WAZIRI NYALANDU ATIA HATI YA UANZISHWAJI WA JUMUIYA ZA WANYAMAPORI ZA WAGA NA UMEMARU
Waziri wa Maliasili na Utalii, ambaye pia ni rais Mtalajiwa wa Awamu ya tano Tanzania, Lazaro Nyalandu, akizungumza na waandishi wa habari ufisini kwake jijini Dar es Salaam leo kabla ya kutia saini hati ya uanzishwaji wa Jumuiya za Wanyamapori za WAGA na UMEMARUMA zilizopo katika bonde la mto Ruaha pande za Iringa na mbeya.
Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Wakuu wa Idara za Wizara hiyo, Waziri amewataka wananchi wanaozunguka maeneo yaliyohifadhiwa nchini kulinda rasilimali za wanyamapori na kupambana kwa vitendo katika vita dhidi ya ujangili nchini.
Katika hafla hiyo pia Waziri Nyalandu amewaomba waandishi wa habari kuelezea ushiriki wa tanzania katika mkutano wa kasane, Botswana uliokamilika March 25, 2015 na kwamba ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Makamu wa rais Dk. Mohamed Ghalib Bilal.
Katika mkutano huo , Jumuiya za Kimataifa Zimeipongeza Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi 6 za kwanza ,kuanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa London wa Februari 2014.
Waziri Nyarandu, amesema kuwa Tanzania iliungana na Botswana, Chad, Gabon, Ethiopia na Kenya katikam kuanzisha mpango wa "Elephant Protection Initiative " EPI, na jitihada hizo zilizoongozwa na mwana wa Mfalme wa Uingereza Prince Charles,zinaendelea kutekelezwa kwa nchi kupiga marufku biashara ya meno ya Tembo katika kipindi cha miaka 10.
Aidha kutokana na ushawishi wa Tanzania,nchi za malawi na Uganda zimekubali kujiunga na Mpango huo wa kuwalinda Tembo.
Waziri amesisitiza kuwa hatua zitachukuliwa na Wizara yake katika kulinda na kuhifadhi akiba ya meno ya Tembo inayofikia tani 130,000 na tayari tanzania na uingereza zimeanza utekelezaji wa mpango wa "Stop Ivory"wenye lengo la kufanya uhakiki wa akiba ya meno ya Tembo nchini na kutengeneza mfuko wa Kisayansi wa kuyahifadhi na kuyalinda. alisema waziri huyo kijana kabisa katika Wizara nyeti ya nchi hii.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, akisaini hati ya uannzishwaji wa jumuiya za wanyamapori za Waga na Umemaruwa zilizopo katika bonde la mto Ruaha. Utiaji saini huo ulifanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesinde na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji Wanyamapoli David Kanyatti.
Wakihakiki anavyosaini waziri
Akimkabidhi Naibu Katibu mkuu
Akipongezana na kaimu wa wanyamapori
Akizungumza wa msisitizo Waziri baada ya kusaini

Comments
Post a Comment