KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
|
|
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS
RELEASE
HATIMAYE NJIA YA RELI KATI YA DAR ES SALAAM
NA RUVU YAFUNGULIWA !
Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9
alasiri leo Januari 30, 2017 njia ya
reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es
salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli.
Taarifa
hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali
l kutoka relini na pia kuikarabati
sehemu iliyo haribika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari 29,
2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017.
Aidha
treni ya abiria iliyoahirisha safari ya
kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo
saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara..
Wakati
huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O.
Bango kutoka Bujumbura Burundi akiwa
anasafiri kutoka Kigoma amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani
wa Pwani kwa ajili ya matibabu zaidi. Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa
kulia hivyo basi kuhitaji kushonwa mguu wake huo.
Taarifa
kutoka Muhimbili zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa
hospitalini hapo usiku wa Januari 29, 2017. Majeruhi wamefamika kuwa ni Nd.
Stephania Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili kuendelea na
matibabu ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha ya kawaida na
anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu
ya ugonjwa wake wa tumbo.
Mgonjwa
wa pili Nd Alice Jovin (37) mkazi wa Salasala
Dar es Salaam alikuwa anatoka Kigoma kuja Dar es Salaam amepata majeraha
ya kawadia ametibiwa na alitarajiwa kuruhusiwa leo asubuhi.
Kuhusu
idadi ya wasafiri treni ya Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya
1000 wakati inapata ajali ilikuwa na abiria 480.
Aidha
imefahamika kuwa ili kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa rasmi
itatolewa baada ya uchunguzi wa Kamati maalum
inayoundwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa.
Taarifa hiyo itatolewa baada ya wiki mbili.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Januari 30, 2017
DAR ES SALAAM
30 JANUARI, 2017
Comments
Post a Comment