MZEE NASSORO MOYO ANAHOJA ASIBEZWE CCM ITAVUNA MAJANGA
Mwanzilishi wa Halakati za Mapinduzi Zanzibar mzee
Nassoro Moyo majuzi ilitangazwa kwamba ametimuliwa katika chama cha mapinduzi
akiwa mwanachama namba 7 kilichomponza mzee huyu ni kusema kweli kwamba
mambo hayaendi vyema kwenye chama chao sasa kimetekwa na ma bwanyenye
wasiopenda kukosorewa na hata Baba wa taifa angekuwa hai hakika angefukuzwa
kwani nae alikuwa haachi kuwakosoa waliopo madarakani
mzee moyo akizungumza kwa masikitiko na mmiliki wa blog hii alipomtembelea nyumbani kwake nje ya mji wa Unguja hivi karibuni
Hakika alikuwa nguzo ya CCm, hapa akiteta na Rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, siku tume ya uchaguzi ilipomtangaza m shindi wa kiti hicho na kuunda serikali ya Maridhiano na chama cha CUF
Mzee Moyo akiwa kwenye picha hii na Rais wa sasa walipomtembelea rais huyo Ikulu na tume yake ya maridhiano yeye akiwa mwenyekiti. Huu ndio ulikuwa mwanzo na mwisho wa kuitwa na mtawala huyo Ikulu. wajumbe wake wawili sasa wametimuliwa ccm tuone mwaka huu itakavyokuwa.
Akizungumza kwa msisitizo
Baada ya mazungumzo tuliamua kupiga picha ya pamoja na kuagana hakika mzee huyu ni hazina kwa nchi ya Zanzibar na tanzania kwa ujumla ila baadhi ya watawala huwa hawataki kuambiwa ukweli.
Comments
Post a Comment