MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mkurugenzi
Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiwasilisha mada kwa wadau kutoka
kwenye asasi za kiraia, maafisa mipango wa wizara mbalimbali pamoja na
watafiti kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya
kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
FORUMCC
imeandaa mkutano na kukutanisha wadau kujadili namna ya kuongeza
jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya
Tabianchi katika mipango na bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa
hapa nchini Tanzania.
Mkutano
huo umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na
serikali ili kuangalia njia nzuri zinazoweza kusadia Tanzania kuwa na
mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza kutegemea zaidi fedha
kutoka kwa wafadhili.
Lengo
la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau kujadili na kuhamasisha jitihada
za kuingiza masuala ya mabadiko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya
Serikali katika kipindi hiki tunapoelekea katika Bunge la bajeti ya
mwaka 2017/18.
Akizungumza
kwenye mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji
toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi amesema serikali kupitia TAMISEMI iko
karibu na wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza
kupunguza majanga mbalimbali hapa nchini, na wao TAMISEMI wana jukumu la
kubwa kwenye asasi za kiraia kuingia kwenye miradi inayohusu mabadiliko
ya Tabianchi.
Pia
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona aliwaomba wadau mbalimbali
waliofika kwenye mkutano huo kushirikiana na FORUMCC ili kuweza kufikia
malengo waliyojiwekea kwenye suala la mabadiliko ya Tabianchi
linalotishia maendeleo ya jamii za mbalimbali na ukuaji wa uchumi nchini
Tanzania.
Mkutano
huo uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na
Teknolojia) leo uliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,
maafisa mipango kutoka wizara mbalimbali, watafiti na waandishi wa
habari.
Mkurugenzi
Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi
akitoa mada kuhusu kazi za TAMISEMI pamoja na ushirikiano wake kwenye
masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye
kumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali
pamoja na kutoa maoni kwa maofisa wa wizara kuangalia namna ya
kushirikiana ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano
ukiendelea uliowakutanisha wadau mbalimbali uliowakutanisha ili
kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya
kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
Mtaalamu
wa Masuala ya Nishati, Erneus Kaijage akiwasilisha mada kuhusu
uwekezaji wa fedha katika sekta ya nishati kwenye mkutano
uliowakutanisha wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi leo jijini
Dar es Salaam
Baadhi
ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakichangia mada pamoja na kuuliza
maswali kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya
kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti kwenye
mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na
Teknolojia) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi
akijibu maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wadau mbalimbali wa masuala ya
mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliowakutanisha wadau hao kwenye
ukumbi wa Chuo cha Sayansi jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa
na wadau mbalimbali waliokutana ili kujadili namna ya kuongeza jitihada
katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi
katika mipango na bajeti.
Mwezeshaji
wa Mkutano wa FORUMCC, Abdallah Henku akizungumza jambo kwenye mkutano
huo uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Baadhi
ya wadau mbalimbali walioshiriki kutoka asasi za kiraia, maafisa
mipango kutoka wizara, watafiti na waandishi wa habari wakifuatilia mada
zilizokuwa zikiendelea kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na
Teknolojia) mkutano ulipofanyika leo ulioandaliwa na FORUMCC.
Picha ya Pamoja
BALOZI WA KOREA AKABIDHI MAKTABA YA KISASA KWA SERIKALI YA TANZANIA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Serikali
ya Korea kupitia mradi wa ''Thank you Small Ribray program'' leo
imekabidhi Vifaa na kuzindua maktaba ndogo ya kisasa katika ofisi za
makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo balozi wa Korea nchini
Song Geum Young amesema kuwa serikali yake licha ya kusaidia serikali
katika miradi mingi lakini kwa sasa wameamua kusaidia katika kuwawezesha
watoto kupata elimu inayoendana na wakati.
"sisi
kama korea tunaamini kuwa ukimpa mtoto elimu umeweza kumpa maisha ya
kesho, hivyo vifaa hivi vitaweza kuwasaidia katika kukuza taaluma yao "
amesema Balozi.Balozi ametoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto waweze
kutumia maktaba hiyo kwa kutumia sehemu hiyo kwa ajili kukuza taaluma
yao .
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea
nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah Mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa wakikata utepekuashiria uzinduzihuo.
Balozi
wa Korea nchini , Song Geum Young akizungumza kabla ya uzinduzi wa wa
Maktaba ya kisasa ambayo imetolewa na Serikali ya korea.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo, akikabidhi vitabu kwa
Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa , Audax Mabula akizungumza kabla ya
uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika Makumbusho ya Taifa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akizungumza kabla ya
uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika ukumbi wa Makumbusho ya taiafa kwa
msaada wa Serikali ya watu wa Korea.
Baadhi ya wadau walioshiriki tukio hilo
Viongozi mbalimbali akiwemo na balozi mteule wa korea wakifatia hotuba ya balozi
Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakishuhudia tukio hilo
Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah akizungumza na waandishi wa habari
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika
Maktaba ya Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika
Maktaba ya Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea
nchini , Song Geum Young wakipata maelekezo jinsi ya namna vifaa vya
kielektronic vinavyofanya kazi katikakutoa elimu kwa watoto ndani ya
maktaba hiyo ambayo imefadhiliwa na serikali ya Korea
Picha
ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa
na Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah wageni
waalikwa wengine waliohudhuria katika hafla hiyo
COCA-COLA YAZIDI KUHAMASISHA WANAFUNZI KUTAMBUA NA KUKUZA VIPAJI VYAO
Wafanyakazi
wa Coca-Cola wakiwagawia wanafunzia wa Shule ya Sekondari ya Olorieni
Vinywaji vya Coca-Cola katika eneo la shule hiyo.
Mwanafunzi
wa Shule ya sekondari ya Olorieni akionyesha kipaji cha kucheza na
Baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko
katika shule mbalimbali.
Wanafunzi
wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kucheza na
baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko
katika shule mbalimbali.
Wanafunzi
wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso (jukwaani)
huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya
Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
Wanafunzi
wa wawili wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha
kucheza muziki kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola katika
shule mbalimbali.
Mwongozaji
wa Promosheni (Supervisor) Onesmo Swila Akimkabidhi zawadi ya mipira ya
miguu mwalimu wa michezo wa shule ya Sekondari ya Olorieni katika
promosheni yao ya Onja msisimko na Coca-ola inayoendeshwa katika shule
mbalimbali jijjini Arusha.
Wanafunzi
wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kuimba kupitia
promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule
mbalimbali.
Wanafunzi
wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso (jukwaani)
huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya
Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
Wanafunzi
wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakigongeana sheazi mara baada ya
kugawiwa vinywaji kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja
msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha. (Picha na Ferdinand
Shayo).
Kampuni
ya Bonite Bottlers Kupitia kinywaji chake cha Coca-Cola imezidi
kuhamsisha wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao kupitia Promotioni
ya Onja Msisimko na Coca-Cola wanayoiendesha katika shule mbalimbali
jijini Arusha. Cocacola imefanya hayo katika shule Sekondari ya Olorieni
jijini Arusha ambapo baadhi ya wanafunzi walipata Fursa ya kuonyesha
vipaji vyao ikiwemo kucheza na baiskeli katika jukwaa, kucheza muziki
pamoja na kuimba. Msimamizi wa promosheni hiyo Onesmo Swila amewataka
wanafunzi katika shule hizo wanazotembelea ikiwemo Sekondari ya Olorieni
ambayo wameitembelea, kuendeleza vipaji vyao kwa kila fursa wanayopata
kwa kuwa kipaji ni hazina.
“wanafunzi
acheni kuficha vipaji vyenu, vionyesheni, ili mpate fursa ya kuvikuza,
sisi Coca-Cola tumeamua kuwahamasisha kwa lengo kuwatia moyo ili mfikie
malengo yenu.” Alisema Onesmo Aidha licha ya kuwashukuru walimu wa shule
hiyo kwa kuwakubalia kutembelea shule hiyo na kuwagawia wanafunzi
zawadi ikiwemo ya kinywaji cha Coca-Cola, amesema ziara hiyo wataendelea
nayo katika shule mbalimbali jiji Arusha ili kuwaonjesha wanafunzi
Msisimko wa Coca-Cola.
Mwalimu
wa Michezo katika Shule ya Sekondari ya Olorieni, Haroon Maluli
akipokea zawadi ya Mipira kutoka Coca-Cola, Ameshukuru kwa zawadi hiyo
huku akiwasihi wanafunzi kutoficha vipaji vyao, bali wavionyeshe kwa
kila fursa inayopatikana ili kuvikuza zaidi. “Tunashukuru kwa zawadi ya
mipira, ila nawasihi wanafunzi kutumia fursa kama hii iliyoletwa na
Coca-Cola kuonyesha vipawa vyenu, kwani hata sisi tulivyokuwa tunasoma
hatukuvificha ndio maana tupo hapa” alisema Mwalimu Haroon.
MUWSA WATUMIA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KUOTESHA MITI KATIKA VYANZO VYAKE VYA MAJI.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) wakishusha miti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya vyanz vya
maji vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) John Ndetiko akiwa amebeba mti tayari kwa ajili ya kuotesha
kando ya chanzo cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisaidia katika zoezi la ubebabji miti kwa ajili ya kuotesha.
Wafanyakazi wa MUWSA wakiwa wamebeba mit kwa ajili ya kuotesha katika chanzo cha maji cha Shiri.
Kaimu Mkurugenzi wa MUWSA,John Ndetiko akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji cha Shiri.
Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiotesha miti katika chanzo hicho.
Hii ni
sehemu ya mitiiliyooteshwa Mwaka jana katika eneo hilo zoezi
lililooongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Saidi Mecky Sadicki.
Huu ndio mti uliooteshwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Mecky Sadicki katika eneo hilo.
Chanzo
cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai kinachoimamiwa na Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi.(MUWSA.)
Wafanyakazi
wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kuotesha miti katika chanzo hicho.
Chanzo kipya cha maji cha Mkashilingi kilichopo jirani na chanzo cha chemichei cha Shiri.
Comments
Post a Comment