KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo Tanzania imeingia ubia na migahawa ya Samaki


Meneja wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.


 Meneja wa Huduma za Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa wa Samaki samaki, Saum Wengert wakionyesha mkataba wa ushirikiano wa kibiashara waliosaini kati ya kampuni ya Tigo na Mgahawa huo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar Es salaam.



 KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo Tanzania imeingia ubia na migahawa ya Samaki samaki kwa lengo la kufanya kazi pamoja kwa kuleta bidhaa na huduma bora kwa wateja.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Olivier Prentout alisema ushirikiano huo ni moja ya kujenga kwa wateja wa tigo na sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki.
Alisema Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja wake kufurahia intaneti ya kasi na haraka wakati wakila na kunywa  kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vitokanavyo na mazao ya baharini hapa nchini.
“Tunaamini ushirikiano wetu utaendelea kuonyesha ni jinsi gani tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongeza kwenye kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa wateja wetu,”alisema Prentout.
Hata hivyo alisema kuwa migahawa ya Samaki Samaki inapatikana Mlimani City, City Centre na Masaki jijini Dar es Salaam.
Aidha muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki Carlos Bastos alisema kuwa mgahao huo unawafanyia kazi watanzania na wameungana na Tigo ili kuwapatia wateja wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za tigo zilivyo.
“Huduma za Tigo zina ubora wa hali ya juu hususani uzoefu kwenye  mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti. Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa,”alisema Bastos.


Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA