Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza Rais mpya wa nchi hiyo
Jenerali Honore Traore Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza Rais mpya wa nchi hiyo
Mkuu
wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa
rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza
kujiuzulu.
Jenerali Traore ameshinikizwa na waandamanaji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa Bwana Compaore.
Compaore amesema kuwa amekubali kuondoka madarakani ili kutii matakwa
ya waandamanaji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada
ya kutawala kwa miaka 27.
Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90. Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanaji kuwa bwana Compaore hayuko tena madarakani huko Ouagadougou.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea mabarabarani kwa siku ya pili
Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari. Siku
ya Alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais
za kuongeza muda wa uongozi wake baada ya kutawala kwa miaka 27
waliteketeza jengo la bunge na kuvamia kituo cha televisheni ya taifa.
Bwana
Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo
ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa
angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi.
TAARIFA KWA UMMA UTEUZI WA AWALI WA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WATAKAOSHIRIKI KATIKA ZOEZI LA KURA ZA MAONI KWA NAFASI ZA UBUNGE NA UJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI Kamati Kuu ya Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, katika kikao chake kilichofanyika tarehe 28 Julai, 2025 Jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine, imepitia na kujadili majina ya wanachama wake walioomba kupendekezwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM. Kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 105 (7)(f) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Julai 2025, Kamati Kuu imefanya uteuzi wa majina ya wanachama wafuatao, ambao watapigiwa kura za maoni kwa mujibu wa Kanuni na Kalenda za Chama Cha Mapinduzi. 1) MKOA WA ARUSHA (i) Jimbo la Arusha Mjini (1) Ndugu Ally Said BABU (2) Ndugu Hussein Omarhajji GONGA (3) Ndugu Aminatha Salash TOURE (4) Ndugu Mustapha Said NASSORO (5) Ndugu Paul Christian MAKONDA (6) Ndugu Lwembo Mkwavi MGHWENO (7) Ndugu Jasper Augustino KISHUMBUA (ii) Jimbo la A...
Kangaroo hupatikana Australia pekee Miamba Bahari ya Australia ni mikubwa kuliko yote Duniani na kivutio kwa watalii Ramani ya Australia Robo tatu ya Waustralia wanaishi katika majiji makubwa na maeneo ya pwani. Fukwe pia ni sehemu za utambulisho wa Australia SAYARI tuishimo yaani dunia ina mabara saba, ambayo tukianzia kwa mtiririko wa bara kubwa hadi dogo ni Asia, Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Ulaya, Antarctica na Australia Mbali ya mabara hayo ambayo Antartica ni pekee lisilokaliwa na watu kutokana na kufunikwa na barafu kwa asilimia 89, dunia ina nchi huru kati ya 180 na 195 huku ikiwa na mamia kwa maelfu ya visiwa. Katika makundi hayo matatu, Australia ni pekee duniani iliyobeba sifa zote tatu yaani bara, nchi na kisiwa, kwani nyingi zimeishia kuwa na sifa moja au mbili yaani nchi na au kisiwa. Australia ni bara dogo kuliko yote duniani, lakini pia kisiwa kikubwa kuliko vyote katika sayari hii. Mbali ya sifa hiz...
Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Sophia Kibaba, akimkabidhi fomu ya kuomba kugombea ubunge Kelvin Wilson ambaye anagombea jimbo la Mtumba. Amesema iwapo atateuliwa na chama chake atawatumikia wananchi wa jimbo lake bila kuchoka.
Comments
Post a Comment