MATUKIO MBALIMBALI LEO

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na akiongea na wananchi wa Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya Mpango Shirikishi wa kuendeleza ardhi na makazi ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Fomu zake za kuwania urais, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi, wakati alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu wa CCM mjini Dodoma leo kwa ajili ya kurejesha Fomu za kuwania urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal. Picha na OMR
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angellah Kairuki akisisitiza namna mabaraza ya ardhi yanavyopaswa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, wakati wa mkutano wa Waziri wa wizara hiyo  na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro



Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe alioambatana nao wakati wa ziara ya kikazi iliyokuwa na lengo la kuongea na wananchi wa Kata ya Makongo leo kuhusu namna bora ya kuwashirikisha wananchi katika kuendeleza ardhi ndani ya kata hiyo kwa maendeleo endelevu na yenye manufaa kwa pande zote mbili yaani wananchi na Serikali. 

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipongezwa na Waziri wake wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Binith Mahenge, baada ya kurejesha  Fomu za kuwania urais, katika Ofisi za Makao Makuu wa CCM mjini Dodoma leo juni 15, 2015 kwa. Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe wake kwa kuahidi na kusisitiza kuwa kufanikiwa kwa mradi wa Makongo kutahamasisha mpango wa ushirikishwaji wa wananchi katika kuendeleza ardhi na kuwa na makazi bora ambapo kufanikiwa kwake kutahamasisha mpango huo kutekelezwa maeneo mengine ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
 Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kulejesha fomu

Mkazi wa Makongo juu Bi Ritha Mbotto akimuuliza swali Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati mkutano na wanchi wa kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwandishi wa habari wa TBC Edward Kondela.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia  wanachama wa CCM, wakati akitoka kwe ye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo, wakati alipotoka kurejesha Fomu za kuwania urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Nyumba yake  ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiteta jambo na Naibu Waziri wake Angellah Kairuki wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Makongo wakimsikiliza  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe wake wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwasikiliza wananchi na kubadilishana mawazo mara baada ya mkutano katika kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Bukoba Mjini Acheni Mwishehe, akimkabidhi  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa fomu zenye majina ya wanachama zaidi ya 6000 waliomdhamini kugombea Urais.
 Samuel Sitta, aakishuka kwenyen gari akiwa na fomu zake kwa ajili ya kulejesha leo mjini  Dodoma

 Akilejesha fomu yake
 Msomi kutoka Morogoro, akiwa na fomu yake baada ya kuchukua leo
 Pprofesa Mark Mwandoshya, akijaza kitabu cha wageni baada ya kuwasili mjini moshi kusaka wadhamini
Akiwa ofisini hapo
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  CCM, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia  wanachama wa CCM, wakati akitoka kwe ye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo, wakati alipotoka kurejesha Fomu za kuwania urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu. Nyumba yake  ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal



 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Mfalme Mswatti wa Swaziland, muda mfupi kabla ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (AU) unaofanyika  Sandton International Conference Center huko Johanessburg Afrika Kusini tarehe 14.6.2015. Aliyesimama kulia ni Mke wa Rais wa Afrika Kusini Mama Tobeka Madiba Zuma


Baadhi ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuhudhuria kikao cha ufunguzi tarehe 14.6.2015. Aliyekaa katikati ni Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sessou Nguesso na kulia ni Mke wa Rais Afrika Kusini Mama Tobeka Madiba Zuma.
 


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sessou Nguesso kabla ya viongozi hao kuhudhuria sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa AU huko Jahanesburg tarehe 14.6.2015.
 Mke wa Rais akisalimiana na Madame Monica Geingob, Mke wa Rais wa Namibia wakati wakisubiri ufunguzi rasmi wa mkutano wa 25 wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaofanyika huko Afrika Kusini.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Madame Getrude Maseko Mutharika, Mke wa Rais wa Malawi kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Marais na Wakuu wa AU.
 


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia Mke wa Rais wa Kenya Mama Magreth Kenyatta wakati wa kikao cha Marais na wakuu wan chi za Afrika.


Wake wa Marais wa nchi mbalimbali za Afrika wakibadilishana mawazo kabla ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Marais wa Afrika unaofanyika huko Johannesburg. Waliokaa kutoka kushoto kwenda kulia ni Mama Magreth Kenyatta, Mama Tobeka Madiba Zuma, Mama Salma Kikwete, Mama Antoinette Sessou Nguesso na Mama Hinda  Derby Itno, Mke wa Rais wa Chad na Mwenyekiti wa OAFLA anayemaliza muda wake.
 



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Ghana Lord INA Draman Mahama wakagti wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais wa AU unaofanyika Afrka Kusini.
 



Mke wa Rais Mama Saloma Kikwete akiangalia moja ya machapisho mbalimbali yanayohusiana na Mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) unaofanyika nchini Afrika Kusini.
 




Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa mkutano wa Sandton Internationa Center unakofanyika mkutano wa wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika huko Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 15.6.2015. Aliyefuatana na Mama Salma ni Mwenyekiti wa OAFLA anayemaliza muda wake Mama Hinda Derby Itno.




Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake ya mwisho kwenye kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Sandton jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini



 Waziri Mkuu, akiwapungia mkono wananchi wa nyumbani kwake waliofika kumpokea uwanja wa ndege  baada ya kuwasili kwaq ajaili ya kuomba udhamini



Akiwshangia wananchi waliofika kumpokea




 Wakipita na matawi mitaani






 Dk. Asha-Rose Mighiro baada ya kuchukua fomu
 Akiwa na mumewe



Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA