DACICO YAWEKA MPIRA KWAPANI BONANZA LA NACTE
Wachezaji wa Timu ya Chuo cha Elimu ya watu wazima, wakipeana mawaidha muda mfupi baada ya kutoka mapumziko kwenye mpambano dhidi yao na Chuo cha St. Joseph kuwania nafasi ya Upendeleo(Bestlooser) mchezo uliochezwa baadab ya timu zote kupoteza kwenye michezo yake ya awali
DACICO YAWEKA MPIRA KWAPANI BONANZA LA NACTE.
Yaomba Suruhu kwa NIT, ST.Joseph yapita kwa nafasi ya dhahabu(Best looser).
Na: Mwandishi Wetu.
1 -National Institute of Transport - Vs Institute of Adult Education -0
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT mwishoni mwa wiki kimefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye michezo ya Sehemu ya pili ya (Season two) iliyofanyika siku ya jumamosi ya tarehe 29 katika Viwanja vya Ustawi wa Jamii Kijitonyama baada ya wapinzani wao chuo cha Dar es Salaam City kushindwa kutokea Uwanjani kucheza Fainali kwa lengo la kupata mshindi wa kwanza na wa pili.
NIT walifanikiwa kuifunga timu ya Institute of Adult Education kwa bao 1-0 mfungaji akiwa ni Abross Kabona dakika 23 kipindi cha kwanza katika mchezo uliochezeshwa na mwamuzi chota
Kijana Chipukizi asiyekuwa na Uzalendo Nadim Muhammed.
Katika mtanange huo wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Watu wazima Institute of Adult Education walitaka ufanyike ukaguzi kwa wachezaji wote kama ni wanafunzi halali wa vyuo vyao.
Nafasi ya Pili kwa upande wa Soka ilichukuliwa na Chuo cha Dar es Salaam City College (DACICO) waliofanikiwa kuwafunga S.t Joseph College(University) kwa bao 1-0 mfungaji akiwa ni
Slyvester Mpoto dakika ya 56 kipindi cha pili baada ya kupokea pasi nzuri ya Mohamed Mapanki katika hatua ya nusu fainali iliyokuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote kuonyesha kiwango cha hali ya juu.
St. Joseph ambao hata hivyo imefanikiwa kupenyeza hatua ya 32 iliweza kushinda baada ya kuitumia vyema nafasi waliyopewa (Best looser) dhidi ya Institute of Adult Education inatakiwa kujipongeza kutokana na jitiada kubwa ilizoonyesha katika kuwania nafasi hiyo ya kushiriki michuano hiyo mipya ya NACTE TANZANIA.
Chuo cha elimu ya watu wazima walijikuta wakiambulia nafasi ya nne baada ya kushindwa kuhimili mikiki ya vijana wa NIT, DACICO na St. Joseph College ambao wamepita kwa kushinda mchezo wa zawadi waliopewa (Bestlooser).
aidha mchezo uliowasisimua mashabiki ulikuwa ni kati ya timu za DACICO na St. Joseph College (University) ambapo wachezaji walionyesha kukamiana kutokana na kuwa majirani maeneo ya Kibamba Chama na Kibamba Makondeko.
Akizungumzia hatua hiyo ya pili mwandaaji wa Bonanza hilo la kihistoria , Mpalule Shaaban alisema kuwa ushindani ni mkubwa kwa sasa kutokana na timu zote kutambua umuhimu wa ushindi wakati wa michezo yao ya awali kutafuta kuingia hatua hiyo ya timu 32 zinazotafutwa kwa ajili ya kushiriki ligi ya NACTE TANZANIA kwa mkoa wa Dar es Salaam ambao unatakiwa kutoa timu sita zitakazowakilisha mkoa kwenye ligi ya timu 16 za tanzania kutoka kanda tano.
Kwa Uapande wa michezo ya mingine Timu ya Chuo cha Elimu ya watu wazima walifanikiwa kuwa washindi wa kwanza katika mchezo wa Kikapu baada ya kuwafunga St. Joseph kwenye hatua ya Fainali.
katika mchezo wa Netbali timu ya chuo cha elimu ya watu wazima kiliibuka kidedea baada ya kuwanyoosha wenzao wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa jumla ya magoli 17-14.
Mpalule alisema pia kwamba mwitikio ni mkubwa kwa wanafunzi ambao michezo hii walikuwa wakiiwaza miaka mingi na hivyo fulsa hii wanaitumia vizuri na kwamba mchezo unaoshangaza ni Voleyball ambao vyuo mbali mbali vimejitokeza kuleta timu wawakilishi katika michezo yao" mchezo kama Voleyball mimi sikutarajia kama ungekuwa na idadi kubwa namna hii ya washabiki, na hata hivyo nimegundua kwamba mchezo huu unapendwa sana kwenye vyuo, na endapo ukipewa kipaumbele unaweza kuwa mchezo wa ushindani mkubwa kwenye vyuo vya NACTE"alisema Mpalule.
Kundi hilo sehemu ya pili lilikuwa na vyuo vya Institute of Social Work (ISW), St. Joseph College (University), Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ), Lugalo Military Medical School, National Institute of Transport,na Institute of Adult Education vyote vya mkoa wa Dar es salaam.
Michezo ya wiki ijayo kwa upande wa Soka ni itakayochzwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari kibaha-Njuweni, tarehe 6/12/2014- utavikutanisha vyuo vya Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management, Kibaha COTC - Kibaha, KAM College of Health Sciences, Eden Hill Community College - Kibaha, Nyerere Institute of Technology and Innovation - Kibaha, Institute of Procurement and Supply (IPS) - Dar es salaam, Mount Ukombozi Health Laboratory Assistants School - DSM, Zoom Polytechnic College - DSM, na Times FM 100.5 ambao watacheza na Kombaini ya Vyuo vyote katika sehemu hiyo ya tatu mchezo utakaoanza mapema saa 10 na nusu jioni mara baada ya kumalizika fainali za mchujo wa Bonanza la NACTE kanda ya Mashariki.
Michezo hiyo ya Vyuo vya Elimu ya Kati Tanzania inasimamiwa na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd kwa kushirikiana na kituo bora cha Matangazo TIMES FM 100.5.
ambapo ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha, na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Wadhamini walionyesha nia mpaka sasa ni VODACOM, Caca –Cola, NMB, Mlonge By Makai, 100.5 Times Fm.
Comments
Post a Comment