LOWASSA ALIPOKUSANYA UMATI WA WATU JANGWANI

 Mashabiki na wapenzi wa UKAWA, wakipokeza jeneza walilodai ni Chama cha CCM mwaka huu kinazikwa katika historia ya vyama nchini hapo katika uchauzi mkuu wa mwaka huu. Hapa wanaingia katika viwanja vya Jangwani kwenye uzinduzi.
 wakiwa katika Bajaji wakiingia Jangwani
 Waliofika tangu asubuhi wakinywa chai kusubili uzinduzi

 Shabiki akiwa na mfano wa ufunguo aliodai ni wa kufunguliwa mgombea wa ccm Magufuli





 Sugu, Msigwa na Wenje wakibadilishana mawazo

 Lowassa na Duni wakiingia Jangwani


 Uwanja huu haujawahi kupokea watu wengi kama hawa tangu uanze kutumiwa na Binadamu
 Masha, akihutubia
 Mambo Ukawa CCM Umbeya
 Mama Regina Lowassa, akiwamkua wananchi

 Mbowe akizindua Irani ya uchaguzi 2015 hadi 2020
 Akimkabidhi mgombea urais

 viongozi wakionyesha Irani
 Wagombea ubunge  Majimbo ya mkoa wa Dar es salaam

 Kiboko ya Mkapa akizungumza
 Umati huu unawesa kuita upendavyo


 Waziri mkuu kwa miaka 10 Frederick Sumaye, akiuzungumza Jangwani na kutoa siri kibao za watafuna fedha za nchi hii

 Lowassa, akizungumza kwa kuwapaipaumbele chake elimu elimu elimu  toka chekechea hadi chuo kikuuu........ zaeni mtakavyo

 Mfano wa Lowassa, akibebwa na mashabiki kabla ya mkutano kuanza wakishangilia
 Bajaza



 Wasamalia wakimsaidia mwananchi aliyezidiwa kutokana na wingi wa watu





Katiba, Mgeja na Guninita wakiingia uwanjani

 Wasanii wa Wasira wakitumbuiza

 Gari la nne likipeleka Jangwani askari wa kulinda umati huo



 Wakiwasili kwa furaha Jangwani kutokea maeneo ya Magomeni na Kinondoni

 Wakingojea kupita kwenye mataa ya Magomeni
Wimbo wa Taifa ukipigwa
 Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiusalimia umati
 Wakiteta Mbowe na Lowassa
 Wakiteta, Seif na Mbowe
 Masha, akiwasalimia
 Mbowe, akiwa haamini umati huo
 Nimewekwa ndani mimi kuwatisha ninyi nawaambia tusonge mbele ushindi upo wazi, alisema Masha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nndani utawala wa Kikwete huu
 Duni Haji na Lowassa, wakiteta
 Mwenyekiti Bawacha, akihutubia umati na kutoa salamu za wanawake  wa chama hicho kwa muungano wa ukawa
 Lowassa na Mbowe wakiteta



 Salum mwalimu Akimweleza ajambo Lowassa
 Hakii, Juma Duni haji na Maalim Seif Sharif Hamadi
 Nani anasema hatuna Irani ya uchaguzi hii hapa mwaiona


 Motomotomoto, Mwenyekiti wa NLD, Dk, Emmanuel Makaidi,akihutubia umati huo

 Kaimu Mwenyekiti wa CUF, akihutubia umati





Joseph Mbatia, akihutubia umati huo
Hawahesabiki hawa
 mama wa pembe la Ng'ombe kutoka Unguja naye alikuwepo katika uzinduzi huo

 Ni  furaha tu na mikono juu kwa sana



 Mbowe akihutubia umati
 Akipongezana na mgombea baada ya kuhutibia
 Lowassa mabadiliko mabadiliko Lowassa, akisema hivyo Sumaye

Wakifurahi baada ya Sumaye wizi wa kutisha umefanyika serikalini wakati Lowassa, hayupo kwenye utumishi huo miaka nane nani mwizi na Fisadi katika nchi hii kama siyo ccm na serikali yake ya Kikwete



 Sumaye akishangiliwa

Lowassa,mabadiliko mabadiliko Lowassa, akisema Seif wakati wa kuhutubia

 Lowassa na Mbowe wakiendelea kuteta

 Babu Duni haji akinena na wanaukawa jangwani na kuuliza  nani kama mama


 Mwananchi huyu, hakupenda mkusanyiko huo Jangwani , mbona kanuna hivyo

 Tambwe hiza, akiisasambua ccm na kumuomba radhi mzee Makamba, aliyekuwa Katibu wa Mkuu wa CCm Taifa


 Kiboko yao Edwald Lowassa, akiusakimia umati huo  na kisha kuelezea kipaumbele chake  huku akiwataka wampe kura, awape elimu kibao bila malipo kuanzia chekechea hadi mavyuo makuu [popote pale kama yeye alisoma kwanini wengine wasisome hebu mjaribu muone aliwataka waachane na watoa ahadi na irani za kila chaguzi lakini mambo ndo yanadidimia hao si wengine ni ccm






 mwanaukawa, akifuatilia kwa umakini hotuba








 
HAIJAPATA kutokea. Pengine ndilo neno sahihi linaloweza kutumiwa kuelezea umati mkubwa wa watu uliojitokeza  wakati wa uzinduzi wa kampeni za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zilizofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Umati huo ambao uliwaacha watu waliokuwa wakifuatilia mkutano huo katika mshangao, umevunja rekodi ile ya uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao ulifanyika wiki iliyopita katika eneo hilo hilo.
Baadhi ya watu waliohudhuria kampeni za uzinduzi wa Ukawa jana na zile za CCM, wanadai kuwa umati uliojitokeza jana ni mara mbili zaidi.
Katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambako mwanahabri huu aliwezo kufika,  kulikuwa na mikusanyiko ya watu iliyokuwa ikijiandaa kuhudhuria mkutano huo tangu saa 12 asubuhi.
Baadhi ya watu walionekana wakiwa wamevalia sare za fulana na kofia zenye nembo ya vyama vinavyounda umoja huo, na zaidi kukiwa na fulana mpya zenye maandishi yanayosomeka; ‘Malofa’, ‘Malofa katika ubora wetu’, ‘Certified lofa’ na mengine mengi.
Kuanzia saa 12:00  msururu mrefu wa watu katika barabara ya Tandale na Morogoro ukiwa na bendera za vyama hivyo ukitembea kuelekea viwanja vya Jangwani.
Pia barabara ya Morogoro ilifurika magari yaliyokuwa yamebeba wafuasi wa vyama hivyo, walioshika bendera huku wakiimba “Lowassa Jembe” na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa kawaida wa barabara hiyo.

JANGWANI
Katika viwanja vya Jangwani, umati wa watu ulianza kumiminika tangu saa moja asubuhi, huku wengine wakidaiwa kulala viwanjani hapo ili kupata nafasi ya mbele katika mkutano huo.
 katika viwanja hivyo saa moja asubuhi,  zaidi ya watu 300 wakiwa wamekaa huku madereva wa bodaboda na bajaji wakicheza na kuchangamsha eneo hilo.
Viwanja hivyo vilianza kufurika kuanzia saa 4:30 asubuhi ambapo idadi kubwa ya wafuasi waliwasili wakiwa na mabango mbalimbali huku wakicheza kwa nyimbo za kusifu umoja huo.
Baadhi ya watu walionekana wakiwa wamejichora rangi za vyama vinavyounda Ukawa mwilini, huku baadhi wakijitengeneza nywele nyeupe zinazofanana na za Lowassa.
Eneo la mapokezi ya watu wanaowasili lilipambwa na vijana wa kike na kiume waliokuwa wamevalia sare maalumu ambazo ni suruali nyeusi, shati jeupe na skafu nyekundu shingoni.
Jukwaa kubwa lilipambwa na mapambo ya rangi nyekundu, bluu, nyeupe na nyeusi, huku kukiwa na picha kubwa ya mgombea urais huyo, Lowassa pamoja na mgombea mwenza, Juma Duni Haji.
Upande mwingine, kulikuwa na hema kwa ajili ya viongozi wa dini, jukwaa la wasanii pamoja na eneo maalumu kwa ajili ya wanawake, viongozi na waandishi wa habari.
Ilipotimu saa 6:00 mchana, tayari viwanja hivyo vilikuwa vimefurika na saa 6:40 wasanii walianza kupanda jukwaani na kuimba nyimbo mbalimbali za Ukawa na Lowassa.

Mabango
Miongoni mwa mabango ambayo yalikuwa ni kivutio kikubwa uwanjani hapo ni lile la ufunguo mkubwa.
Mengine ni yale yaliyosomeka; ‘Afe beki, afe kipa, Lowassa ndiyo rais 2015’, ‘Goli la mkono ni red card, mechi mbili huchezi mpaka 2025’ na ‘Mzee ukifika Ikulu tuletee Balali ana fedha zetu nyingi’.
Mengine yalisomeka; ‘Lowassa kama maji usipoyaoga utayanywa, usipoyanywa utayaoga, kuyazuia  yatakusumbua’, ‘Malofa na wapumbavu tunaingia Ikulu 2015’ na ‘Malofa katika ubora wetu’.
Kadiri muda ulivyokuwa ukisogea, ndivyo umati mkubwa wa watu walivyokuwa wakiongezeka hali iliyosababisha kuvuka hadi upande wa pili wa barabara ya Morogoro na upande wa Klabu ya Yanga ambako watu walisimama kwenye maghorofa na maeneo ya njia ya kuelekea Hospitali ya Muhimbili.
Baadhi ya wananchi pia waliopanda juu ya ukuta wa Kampuni ya mabasi yaendayo kasi (DART) ili kuushuhudia uzinduzi huo.

POLISI WAMWAGWA
Kwa upande wa ulinzi, ulikuwa imara na uliimarishwa na askari polisi waliokuwa wametanda kila eneo katika uwanja huo.
 kuanzia saa 5:00 asubuhi, magari ya polisi yakiteremsha askari wake na kuwatawanya katika viunga vya Jangwani.
Askari hao walionekana kupewa maelekezo na viongozi wao wakiwa ndani ya kituo cha mabasi ya DART na kisha kutawanyika.
Baada ya muda, iliwasili gari aina ya Defender yenye namba PT 1438 iliyokuwa na polisi zaidi ya wanane huku wakiwa wamebeba silaha.
Ilipofika saa 6:41 mchana, gari jingine la polisi aina ya Yutong liliwasili likiwa limejaa askari, huku likiongozana na magari mawili ya maji ya kuwasha.

VIONGOZI KUWASILI
Viongozi wa Ukawa walianza kuwasili saa 9:00 alasiri. Wa kwanza alikuwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa akiongozwa na king’ora cha pikipiki na magari matatu likiwamo aina ya Range Rover alilokuwa amepanda.
Ilipofika saa 9:43, Lowassa akiwa na mgombea mwenza Juma Duni Haji waliwasili wakiwa katika gari jeupe, likifuatiwa na gari jingine lililombeba mke wake, Regina Lowassa.

KIFAA CHA KUPIGIA PICHA CHADUWAZA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kifaa cha kupigia picha ambacho umoja huo ulilazimika kukitumia kutokana na wingi wa watu kiligeuka kivutio kikubwa.
Kifaa hicho maalumu ambacho kinarushwa angani kwa kutumia ‘rimoti’, kilianza kuonekana tangu saa 9 alasiri kikizunguka juu, jambo ambalo liliwafanya wananchi waliokuwapo katika eneo hilo kupunga mkono huku wakionyesha ishara ya vidole.

WAZIMIA
 Zaidi ya wafuasi watano wa Ukawa wakizimia kwa kukosa hewa kutokana na umati huo mkubwa wa watu.
Kitengo cha huduma ya kwanza kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) kilikuwa makini katika kuwapatia huduma ya kwanza.
Asilimia kubwa ya waliokuwa wanazimia ni wanawake ambao walikuwa wamekaa kwa kubanana katika eneo maalumu walilotengewa.

MADUKA YAFUNGWA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,  katika maeneo ya Kariakoo, baadhi ya wafanyabiashara wakifunga maduka yao kuanzia saa 6:30 mchana na kisha kuelekea Jangwani.

WAGOMBEA UBUNGE DAR
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, uliwatambulisha wagombea ubunge wa Ukawa katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Wabunge hao waliotambulishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ni pamoja na Halima Mdee (Kawe), John Mnyika (Kibamba), Julius Mtatiro (Segerea), Abdallah Mtolea (Temeke), Muslim Hassanali (Ilala), Juma Nkumbi (Kigamboni), Saed Kubenea (Ubungo), Kondo Bungo (Mbagala), Mtulya Said (Kinondoni) na Waitara Mwita (Ukonga).
Hata hivyo, ilibainishwa katika mkutano huo kuwa bado umoja huo unamalizia makubaliano ndani ya siku tatu kuhusu chama gani kisimamishe mgombea katika majimbo ya Segerea na Kigamboni ambayo yana wagombea wawili kila moja.

KURUDI MAJUMBANI
Baada ya mkutano huo uliomalizika saa 11:55, asilimia kubwa ya wananchi walionekana wakitembea kwa miguu kuelekea majumbani mwao.
Idadi kubwa ya watu walionekana katika barabara ya Morogoro wakielekea Ubungo, Kimara na Mbezi hali kadhalika pia katika barabara ya Kigogo kuelekea Mburahati.
Eneo la Mabibo walionekana watu wamekaa vikundi wakiimba nyimbo mbalimbali za kumtaja Lowassa na vyama vinavyounda Ukawa.
Makundi mengine yalionekana yakitembea mwendo wa haraka na mchakamchaka huku wakiimba ‘Magufuli toroka uje’.






Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA