaji wa masoko.
Baadhi
ya wajumbe kutoka nchi 21 duniani wakifuatilia mkutano huo. Nchi hizo
ni Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Gambia,Ghana, Italy, Mali, Niger,
Nigeria, Senegal, Sudan, Liberia, Cameroon, Swaziland, Finland, Zambia,
Canada,Mozambique, Zimbabwe, Kenya na Tanzania.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe akizungumza katika mkutano huo.
Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kuishauri dunia namna bora
ya kutunza na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho
ikiwemo utekelezaji wa sheria za usimamizi wa misitu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.
Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka
wajumbe kujadili kwa uwazi kuhusu mikakati mbalimbali ya kukabiliana na
changamoto za sekta ya misitu na kwamba Serikali kupitia Wizara itapokea
maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuimarisha
ustawi wa sekta hiyo.
Waziri
Maghembe akieleza jambo kwenye ka mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe
wajumbe wajadili namna bora ya kuwafundisha wakulima wa miti kufanya
kilimo bora ikiwa ni pamoja na mafunzo uvunaji wa hewa ukaa ili kuwainua
kimapato. Aliwataka pia kusaidia wakulima wa miti katika upatikanaji wa
masoko ya uhakika.
Prof. Maghembe akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana
na baadhi ya viongozi waliondaa mkutano wa pili wa Mashirika
yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya
misitu barani Afrika muda mfupi kabla ya kufungua mkutano huo wa siku
mbili uliowashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la
kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa
masoko.
Baadhi ya wajumbe walishiriki mkutano huo kutoka nchi 21 duniani.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Mbunge
kutoka Kenya, Chariti Katambi mkoani Morogoro jana baada ya kufungua
mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara
na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku
mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la
kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa
masoko.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari
mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika
yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya
misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe
kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya
kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko.
Picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)
"Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira"- Rutayuga
Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na
kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa
kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.
Kaimu
katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph
Rutayuga amesema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa
warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini
yaliyoandaliwa na UNESCO.
Akizungumza
kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt,
Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu
gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa
viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya
ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora
usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri.
“Tunalenga
kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu
iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na
kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda
na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.
Ameongeza,kama
suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana
potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale
walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye
uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni
kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua
umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo
ya kukuza uchumi,” amesema.
Naye,
Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo
itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo
ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo
matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu
bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la
kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa
mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema
Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii .Kaimu
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa
warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya
ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar
es Salaam leo. Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf
Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi
na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya
kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi
ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa
kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika
jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
Comments
Post a Comment