WASHUKIWA WA DAWA ZA KULEVYA KUNYONGWA
Mzozo wa kidiplomasia watokota Indonesia
Mzozo wa kidiplomasia watokota Indonesia
Mzozo wa kidiplomasia unaendelea
kutokota kati ya Indonesia na jamii ya kimataifa kuhusiana na uamuzi wa
serikali ya Indonesia wa kutekeleza adhabu ya kifo kwa washukiwa kadhaa
wa ulanguzi wa dawa za kulevya nchini humo.
Indonesia inajiandaa
kutekeleza uamuzi huo dhidi ya raia kadhaa wa Australia, Brazil,
ufaransa na Nigeria ambao walipatikana na hatia ya kusafirisha dawa za
kulevya nchini humo kinyume cha sheria. Wanyama wa chebusiri anamaelezo zaidi.
Rais wa indonesia Joko Widodo, amesema mpango wao wa kuwanyonga wafungwa kumi na mmoja wa ulanguzi wa mihadarati, utaendelea kama ulivyopangwa.
Akiongea na waandishi wa habari rais Widodo amesema kuwa hakuna anayepaswa kuingilia kati masuala ya ndani ya taifa hilo.
Mapema hii leo mahakama nchini humo ilipuuzilia mbali juhudi za raia wawili wa australia wanaokabiliwa na hukumu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya, za kupinga uamuzi wa rais wa kukataa
maombi yao ya kusamehewa.
Myuran Sukumaran na Andrew Chan, wanaoaminika kuwa viongozi wa genge la ulanguzi wa mihadarati, walikamatwa wakijaribu kusafirisha herion nchin ya nchi hiyo mwaka wa 2005 na walihukumiwa kifo mwaka wa 2006.
Rais wa nchi hiyo, Joko Widodo. alikataa rufaa yao ya kupinga uamuzi wake kutowasamehea, hatua ambayo ndiyo ya mwisho kwa mfungwa yeyote, kuepukana kunyonywa kwa kupigwa risasi.
Rais widodo amekuwa mwanasiasa maarufu ambaye anaunga mkono kunyongwa kwa walanguzi wote na amekariri kuwa mataifa ya magaribi ni sharti kujiepusha na kuingilia kati masuala ya ndani ya Indonesia.
Indonesia inakabiliwa na shinikizo chungu nzima kutoka kw a jamii ya kimataifa sio tu kutoka australia lakini pia mataifa ya Brazil na Ufaransa, ambayo raia wao pia wanakabiliwa na adhabu hiyo hiyo ya kifo.
Akikataa maombi ya washukiwa hao jaji amesema kuwa washukiwa hao sasa wana siku kumi na nne kuwasilisha rufaa zao na tayari mawakili wao wanajiandaa kufanya hivyo.
Lakini Rais widodo amekariri kuwa utawala wa Jakarta utatekeleza hukumu hiyo ya kifo kwa raia hao wa Australia na wa mataifa mengine licha ya shinikizo hizo za jamii ya kimataifa.
Waziri mkuu wa Australia Tonny abbott, mara kwa mara ameto wito kwa serikali ya indonesia kuwaepushia washukiwa hao adhabu hiyo na badala yake kuwarejesha australia,
na wakati huo huo kukumbusha widodo kuwa serikali ya Australia iliipa misaada nyingi mwaka wa 2004 kukabiliana na janga la tsunami.
Lakini makamu wa Rais wa Indonesia Jusuf Kalla amesema fedha walizopokea zitarejeshwa ikiwa serikali ya australia haitasema kuwa ilikuwa misaada ya kibinadam.
Matamshi hayo yamezua hasira miongoni mwa makundi kadhaa ya kijamii nchini Indonesia ambao wameanza kukusanya pesa ili kurudisha msaada huo walioupokea kutoka Australia.
Comments
Post a Comment