DKT. KINGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU NA MTOKO WA DIAMOND

MAPEMA ASUBUHI YA LEO DKT. KINGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU YA WATUMISHI WACHELEWAJI WA WIZARA YA AFYA

IMG_9118
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwaamrisha askari wa getini wizarani hapo kuweka kufuli na kutoruhusu mtumishi yoyote wa ofisi hiyo kuingia ndani ya ofisi za wizara ilipotimu saa 1:32 asubuhi mapema leo.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_9122
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akisimamia zoezi la ufungwaji wa geti hilo, Kulia ni askari wa SUMA JKT akiweka kufuli katika lango kuu la kuingia katika ofisi za Wizara ya Afya.
IMG_9123
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwauliza askari wa getini kuhusu daftari la mahudhurio ya watumishi wa wizara baada ya kufungwa geti hilo, na kupewa maelezo kuwa watumishi huonyesha vitambulisho pekee na husaini katika vitengo vyao.
IMG_9139
Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya akiwasili ofisini huku muda wa kuingia kazini ukiwa umepitiliza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na mmoja watumishi wa wizara hiyo na kuagiza kuletewa vitabu vya mahudhurio kwa vitengo vyote vilivyopo wizarani hapo.
IMG_9149
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya, Michael John akitoa maelezo kuhusu mahudhurio ya watumishi kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
IMG_9155
Magari ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya kutambua kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Kigwangalla ametoa agizo la kuizuia watumishi wachelewaji.
IMG_9156
Askari wa getini wakimpa maelezo mmoja wa watumishi wa wizara hiyo kuwa Mh. Naibu Waziri ameagiza watumishi wote waliochelewa kuzuiliwa kuingia ndani.
IMG_9164
Mmoja wa wasaidi wa idara ya rasilimali watu akimkabidhi vitabu vya mahudhurio Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.

Kichupa cha 'Utanipenda' cha Diamond nyuma ya pazia

Diamond platinumz (4)
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kasimama mbele ya magari aliyoyatumia katika video yake mpya ya Utanipenda.
Diamond platinumz (10)Staa wa Bongo, Jacqueline Wolper, akiongea jambo na Diamond.
Diamond platinumz (7)Gari ya Wolper katika video hiyo ikimmwagia maji Diamond.
Diamond platinumz (5)
Diamond akiangalia vipande vya video hivyo kabla ya kuendelea kushuti.
Diamond platinumz (8)Diamond akiangalia Magazeti Pendwa baada ya kupata matatizo, nayo hayakuwa nyuma kuandika.
Diamond platinumz (1)Diamond akipiga kinanda huku akimuimbia mpenzi wake Zari.
Diamond platinumz (12)Mama yake Diamond, Sanura Kasim (kushoto) akifukuzwa na mlinzi baada ya kwenda kuomba msaada kwa JK.
Diamond platinumz (11)Diamond akiongea jambo.
Diamond platinumz (2)Diamond akiwa kapozi na mpenzi wake Zari.

Sasa hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda.
 Ni ngoma kali ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar. Mbali na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo, nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB).
 Itakuwa ni siku ya Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii wengine kibao. Burudani yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000. Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo kikiandaliwa. Video hiyo ni mkono wa yuleyule mkali wa vichupa kutoa Sauzi anayekwenda kwa jina la God Father.
Hajakosea! Amefanya bonge la kazi na hata mashabiki ni mashahidi kwamba wimbo ni mkali na kideo chenyewe ni ‘kitamu’. Maneno mengi siyo ishu, kwenye hili picha zinaongea zaidi hivyo pitisha macho kwenye baadhi ya picha hizo ili upate uhondo! Kwani kuna mtu kaibiwa? Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA