SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI MKOA WA SHINYANGA
Maadhimisho
ya siku ya Kifua Kikuu Duniani “World TB Day” mkoa wa Shinyanga
yamefanyika katika machimbo ya dhahabu ya Nyangarata kata ya Lunguya
halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.
CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO CHATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO KANISA KUU LA KKKT SHINYANGA
Chama
cha watu wenye ualbino nchini (Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza
kampeni ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika nyumba za ibada
ambapo leo viongozi wa chama hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la
KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.
Balozi Seif atembelea Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa miundombinu ya Ujenzi ya Garware mjini Mumbai, India
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa miundombinu ya Ujenzi ya Garware
yenye Makao Makuu yake Mjini Mumbai Nchini India imeonyesha nia yake
ya kutaka kujenga Ukumbi Mpya wa Kisasa wa Kimataifa wa Mikutano
Zanzibar endapo itapata fursa ya kufanya kazi hiyo.
Uwamuzi huo umekuja kufuatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na
mpango wa Kutaka kujenga Ukumbi wenye hadhi hiyo katika azma yake ya
kuimarisha Sekta ya Utalii inayoonekana kuimarika na kuleta ufanisi
mkubwa.
Mkurugenzi Miradi wa Kamuni Garware Bwana Deepak Menghnani
alithibitisha hilo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mwishoni mwa ziara ya Wiki Moja ya
Ujumbe wa Zanzibar hapo katika Hoteli ya Kimataifa ya Eros Mjini New
Delhi India.
Bwana Deepak Menghnani alimthibitishia Balozi Seif kwamba Wahandisi
wa Kampuni ya Garware iliyoanzishwa karibu miaka sita iliyopita wana
uwezo wa Kujenga Jengo la Mikutano katika kipindi kisichozidi miaka
Mitatu kwa mujibu wa uwezo wa mahitaji ya muhusika.
Alisema teknolojia rahisi inayotumika katika Kampuni hiyo imewawezesha
Wataalamu na Wahandisi wake kuendesha ujenzi wa Mjengo tofauti ikiwemo
Hospitali, Skuli, Ofisi za Serikali na hata Taasisi Binafsi pamoja na
nyumba za Makaazi kwa bei inayomuwezesha mtu wa kawaida kumudu
kununua.
Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa miundombinu ya
Ujenzi ya Garware alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
Taasisi hiyo ya ujenzi imekuwa ikishirikiana na Wahandisi waliobobea
kutoka Nchini Misri ili kuiwezesha kuwa na uhimili wa Kimataifa.
Bwana Deepak Menghnani alisema Garware tayari imeshatoa huduma za
ujenzi katika Mataifa ya Bukinafaso,Sri Lanka na Dubai ndani ya
kipindi cha miaka Minane tokea kuanzishwa kwake.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuuandalikia barua ya
mualiko Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni hiyo katika muda mfupi ujao ili
kujionea mazingira ya Zanzibar na kuona hatua gani zinastahiki
kuchukuliwa katika mwanzao wa kuelekea kwenye mpango huo wa ujenzi wa
Ukumbi wa Kimataifa.
Balozi Seif alisema Zanzibar imeshafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika
uimarishaji wa Sekta ya Utalii lakini kinachokosekana kwa wakati huu
ni uwepo wa Ukumbi wa Kimataifa unaotoa fursa kwa Wageni na hata
Nchi
rafiki kuelekeza nguvu zao za kufanya makongamano, Mikutano na hata
Vikao vya Kimataifa.
“ Zipo kumbi za Mikutano zinazotumika katika baadhi ya Mahoteli Mjini
na sehemu za Vijijini Zanzibar lakini hazikidhi mahitaji halisi
kutokana na udogo wake ”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema ipo mikutano na baadhi ya semina za Kimataifa
zinazopangwa kufanyika Visiwani Zanzibar lakini wajumbe wa Mikutano
hiyo hulazimika kuishi mbali na maeneo yao ya mikutano jambo ambalo
huleta usumbufu wa kujipangia mambo yao mengine binafsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemaliza
ziara yake Nchini India na sasa amewasili Dubai kwa Mapumziko mafupi
ya siku mbili na baadae atarejea Nchini Tanzania kuendelea na majukumu
yake.
KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YARIDHISHWA NA MIRADI YA TASAF, TAMISEMI , MKURABITA NA MFUKO WA RAIS WA KUJITEGEMEA MKOANI NJOMBE.
Kamati
ya kudumu ya bunge Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea mkoani
Njombe na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii-TASAF,TAMISEMI, Mfuko wa Rais wa Kujitegemea na MKURABITA na
kuridhishwa na mchango wa taasisi hizo katika kupiga vita umasikini kwa
kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Wakiwa
mkoani humo,wajumbe wa Kamati hiyo walikutana na Walengwa wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ambapo licha ya kuvutiwa
na hatua ya kujiongezea kipato kutokana na ruzuku kwa kuanzisha miradi
midogo midogo, lakini pia walipongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika sekta za elimu, afya na lishe katika kaya za walengwa hao.
Aidha
wajumbe wa kamati hiyo ambao waliongozana na Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah
Kairuki pia wamepongeza hatua ya TASAF ya kupunguza tatizo la makazi ya
walimu kwa kujenga nyumba katika kijiji cha Uwemba nje kidogo ya mji wa
Njombe.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Mhe.Kairuki amesema serikali itaendelea kuweka mkazo
katika miradi inayolenga kuwapunguzia wananchi adha ya umasikini hivyo
akataka wananchi kuitumia fursa hiyo vizuri ili waweze kuboresha maisha
yao.Waziri huyo alionyesha kuridhika na baadhi ya wananchi mkoani Njombe
kwa kutumia fursa zilizowekwa na serikali kuendesha shughuli za
kiuchumi kikiwemo kilimo,ufugaji ,biashara na uanzishaji wa vikundi vya
kuweka akiba.
Kwa
Upande wa MKURABITA,Wajumbe wa Kamati hiyo walipata ushuhuda kutoka kwa
baadhi ya wananchi ambao wamepata mikopo kwa kutumia hati za ardhi
iliyopimwa chini ya Mpango huo ambao baadhi yao wameweza kupanua
biashara zao baada ya kukopa fedha kwa wastani wa shilingi milioni 80 na
kurejesha mikopo hiyo kwa wakati
Kwa
upande wake Mwenyekiti aliyeongoza wajumbe hao,Mhe. Venance Mwamoto
alitoa wito kwa wataalamu walioko kwenye maeneo ya wananchi kutumia muda
wao mwingi kuwapatia elimu na mafunzo yatakayowawezesha kuboresha
miradi wanayoianzisha ili iwe endelevu na yenye kuleta tija.
Hata
hivyo wanufaika wa mikopo kutoka taasisi za fedha walionyesha kilio chao
kutokana na riba kubwa wanayotozwa jambo ambalo wamedai kuwa linaathiri
maendeleo ya biashara zao na kufifisha nia ya kuendelea kukopa
.Zifuatazo ni picha za ziara hiyo ya kamati ya bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa mkoani Njombe.
Wajumbe
wa kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakikagua ujenzi wa
nyumba ya Walimu inayojengwa na TASAF katika kijiji cha Ulembwe nje
kidogo ya mji wa Njombe.
Wajumbe
wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali Mitaa wakipata
maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba ya Walimu katika kijiji cha Ulembwe
inayojengwa TASAF ikiwa ni jitihada za serikali za kutatua tatizo la
makazi kwa walimu.
Baadhi
ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
, wakisalimiana na walengwa ya TASAF katika kijiji cha Ulembwe mkoani
Njombe katika ziara ya kamati hiyo kukagua miradi ya
TASAF,MKURABITA,TAMISEMI na Mfuko wa Rais wa Kujitegemea.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe ,Christopher ole Sendeka (watatu kulia), baadhi ya
wabunge na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyevaa
Kaunda suti nyeusi ) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walengwa
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Uwemba mkoani
Njombe.
Baadhi
ya walengwa wa TASAF katika wa kijiji cha Ulembwe ,nje kidogo ya mji wa
Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya
kudumu ya bunge waliofanya ziara kijijini hapo .Wakiwa kijijini hapo ule
usemi wa mgeni njoo mwenyeji apone ulidhihirika baada ya Waziri Kairuki
kuahidi kumsomesha mmoja wa watoto kutoka kaya ya mlengwa hadi kidato
cha nne.
Wajumbe
wa kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa wakipata
maelezo kutoka kwa mmoja wa wananchi walionufaika na fedha kutoka mfuko
wa Rais wa kujitegemea katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambaye
anaendesha kilimo cha viazi mviringo.
Waziri
Kairuki na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala bora na
Serikali za Mitaa wakiangalia bidhaa za ususi zinazofanywa na baadi ya
wanawake kupitia kikundi chao kilichowezeshwa na Mfuko wa Rais wa
Kujitegemea mjini Njombe.
Baadhi
ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa
wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa Mfuko wa Rais wa
kujitegemea mkoani Njombe aliyetumia fedha alizokopeshwa na mfuko huo
kuanzisha mradi wa kufuga n’gombe.
Waziri
Kairuki wa kwanza kushoto akifuatiwa na mhe. Mwamoto,wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Njombe akiwemo mkuu wa
mkoa huo Christopher Ole Sendeka ,nyuma yao ni baadhi ya wanufaika wa
MKURABITA.
Waziri
Kairuki aliyevaa gauni lenye rangi nyekundu na Mwenyekiti wa kamati ya
bunge ya utawala na serikali za mitaa mhe. Venance Mwamoto wakitoa
nasaha kwa baadhi ya wanufaika wa MKURABITA mkoani Njombe.
‘’Karibuni
tena Mkoani Njombe’’ndivyo wanavyoelekea kusema wenyeji kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea
mkoa huo kukagua miradi ya TASAF,TAMISEMI ,MKURABITA na Mfuko wa Rais wa
Kujitegemea.
Waziri
Angellah Kairuki watatu kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na
Mhe.Magreth Sitta na Mhe.Ruth Mollel ambao ni wajumbe wa kamati ya
kudumu ya bunge wa utawala na serikali za mitaa wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ulembwe nje
kidogo ya mji wa Njombe.
AICC yashauriwa kuwekeza Dodoma
Kamati
ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeushauri uongozi wa
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kuelekeza nguvu ya
uwekezji katika mji wa Dodoma ili kuziba kukidhi ongezeko la huduma za
kumbi za kufanyia muikutano linalosababishwa na serikali kuhamia katika
mji huo.
Akizungumza
katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati ya PIC kutembelea AICC
mwishoni mwa wiki na kukagua miradi miwili, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Albert Obama ameshauri AICC kuupa kipaumbele mkoa wa Dodoma katika
mkakati wa kujenga kituo kingine cha kisasa cha Mikutano.
“Tunahitaji
kuiona taasisi hii ikipanuka na kujenga vituo vingine vya mikutano huko
mikoani na moja ya mikoa ambayo tungependa muipe kipaumbele ni Dodoma
maana huko ndio serikali inahamia na mahitaji ya huduma ya kumbi za
mikutano yanakwenda kuongezeka”, alisisitiza Obama.
Nae
Mjumbe wa Kamati hiyo, Amina Mollel alieleza kufurahishwa na juhudi za
uongozi wa AICC kumilisha ujenzi wa mradi wa nyumba za kisasa
(apartment) 48 ambapo azote zina wapangaji na kuwa sehemu muhimu ya
kuongeza mapato ya shirika.
Aidha
ameushauri uongozi wa AICC kuzingati uwekaji wa miundombinu ya walemavu
katika miradi mingine inayotekelezwa ukiwemo mradi wa ujenzi wa ukumbi
wa kisasa kwa ajili ya maonesho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Mei
mwaka huu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Elishilia Kaaya aliieleza
Kamati ya PIC kuwa Kituo kina mipango ya baadae ya kujenga Kituo kingine
cha Kisasa cha Mikutano kitakachojulikana kama Mount Kilimanjaro
International Convention Centre (MKICC) ili kukabiliana na ushindani wa
biashara ya mikutano kutoka nchi za jirani kama Rwanda ambayo tayari ina
Kituo cha kisasa cha Kigali na Kenya ambayo tayari inatarajia kujenga
Kituo cha kisasa cha Mikutano huko Mombasa.
Kaaya
ameeleza kuwa AICC imefanikiwa kununua ekari 23 katika mji wa Mtwara na
pia inatafuta ardhi katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Iringa kwa ajili
ya kujenga Vituo vingine vya Mikutano. Aidha alieleza Kamati kuwa mbali
na kujenga Vituo vya Mikutano, AICC inatarajia kujenga miundombinu kwa
ajili ya Wanajuiya ya Kidiplomasia eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji
wa Arusha ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imetenga eneo kubwa kwa ajili ya taasisi mbalimbali za
kimataifa kujenga ofisi.
Mbali
na biashara ya mikutano, AICC inajishughulisha pia na upangishaji wa
ofisi na nyumba na pia inatoa huduma za afya kupitia hospitali yake. Pia
AICC inamiliki Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo
Dar es Salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiwa
katika mradi wa nyumba za kisasa za kupangisha za AICC ambapo mradi huu
umekamilika na tayari nyumba hizo zimeisha pata wapangaji.
Mkurugenzi
wa Miliki na Miradi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha
(AICC), Victor Kamagenge (kushoto) akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya
Uwekezaji Mitaji ya Umma, juu ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa
maonesho. Kamati hiyo ilitembelea AICC mwishoni mwa wiki kukagua miradi
miwili ya ujenzi wa ukumbi wa maonesho ambapo ujenzi wa unaendelea na
mradi mwingine wa nyumba za kisasa 48 ambao tayari umekamilika.
Comments
Post a Comment