WAZIRI KITWANGA ALA KIAPO CHA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa 

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga  baada ya kumuapisha
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (katikati), mara baada ya Jaji huyo kumuapisha Waziri Kitwanga kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akipandisha ngazi za kuingia Mahakama Kuu wakati alipokuwa anaenda kuapishwa Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya kumalisika hafla hiyo

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu nchini, Shabani Lila (katikati) akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) mara baada ya kumaliza kumuapisha

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA