MATUKIO MBALIMBALI LEO
Mwandishi wa Kituo cha ITV mkoani Arusha,Khalfan Lihundi,akizungumza jana na waandishi wa habari nje ya Kituo cha Polisi cha Usariver,wilayani Arumeru mkoa wa Arusha baada ya kuachiwa kwa dhamana ambapo alishikiliwa kwa zaidi ya saa 24 kituoni hapo akidaiwa kuandika habari za migogoro ikiwemo ya ardhi na maji katika wilaya hiyo PICHA NA JANETH MUSHI
Akitoka mahabusi akiwa ameogozana na wanahabari wenzake
WAZIRI MKUU APOKEA FEDHA ZA MAAFA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT, Dkt. Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msada wa shilingi milioni 10 uliotolewa na kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt. Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msaada wa Shilingi milioni 10 ukiwa ni mchango wa kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam

KAMANDA MPYA WA POLISI SINGIDA AANZA KAZI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,
Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) DEBORA MAGILIGIMBA akikagua gwaride la
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Singida mara baada ya kuteuliwa
kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo. Kamanda Debora anachukua nafasi ya marehemu
SACP PETER KAKAMBA aliyefariki hivi karibuni kwa maradhi ya tumbo. (Picha na
Shabani Marissa, Mwandishi wa Habari wa Jeshi la Polisi Singida)
Comments
Post a Comment