EWURA YAIDHINISHA 8.5 % YA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix
Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya
ongezeko la bei ya umeme, Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Umeme, Godfrey
Chibulunje katikati Meneja Mawasialiano wa mamlaka hiyo Titus Kaguo.
Na
Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeidhinisha asilimia 8.5 ya
ongezeko la bei ya huduma za umeme ili kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.
Ongezeko
hilo limetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Felix
Ngamlagosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maombi ya kurekebisha
bei za umeme ambapo marekebisho hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia Januari
Mosi mwaka 2017.
Ngamlagosi
amesema kuwa TANESCO iliomba kuidhinishiwa ongezeko la bei ya huduma hizo ili
kuliwezesha shirika hilo kupata fedha za kulipia gharama za uendeshaji, kupata
fedha za uwekezaji katika miundombinu pamoja na kuhakikisha huduma ya umeme
inawafikia asilimia 75 ya wananchi wote ifikapo mwaka 2025.
”Baada
ya TANESCO kuwasilisha taarifa zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha maombi
yao, EWURA ilifanya mikutano ya taftishi, matangazo kwa umma pamoja na kushirikisha
wadau mbalimbali kutoa maoni juu ya ongezeko hilo ambapo baada ya uchambuzi wa
maoni hayo tulilidhia kuongeza asilimia 8.5 tu ya ongezeko la bei hizo ,”
alisema Ngamlagosi.
Mkurugenzi
huyo ameongeza kuwa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa
jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa asilimia 5.7 ya bei ya umeme badala ya
asilimia 19.1 iliyoombwa na TANESCO.
Amefafanua
kuwa kulingana na marekebisho yaliyofanyika, jumla ya mapato yanayohitajika kwa
mwaka 2017 ni shilingi bilioni 1,608.47 ambayo ndiyo iliyopelekea ongezeko la
bei la wastani wa asilimia 8.5 hivyo gharama za umeme zimeongezeka kutoka
shilingi 242.34 kwa uniti moja hadi shilingi 263.02 kwa uniti moja.
Aidha,
Mkurugenzi huyo ametoa maagizo kwa TANESCO yakiwemo ya kuanzisha tozo ya mwezi
ya shilingi 5,520 kwa wateja wa kundi linalohusisha viwanda vidogo, mabango na
minara ya mawasiliano, kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuacha kuwaunganisha
wateja wadogo kwenye kundi la wateja wakubwa na badala yake kuwaonganishe moja
kwa moja katika kundi la wateja wadogo.
Amewataka
wananchi kuelewa kuwa kundi linalojumuisha wateja wa majumbani ambao matumizi
yao ya umeme hayazidi uniti 75 kwa mwezi hawataathirika na ongezeko hilo la
bei.
Comments
Post a Comment