VIUNO PAB YATEKETEA KWA MOTO ZINZA MUGABE DAR
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Dar es Salaam, wakizima moto ulioteketeza nyumba ya biashara iliyojulikana kwa jina la VIUNO PAB iliyopo Sinza Mugabe.Inadaiwa jumla ya Sh Milioni 10 zimeteketea katika Pab hiyo leo
Hata hivyo wenye nyumba wawe na huruma, hata wanaopanga yawapasa kuwatafuta wtuwa kuzuia majanga ili kujilidhisha kama kweli sehemu anayopanga ataweza kufanya biashara kwa uhakika je moto ukitokea ataweza kuokoa mali zake.
Inadaiwa Pab hii ipo katika kichochoro mabacho kinatenganisha nyumba moja hadi nyingine sas huu uichochoro ulikuwa unamilikiwa na nani kwa kawaida huo ni mali ya serikili haipaswi kupangishwa labda kwa kupandwa mit tu.
Uzembe wa wafanyakazi wa Serikali kufuatilia uzibaji wa sehemu hizo inabidi ufanyika msako wa kubomoa vichochoro vilivyozibwa kinyume cha sheria, kama usingekuwa umezibwa nyumbambili zisingeteketea, kungekuwa na sehemu ya kupita.
Askari hao wakipata taabu kuzima moto huo pa kupitia kwenda upande mwingine inakuwa vigumu kutokana na ujenzi wake.
Evarist Otalo, mpgapicha wa kituo cha ITV, akiwajibika katika tukio hilo
Askari Polisi wa kituo cha Urafiki nao walifika katika tukio hilo
Manispaa ya Kinondoni kitengo cha biashara huenda nao kama hawapo nguzo ya umeme imepitishwa eneo hilo na jiko la chipsi lipo hapohapo ikitoke hitilafu lolote linaweza tokea
Askari akishuhudia unavyopamba moto
Tanesco walichelewa katika eneo hilo umeme na moto ukawa unashindana
Mfanyakazi wa tanesco akikata umeme
Wakibomoa paa la nyumba ili waweze kuzima moto uliokuwa ukiteketeza kenji za nyumba hiyo
Mmoja wa wamiliki wa nyumba hiyo akilia
Polisi wakiwajibika
Mmoja wa wamiliki wa Viuno Pab makihojiwa na wanahabari na kudai amepoteza zaidi ya Sh Milioni 10
Comments
Post a Comment