NAPE AVIFUNGIA VITUO VYA REDIO DAR NA ARUSHA
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akitoa tamko la kufungia vituo viwili vya redio ambavyo ni Kituo cha Redio Five Arusha na Magic FM Dar es Salaam kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kutokana na kukiuka Kanuni za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 kwa kurusha hewani vipindi vyenye maudhui ya uchozezi,na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo vya Habari Bw. Jamal Zuberi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia tamko alilokuwa akitoa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) la kufungiwa kwa Redio Five Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam leo Agosti 29,2016 Jijini Dar es Salaam.
Serikali yafungia vituo viwili vya
redio nchini kutokana na kurusha hewani taarifa za kichochezi zinazoweza kuchangia
uvunjifu wa amani.
Tamko la kufungwa kwa vituo hivyo vya
redio limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni
,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari.
Aidha,Waziri Nape alivitaja vituo
hivyo kuwa ni Kituo cha Redio Five cha Arusha na Kituo cha Redio Magic FM
Dar es Salaam na alisisitiza kuwa utekelezaji wa tamko hilo unaanza leo tarehe
Agosti 29, 2016 mara baada ya kutangazwa.
“Uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo
umefikia baada ya kujiridhisha kuwa kipindi cha MATUKIO kilichorushwa tarehe 25
Agosti ,2016 muda wa 02:00 usiku hadi 03:00 usiku na Kituo cha Utangazaji
cha Redio Five Arusha na kipindi cha cha Morning Magic katika
kipengele cha KUPAKA RANGI kilichorushwa tarehe 17 Agosti, 2016 kati ya saa
01:00 asubuhi na saa 02:00 asubuhi vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza
kuleta uvunjifu wa amani na hivyo kukiuka masharti ya kanuni ya 5 (a),(b),(c)
na (d) pamoja na Kanuni ya Huduma za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005”, alisema
Waziri Nnauye.
Waziri huyo mwenye dhamana na vyombo
vya habari nchini alisema vituo hivyo vimefungiwa kwa muda usiojulikana na
ameelekeza Kamati ya Maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza
kwa kina zaidi na kumshauri hatua zaidi za kuchukua kwa mujibu wa Kanuni za
Utangazaji za mwaka 2005.
Pamoja na hayo Waziri Nape
alivitahadharisha vyombo mbalimbali vya habari ,kutoshawishika
kuvunja Sheria na Kanuni zinazoongoza tasnia ya Habari ili kulinda
heshima ya tasnia ya habari na kuhakikisha nchi inabaki na Amani.
Comments
Post a Comment