Posts

Showing posts from March, 2017

SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI MKOA WA SHINYANGA

Image
Maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani “World TB Day” mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika machimbo ya dhahabu ya Nyangarata kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala wilayani Kahama. CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO CHATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO KANISA KUU LA KKKT SHINYANGA Chama cha watu wenye ualbino nchini (Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza kampeni ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika nyumba za ibada ambapo leo viongozi wa chama hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.   Balozi Seif atembelea Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa miundombinu ya Ujenzi ya Garware mjini Mumbai, India Na Othman Khamis Ame, OMPR Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa miundombinu ya Ujenzi ya Garware yenye Makao Makuu yake Mjini Mumbai Nchini India imeonyesha nia yake ya kutaka kujenga

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI Simu:   +255-22- 2112035/40 Nukushi: +255-2122617/2120486 Baruapepe: ps@moha.go.tz        9 Barabaraya Ohio               S.L.P.   9223 11483 DAR ES SALAAM                                                                                                TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha Cheo Maafisa sita wa Uhamiaji kuwa Makamishna wa Uhamiaji kuanzia tarehe   28 mwezi Februari mwaka 2017, Wakati huo huo amewateua kushika   nyadhifa   mbalimbali katika Jeshi la Uhamiaji. Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka, Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald J

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiwasilisha mada kwa wadau kutoka kwenye asasi za kiraia, maafisa mipango wa wizara mbalimbali pamoja na watafiti kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti. FORUMCC imeandaa mkutano na kukutanisha wadau kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa hapa nchini Tanzania.  Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikali ili kuangalia njia nzuri zinazoweza kusadia Tanzania kuwa na mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili. Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau kujadili na kuhamasisha jitihada za kuingiza masuala ya mabadiko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya Serikali katika kipindi hiki tunapoelekea katika Bunge la