Posts

Showing posts from February, 2015

MCHINJAJI MWOGA HATIAME AJULIKANA. KWANINI UFICHE USO KAMA WEWE NI JASIRI

Image
Mchinjaji mateka wa IS 'Jihadi John' ni raia wa Uingereza Mwanamgambo anayejulikana kwa jina la utani 'Jihadi John' wa kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la dola la kiislamu IS, ambaye amekuwa akionekana katika video akiwachinja mateka ametambuliwa kama Mohammed Emwazi  Nenda kwenye makala   Matukio ya Kisiasa Mchinjaji mateka wa IS 'Jihadi John' ni raia wa Uingereza Mwanamgambo anayejulikana kwa jina la utani 'Jihadi John' wa kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la dola la kiislamu IS, ambaye amekuwa akionekana katika video akiwachinja mateka ametambuliwa kama Mohammed Emwazi Mohammed Emwazi ni raia wa Uingereza, mtaalamu wa masuala ya programu za kompyuta anayetokea familia inayojiweza iliyoko mjini London na alikuwa akifahamika na maafisa wa usalama nchini Uingereza hata kabla ya kuelekea Syria. Mwanamgambo huyo ambaye huonekana katika video za kundi la IS akiwa amevalia nguo nyeusi na kuufunika u

TIGO YADHAMINI WANARIADHA KILI MARATHONI

Image
 Mwanariadha Mary Naali akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha na kushoto ni Meta Petro Mjumbe toka riadha Tanzania pia ni kocha wa wanariadha hao. Mwanariadha Alphonce Felix  akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.  Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza udh

MCHUNGAJI DK.LWAKATARE,AWAANDALIA CHAKULA CHA JIONI WANANDOA KANISANI KWAKE

Image
 Mchungaji Mkuu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Dk. Getrude Lwakatare, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuandaa chakula cha wanandoa kitakachofanyika March 6 mwaka huu. lego lake ni kuwaweka karibu wanandoa kwa siku hiyo pamoja na kupatiwa mafunzo ya kuimalisha ndoa zao. mchungaji huyo alisema kwamba siku hizi baadhi ya ndoa zinavunjika hata zikiwa na miezi sita tu zamani ilikuwa vigumu kuona kitu kama hicho, wengine wanaolewa au kuo ni kudai kuondoa mkosi na badai kuachana  kitu ambacho ni makosa, mmeapa mbele ya madhabahu ya mwenyezi mungu na mashahidi ni ndugu zenu na kuapa kwamba  ni kifo tu kitakachowatengeneisha sasa wanaachana mapema kiasi hicho. Amewaomba wanandoa kujitokekza kwa wingi kiingilio kitkuwa Sh 30000 kwqa wawili na Sh 15,000 kwa mmoja cha muhimu ni kuja kusikiliza mafundisho hayo ili tanzania iondokane na kuwa na watoto wengi wa mitaani ambao wanasababishwa wakati mwingine kuachana kwa wazazi baada ya hapo watoto wanaona kulele na mam

GUNINITA AMSHITAKI MAKONDA

Image
Kada na Kiongozi wa siku nyingi wa Chamam cha Mapinduzi (CCM), John John Guninitam, akiwa ameambatana na wakili wake wakiingia katika chumba cha mikutano katika ofisi za Idara ya Habari Maelezo leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu yeye na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida Mghana Msindai kumshitaki aliyekuwa mhamasishaji wa Chipukizi wa umoja wa chama hicho ambaye hivi sasa ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kwa kile alichodai kwamba kabla ya kuteuliwa na Rais aliwatukana bila sababu za msingi, istoshe alisema kwamba hivi sasa ccm kimekuwa kimbilio la wahuni wanaodiliki kutukana wakubwa hata waliowatangulia hata kwenye kazi wanaogawiwa sasa, kimekuwa chama cha wasaka tonge ambao hawajawahi hata kuchaguliwa wao ni kuteuliwa tu. Pia amewashutumu washauli wa rais akaisema kwamba hawamshauli vizuri kwani angekuwa yeye angetengua uteuzi wa Makonda, CCM na Serikali ni kama Jeshini, wanaheshimiana kwa vyeo na usinia, haiwezekani itokee siku koplo amke asubuhi

WASHUKIWA WA DAWA ZA KULEVYA KUNYONGWA

Image
Rais Widodo ameyapuuza mataifa ya Australia Brazil na Ufaransa  Mzozo wa kidiplomasia watokota Indonesia Mzozo wa kidiplomasia watokota Indonesia Mzozo wa kidiplomasia unaendelea kutokota kati ya Indonesia na jamii ya kimataifa kuhusiana na uamuzi wa serikali ya Indonesia wa kutekeleza adhabu ya kifo kwa washukiwa kadhaa wa ulanguzi wa dawa za kulevya nchini humo. Indonesia inajiandaa kutekeleza uamuzi huo dhidi ya raia kadhaa wa Australia, Brazil, ufaransa na Nigeria ambao walipatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya nchini humo kinyume cha sheria. Wanyama wa chebusiri ana maelezo zaidi. Rais wa indonesia Joko Widodo, amesema mpango wao wa kuwanyonga wafungwa kumi na mmoja wa ulanguzi wa mihadarati, utaendelea kama ulivyopangwa. Akiongea na waandishi wa habari rais Widodo amesema kuwa hakuna anayepaswa kuingilia kati masuala ya ndani ya taifa hilo. Mapema hii leo mahakama nchini humo ilipuuzilia mbali juhudi za raia wawili wa au

IS Yawateka wakristu 90 Syria

Image
  IS Yawateka wakristu 90 Syria 24 Februari 2015 Jamii ya wakristu nchini Syria Kundi la Islamic State limewateka nyara watu 90 wa jamii ya wakristo kutoka katika kijiji kimoja kazkazini mwa Syria. Kisa hicho cha utekaji nyara kilifanyika mapema leo alfajiri, baada ya wanamgambo hao kuchukua udhibiti wa vijiji kadhaa kutoka kwa walinda usalama wa kabila la Wakurdi. Wanamgambo hao walivamia kituo cha Radio na kuchukua udhibiti wa mawasiliano na kuanza kutangaza Radioni, kuwa wamewateka nyara wale wanaojiita watetezi wa Dini. Kwa muda mrefu kundi la wakristo wachache walioko Nchini humo limekuwa likishirikiana na wapiganaji wa kabila la Wakurdi kukabiliana na wanamgambo wa IS.     Jamii ya wakristu nchini Syria Awali Kundi la I S limekuwa likiharibu makanisa ya wak

MAHAKAMA KUU NCHINI KENYA YALIGOMEA BUNGE NA RAIS

Image
Serikali ya Kenya Kenya imepata pigo jingine baada ya mahakama kuu kuharamisha baadhi ya vipengee katika sheria ya usalama iliyolega kukabiliana na ugaidi. Muungano wa upinzani nchini Kenya na mashirika mbalimbali yalienda mahakamani mwaka uliopita baada ya bunge kupitisha sheria hiyo. Jopo la majaji watano wa mahakama kuu wakiongozwa na Jaji Isaac Lenaola waliharamisha vipengee 10 kikiwemo kile kinachohusu uhuru wa vyomo vya habari na haki ya washukiwa wanapofikishwa mahakamani. Uamuzi huo ulichukua takriban saa tano na majaji wakaamua kuwa baadhi ya vipengele havikuaambatana na katiba. Katika uamuzi wao walikubali kuwa Kenya imekumbwa na visa vingi vya ugaidi katika miaka mitatu iliyopita na inastahili kuwa na mbinu za kuisaidia kukabilana na tatizo hilo… hata hivyo majaji walisema kuwa haki za washukiwa zinatakiwa kuzingatiwa. Mengine yaliyoharamishwa yanajumuisha kuwalazimisha wanahabari kuchapisha baadhi ya picha ya ruhusa ya polisi, kuwazuilia washukiwa bil