WABUNGE NA MUSWAADA WA KADHI
Baadhi ya wabunge wakiwa wamesimama kupinga hoja za kutaka kuwasilishwa Muswada wa Mahakama ya Kadhi bungeni wakati wa semina ya wabunge iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma
Waziri Mkuu Mizengo Pinda(katikati),Waziri wa Sheria na Katiba,Dk. Asha-Rose Migiro(kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, William Ngeleja wakisiliza hoja za wabunge kupinga kuwasilishwa Muswada wa Mahakama ya Kadhi bungeni katika semina ya wabunge iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma
Spika wa Bunge ,Anna Makinda, akijaribu kuwatuliza wabunge kuhusu Muswada wa Mahakama ya Kadhi
Mbunge wa Semve, Richard Ndassa, akipinga kuwasilishwa Muswada wa Mahakama ya Kadhi bungeni
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, akipinga kuwasilishwa Muswada wa Mahakama ya Kadhi bungeni katika semina ya wabunge iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma
Jaji wa Mahakama Kuu, Robert Makalamba, akizungumza katika Semina ya wabunge kuhusu Mahakama ya Kadhi iliyoandaliwa na Ofisi y Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma
WABUNGE
jana nusura wazihape kavukavu baada ya kutofautiana juu ya uanzishwaji wa
mahakama ya kadhi nchini.
Hali hiyo ilijitokeza wakati
wabunge hao wakiwa kwenye semina Muswada ya Sheria ya Mabadiliko ya Sheria
Mbalimbali, ambapo miongoni mwa sheria zilizo ndani yake ni ile ya Mahakama ya
Kadhi.
Sakati hilo lilitokea katika Semina kuhusu muswada
huo unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni keshokutwa iliyofanyika katika Ukumbi wa
Msekwa.
Katika semina hiyo, iliyofanyika kwenye
ukumbi wa msekwa, licha ya badhi ya baadhi ya wabunge kutaka kunyanyuka kwenye
viti vyao na kwenda kupigana, wapo waliokuwa wakirushiana matusi ya nguoni.
Awali semina hiyo ilionekana kwenda
shwari ambapo wabunge wote waliokuwa wakisimama bila kujali dini zao ama vyama,
walikuwa wakiupinga mswada huo kwa sababu tofautitofaut.
Katika Semina hiyo ambayo wabunge
waliopata nafasi ya kuchangia walikuwa takribani 38, waliokubali mswada huo
uwasilishwe bungeni ni takribani watano.
Hali ilibadilika baada ya Mbunge wa
Kisarawe, Seleman Jafo (CCM), aliposimama na kuchangia ambapo aliunga mkono
mswada huo.
Alipokuwa akichangia, baadhi ya wabunge
walikuwa wakimshangilia, hali iliyomfanya kususa na kukaa chini huku akiwataka
wabunge waisilamu wakutane baada ya semina hiyo.
Hali hiyo ilizua zaidi vurugu ambapo
baadhi ya wabunge wa CCM na upinzani walisimama wakipinga kauli hiyo na wengine
kutoka nje ya ukumbi huo.
Wabunge waliosimama na kuanza kumpinga
Jafo ni pamoja na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), Mbunge
wa Viti Maalum, Pauline Gekul (Chadema), Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya
(CCM) na Mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje (Chadema).
Wakati hali hiyo ikiendelea, Mbunge wa
Chakwa, Yahaya
Kassim Issa (CCM) na Khatibu Saidi Haji, (CUF) walisimama kwenye viti
vyao na kutaka kwenda kumshambulia machali, kabla ya kuzuiwa na wenzao
waliokuwa wamekaa nao karibu.
Hali hiyo ya vurugu na makelele
iliendelea kwa takribani dakika 10 huku baadhi ya wabunge wakitaka semina
ivunjikee.
Wakati vurugu hizo zikimshinda aliyekuwa
mwenyekiti wa semina hiyo, William Ngeleja, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo, walimuwa wameketi kwenye viti
vyao huku Sipka Amma Makinda akiwa amesimama kuwatuliza wabunge hao.
Baada ya muda alifanikiwa kutuliza vurugu
hizo huku akiwataka kujenga utaratibu wa kuheshimiana na kuwa
wanyenyekevu.
Awali katika mchango wake, Jafo
aliwashangaa wakristo kujifanya wazungumzaji wakubwa kuhusu suala hilo la Mahakama ya Kadhi wakati jambo hilo haliwahusu.
“Nataka niwaambie Serikali msije mkafanya
masihara Muswada huu usiingie bungeni, muswada uje tutafanya ‘amendment’
(marekebisho) huko, na naitahadhalisha Serikali iwe makini katika hili,”
alisema Jafo.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa
(CCM), alisema katika katiba Ibara ya 19 ilishaweka wazi kuhusu suala la uhuru
wa kuabudu kwamba jumuiya zote za kidini zitakuwa nje ya mamlaka za nchi.
Mwenyekiti wa kikao hicho (Ngeleja)
alimtaka Ndasa avute subira kusikia maudhui ya semina hiyo huku akisisitiza
kwamba hakuna kipengele chochote cha Katiba kilichovunjwa.
Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina
(CCM), alisema yeye kama mjumbe wa Kamati ya
Bunge Katiba na Sheria walikutana na makundi 11 ya mashehe lakini yaliukataa
muswada huo.
“Waislamu hawa walisema wao hawaitambui
Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania),
naiomba Serikali kwa jambo hili kubwa la Mahakama ya Kadhi hamuwezi
kulileta kwa marekebisho madogo kama haya.
“Kama mkitaka leteni muswada maalumu wa kuanzisha Mahakama
ya Kadhi baada ya waislamu wenyewe kukubaliana, mimi natambua uhumimu wa
mahakama hii ambazo hata sisi tunazo ila hatutaki Serikali izitambue,” alisema.
Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Isssa
(CUF) alipinga kitendo cha mahakama hiyo kuanzishwa chini ya Bakwata
akidai kwamba Bakwata ni taasisi ya mtu binafsi iliyosajiliwa na Rita kama
zilizovyo taasisi nyingine.
“Suala hili halikubaliki, kwa nini
Mahakama ya Kadhi iundwe chini ya Mufti, au Waziri Mkuu anataka tu kuundwa kwa
mahaama ya Kadhi kwa kuwa alishaahidi, msitakake kuipasua hii nchi.
“Kama Waziri Mkuu yeye aliahidi kwa ajili
ya kuutafuta urais shauri yake ila ni marufuku kuwalazimisha watu kuwa chini ya
Bakwata, kufanya hivyo ni kukiuka Katiba.
“Huyu
Mufti anapatikana kwa mujibu wa Katiba ya Bakwata, na Bakwata ni taasisi tu,
Waziri Mkuu anajua suluhisho la jambo hili.
“Tume ya watu 25 iliundwa kulishughulikia,
baadae ikawaundwa ya watu watano kupanga muundo wa Mahakama ya Kadhi, lakini
leo hii anawapa Bakwata, Waziri Mkuu ndio chanzo cha yote haya, suala hili
halikubaliki na tutalipinga,” alisema.
Mbunge wa Kasulu Mjini,Moses Machali
(NCCR-Mageuzi) alisema wabunge hao wanakosea kulijadili suala hilo na kwamba tayari limeleta mgawanyiko
baina ya waislamu wenyewe.
“Inawezekana Waziri Mkuu aliahidi jambo
hili kwa malengo ya urais, na kama muswada utaingizwa ndani ya Bunge, na sisi
wakatoliki tutaleta mabadiko yetu ya Canon Laws, huko Mbeya na wenyewe
madhehebu yao yote wataleta mabadiliko yao,” alisema.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa (CCM),
aliitaka Serikali kusoma alama za nyakati wasiuleta muswada huo bungeni
“Kama Serikali imeamua kuanzisha taasisi
ya kidini itambue kuwa inakiuka misingi waliyotuachia wassisi wa taifa hili,
Mwalimu Julius Nyerere na Abei Aman Abeid Karume, hawa waliposema Serikali
haina dini hawakuwa na akili.
“Hili jambo ni jema lakini nashauri
muswada huu urudishwe ili ukaboreshwe ili uje kwa mapana kuliko kuja hapa
kufanya marekebisho,” alisema.
Mbunge wa Tarime, Nyambari Nywangwine
(CCM) pamoja na kusema kwamba jambo hilo
ni zito alisema taasisi za dini ziliukataa katika Kamati ya Bunge na
kwamba Bakwata walitoa masharti kwamba Serikali igharamie.
“Wakristo wakataka waislamu wenyewe
wakakae kwanza wakubaliane , mimi sina dini ni mpagani nikitaka kuleta sheria
zangu mtazikubali,” alisema.
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini
(Chadema) alisema Serikali isipokuwa makini Bunge linaweza kuingia katika
historia ya kuivuruga nchi.
“Mimi hapa sitaki kuwa sehemu ya historia
hiyo, jambo hili limeligawa Taifa, hakuna ambaye hawasikii maaskofu wanasema
nini na kama hamuwasikii kwani usalama wa
Tiafa hawaambii?
“Tusifungue jini kwenye chupa
lililofungiwa na waasisi wetu halafu baadae likaja kutusumbua,semina hii
mnayotupatia mlipaswa kuwapa maaskofu ambao wana hofu juu ya kuanzishwa kwa
Mahakama ya Kadhi.
“Kwanza Serikali inatenda dhambi
kuwatumia waislamu kutafuta kura, acheni hili jambo nchi hii itakuwa
vipandevipande,” alisema.
Mbunge wa Viti Maalum, Marry Mwanjelwa
(CCM) alisema Nyerere na Karume hawakuwa wajinga waliposema nchi haina dini na
kutahadharisha kuwa Serikali isopokuwa makini inaweza kuliingiza taifa kwenye
machafuko ambayo hayajawahi kutokea na kwamba yeye hata kubali hilo litokee.
Mbunge wa Viti Maalum, Christowaja Mtinda
(Chadema) alisema suala la kuitambua Mahakama ya Kadhi kutaingiza nchi katika
machafuko.
“Hao maaskofu na wachungaji mnaokutana
nao sio hao, sasa hivi tunakwenda kwenye uchaguzi msitake kuwagombanisha
wabunge na wapiga kura wao,” alisema.
Mbunge wa Gando, Khalifa Seuleiman
Khalifa (CUF) alisema Serikali haikujipanga kuleta muswada huo bungeni na
kwamba inatafuta wingi wa waislamu.
“Kama
kweli wana nia na wanawapenda waislamu walete muswada kalimi na sio kufanya
haya marekebisho, huu mnaoufanya ni unafiki ambao Mungu hapendi.
“Serikali iende ikajiande
upya na kama suala ni hofu ya gharama za
kuendesha mahakama hizo waislamu watalipia au hata wafadhili kwani nyie mangapi
mnafadhiliwa, hapa sasa hivi tutawanyike tukafanye mengine,” alisema.
Mbunge wa Mbozi Magharibi, Davi Silinde
(Chadema) alimshukia Waziri Mkuu kwa kulileta jambo hilo kubwa kuahidi kulileta bungeni.
“Huwezi ukamlazimisha mtu aamini kinyume
na imani yake, wakristo tumekaa hapa tunajadili waislamu ‘non of our business’
tuwaache wajadili mambo yao
hii ni ‘non sense’ na ndio maana suala la imani limevuka mipaka ya vyama.
“Mnataka
kutuvurugia nchi hii kwa kutafuta kura, tumeishi pamoja kwa miaka 50 sasa,
mnataka kutupelekea wapi, juzi Rais Kikwete alisema Serikali haitaanzisha
Mahakama ya Kadhi bali itaanzishwa na waislamu wenyewe,” alisema.
Mbunge
wa Mwanakwerekwe Haji Juma Sereweji (CCM), alitaka muswada huo uwasilishwe
bungeni na kwamba wabunge watapewa nafasi ya kupendekeza marekebisho yao.
“Sioni
sababu ya kwanini muswada usipelekwe bungeni, yule ambaye anaona haufai siku
hiyo wasije bungeni au watoke nje.
“Karuume
alikubali Mahakama ya Kadhi ndio maana Zanzibar
ipo, Nyerere alishauri kuanzishwa kwa Bakwata ili waislamu wawe na sehemu yao ya kusemea, sheria hii iletwe ili waislamu wasimamie
mambo yao,”
alisema.
Mbunge
wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) alitaka muswada uwasilishwe bungeni
na kwamba wabunge watapata fursa ya kufanya marekebisho.
“Mimi
binafsi sikubaliani na Mufti kuchagua makadhi kwa sababu cheo cha kadhi ni
kikubwa kuliko cha Mufti, tusisukumwe na makundi ya kisiasa na imani
zisizokubalika na Mungu.
Mangungu
aliwataka wabunge wasiwasemee wananchi kwa kuwa wao kama
hawautaki muswada huo haina maana kwamba Watanzania wote hawautaki.
Hata
hivyo mbunge huyo alirushiana vijembe na Mbunge wa Viti Maalum,Esther Bulaya
baada kumzonga pale alipowaita wabunge kwamba ni wanafiki kutokana na
michango yao
waliyokuwa wanaitoa.
Mbunge
wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CUF) alisema ni wakati muafaka muswada huo
uwasilishwe bungeni na kwamba wanachotaka waislamu ni kutambulika kwa hukumu
zinazotolewa na Mahakama ya Kadhi.
“Sasa
hawa wenzetu pilipili wasoila inawawashia nini, milishaambiwa mahakama hii
haitajihusisha na masuala ya jinai isipokuwa masuala ya ndoa, mirathi, talaka
na wakfu,’ alisema.
Mbunge
wa Igunga, Dk Dalay Kafumu (CCM) aliitaka Serikali kutoa elimu kwa
viongozi wa dini wakiwemo maaskofu kuhusu mahakama hiyo kwa kuwa bado hawana
uelewa.
Awali
akifungua semina hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema baada ya Serikali
kuwashirikisha wadau mbalimbali ikaamua kuuleta muswada huo ambao utatambu
Mahakama ya Kadhi.
Alisema
mahakama hizo zilianzishwa tangu mwaka 212 na kwamba zipo kesi
zinashughulikiwa huko na kwamba hakuna mkono wa Serikali katika kugharamia
mahakama hizo.
“Wenzetu
wanataka mahakama zetu zitambue hukumu zinazotolewa na Mahakama za Kadhi, na
mahakama hizi hazishighulikii masuala ya jinai isipokuwa masauala ya Ndoa,
miradhi, talaka na wakfu,” alisema.
Alisema
mabadiliko hayo hayavunji Katiba kama ambavyo
watu wengi walikuwa na hofu hiyo na kwamba Katiba inayopendekezwa hakuna
kipingele kinachozungumzia mahakama hiyo.
Mtoa
mada katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria alikuwa ni
Jaji Robert Makaramba
Kwa upande wa Harubu Shamsi, alisema
licha ya kuhitajika kwa mahakama hiyo, siyo sahihi kwani wameshindwa
kusimamia haki za msingi ikiwamo kuuza aridhi.
“Mkiwapa na hii watavunja ndoa za watu
ili waowe wake zao” alisema.
Alisema muswada haukidhi mahitaji ya
waisilamu na kuwa ni sawa danganya toto.
Mbunge wa Nkasi Kasikazini, Alli Kesy,
alisema hakubaliani na suala la mahakama ya kadhi kwani siyo kati ya nguzo kuu
za waisilamu.
Alisema baadhi ya wabunge wanaotaka
mahakama hiyo hawaheshimu nguzo muhimu ya dini hiyo ambayo ni kuswali na badala
yake hutumia muda mrefu kunywa pombe.
Naye
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alisema serikali inasema haita
hudumia mahakama hiyo lakini kuna nyaraka za kamati ndoyo ya serikali ambayo
pamoja na mambo mengine inaonyesha kwamba Serikali itasaidia uanzishwaji wa
mahakama hiyo kwenye hatua za awali.
Alisema
nyaraka hiyo ambayo iliwasilishwa pia kwenye kamati ya Bunge ya Katiba na
Sheria, inasema sehemu ya vitu vitakavyotolewa na serikali ni pamoja na mafunzo
na majengo.
Pinda
Akifunga warsha hiyo, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, alisema baada ya kusikiliza wabunge hao alitambua kuwa ndani ya
waisilamu wenyewe hakuna maelewano juu ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Alisema kuwa, baada ya kuona hali hiyo
serikali itaona kama jukumu lake
kurekebisha hiyo
hali ama laa.
Alisema pia ameona kuwa, baadhi ya watu
wanafikiri kwamba sheria iliyotungwa na serikali ni kilemba cha ukoka kwa
waisilamu.
“Kwamba baadhi ya waisilamu
hatujawafikisha pale wanapotaka, lakini hiki ni matokeo ya mjadala ulioibuka
ndani ya bunge la katiba,” alisema.
Alisema wasiwasi mwingine ni ule wa kuona
kwamba, yawezekana kuna kilichojificha nyuma ya muswada huo na kwamba baada ya
kupitishwa kwa sheria hiyo mambo mengine yaingizwe kimiakimia.








Comments
Post a Comment