RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BILL GATES NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana
na Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill
Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es
salaam leo Agosti 10, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akizungumza
na Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. ill
Gates aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na
Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill
Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es
salaam leo Agosti 10, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia), Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dk Charles Tizeba (wa tatu Kushoto),
Msaidizi wa rais Masuala ya diplomasia Bi. Zuhura Bundala (kushoto)
pamoja na maafisa alioongozana nao Bw. Bill Gates
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana
na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea
na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10,
2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa katika
mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Immi Patterson
aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli
akimsindikiza Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Immi Patterson
aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo
Agosti 10, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na
kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10,
2017.PICHA NA IKULU
HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA YASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA KAMATI YA LAAC
Na Jumbe Ismailly IRAMBA
HALMASHAURI
ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida imeshindwa kutekeleza agizo la
kamati ya kudumu ya Bunge la kutenga asilimia kumi kutoka kwenye mapato
yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya wanawake pamoja na vijana katika
kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha wa 2012/2013 hadi 2014/2015.
Kaimu
Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,CARROLINE DALULI
aliyasema hayo kwenye taarifa aliyotoa kwenye mkutano wa Baraza maalumu
la madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo lilipokutana kujadili hoja za
Ukaguzi na Mpangokazi wa utekelezaji wa maoni yaliyotolewa na Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2015/2016.
“Kamati
iliagiza Halmashauri kuchangia asilimia kumi kutoka kwenye mapato ya
ndani kwa ajili ya wanawake na vijana kwa miaka hiyo iliyotajwa na kiasi
kilichoonekana”alifafanua kaimu Mweka Hazina huyo.
Kwa
mujibu wa Kaimu Mweka hazina huyo kwa mwaka 2012/2013,2013/2014 na
2014/2015 Halmashauri ya wilaya ya Iramba haijatekeleza agizo la kamati
ya kudumu ya Bunge kwani hakuna fedha yeyote ile iliyotengwa na
iliyopelekwa kwenye vikundi hivyo.
Aidha
Daluli aliweka bayana pia kwamba kwa mwaka 2016/2017 Halmashauri hiyo
imechangia shilingi milioni mbili,zikiwemo shilingi milioni moja kwa
Mazega Kisimba na shilingi zingine milioni moja kwa kikundi cha
Maendeleo Shelui na itaendelea kuchangia kadri fedha zitakapopatikana.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Huduma za jamii wa
Halmashauri hiyo,Hamisi Kinota akichangia hoja hiyo ya michango ya
vikundi vya wanawake na vijana alisisitiza kwamba kutokana na uchangiaji
wa Halmashauri hiyo unadhihirisha wazi kwamba Halmashauri haitaweze
kuchangia michango hiyo kwa asilimia mia moja.
Hata
hivyo Kinota huku akionyesha hofu ya utekelezaji wa agizo hilo la kamati
ya kudumu ya Bunge alibainisha kuwa katika kipindi cha mwaka
2012/2013,2013/2014 na 2014/2015 kati ya shilingi milioni 109,819,388
zilizotarajiwa kutumika,ni shilingi milioni mbili tu ndizo zilizotolewa
na hivyo kubakiza zaidi ya shilingi milioni 107,hali ambayo inaonyesha
hakuna uwezekano kwa Halmashauri hiyo kumaliza deni hilo kwa asilimia
mia moja.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi alishauri kwamba njia pekee ya
kumaliza deni hilo la michango ya vikundi vya wanawake na vijana ni
kuandika maandiko mbali mbali na kusambaza kwa wafadhili na kudai kwamba
kuna watu wenye fedha walio tayari kuwasaidia wanawake na vijana.
“Mtakapopata
hizo fedha najua mnaweza kupata hata zaidi ya shilingi milioni mia
mbili,mtakapopata hizo fedha mtaaandika kwamba ni fedha ambazo ninyi
wenyewe Halmashauri mmezitafuta kwa hiyo itakuwa ni sehemu ya mapato
yenu na mtazipeleka kwa wanawake na vijana”alisisitiza Dk.Nchimbi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi akimkabidhi mmoja wa madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Iramba cheti cha mafunzo ya udiwani aliyopata
na ambayo yatawawezesha madiwani wote kutambua majukumu pamoja na mipaka
yao ya kazi.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi akisisitiza juu ya maafisa
watendaji wa vijiji 30 walioiba fedha za chakula cha njaa kuhakikisha
wanazirejesha ifikapo aug,30,mwaka huu na kupendekeza njia rahisi ya
fedha hizo kurejeshwa kuwa ni kuanzishwa kwa Mahakama tembezi
itakayomtembelea kila mdaiwa na kuuza mali alizonazo ili kulipia deni la
chakula hicho cha njaa walizokula.
SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa Kanuni za taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha taslimu kutoka na kwenda nje ya nchi (Crossborder Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments Regulations) ambapo wasafirishaji wa fedha taslimu na wasafiri wote wanaotoka au kuingia nchini, watatakiwa kutoa taarifa za fedha taslimu wanazosafirisha ikiwa fedha hizo zinalingana au zinazidi kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi (USD 10,000).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni hizo, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema utekelezaji wa kanuni hizi, pamoja na mambo mengine utaiwezesha nchi kuwa na takwimu za usafirishaji fedha taslimu.
“Takwimu hizo zitakazosaidia pamoja na mambo mengine kubaini vitendo vya kihalifu, kupunguza utoroshaji wa mitaji na kuhakikisha kuwa tunapunguza kama siyo kumaliza kabisa usafirishaji wa fedha zitokanazo na uhalifu au/na fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi” alisema Bw. Makombe
Aidha kanuni hizo zimeweka adhabu zitakazochukuliwa dhidi ya wale watakabainika kutaka kupita na fedha zinazolingana au zinazozidi kiwango kilichowekwa bila kutoa taarifa au watakaotoa taarifa za uongo. Alizitaja adhabu hizo kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa fedha taslimu walizonazo na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kama vile kufunguliwa mashtaka.
“Wahalifu pamoja na mambo mengine, wanapenda kusafiri na fedha taslimu kwani wanaogopa kutumia benki kutuma fedha kutokana na umakini unaoongezeka katika benki na udhaifu unaoweza kuwepo mipakani” Alisisitiza Bw. Makombe.Kamishna huyo amewaasa washiriki wa warsha hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kuziba mianya yote ambayo wahalifu wanaweza kuitumia kutimiza kusudi lao ovu na kuhatarisha usalama wa nchi.
Kutokana na umuhimu wa ushiriki wa wadau mbalimbali katika utekelezaji wa kanuni hizo warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka taasisi mbalimbali wengi wao wakiwa ni maafisa forodha.
Washiriki hao wametoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kikanda, Mamlaka ya Mapato Tanzania na vikosi vya ulinzi na usalama
Wengine ni Bodi ya Mapato Zanzibar, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo-Zanzibar, Shirika la Posta, Benki kuu ya Tanzania, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka-Zanzibar, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka-Tanzania Bara Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bara na Zanzibar, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Idara ya uhamiaji na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu.
JK NA LOWASSA WAJUMUIKA NA MAMIA YA WANANCHI MAZISHI YA BILIONEA MREMA ARUSHA
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea marehemu Maleu Mrema
katika ibada ya mazishi yaliyofanyika jana katika hoteli yake ya Ngurudoto
iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha(Habari Picha NA Pamela Mollel,Arusha)
Waziri
Mkuu mstaafu,Edward Lowassa akiweka shada la maua pamoja na mke wake
katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema jana nje kidogo ya jiji la Arusha
katika hoteli ya Ngurudoto
Mkuu
wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiweka shada la maua katika kaburi la
marehemu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika katika hoteli yake
ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha
Baadhi ya wake za marehemu wakiweka udongo katika kaburi la mpendwa wao
Waziri Mstaafu wa mambo ya nje Benard Membe akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema
Meneja mahusiano Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)Pascal Shelutete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema.
Watoto wa marehemu wakiwa wamebeba mashada ya maua
Rais
mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete wakisalimiana na Waziri Mkuu
mstaafu,Edward Lowassa katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema leo nje
kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
Baadhi
ya wanakamati wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mrema
kuelekea katika eneo maalumu lililotengwa na familia kwaajili ya maziko
Hapa watoto wakiwa wanaweka udongo katika kaburi la baba yao
Wake wa marehemu wakiwa wanaingia katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya maziko
Kulia ni Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete,katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na
Abdulrahman Omari Kinana wakiteta jambo katika msiba wa Mrema
Abdulrahman Omari Kinana wakiteta jambo katika msiba wa Mrema
Wake wa marehemu Mrema wakiwa katika huzuni kulia aliyevalia suti nyeusi ni baba mzazi wa Bilionea huyo
Mh Abdulrahman Omari Kinana mara baada ya kuweka shada la maua
Jeneza la marehe Bilionea Maleu Mrema likiwa linashushwa katika nyumba yake ya milele
Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete
Nyumba ya milele ya Bilionea Maleu Mrema
Comments
Post a Comment