BEN KIKO AFARIKI DUNIA
ALIEKUWA MTANGAZAJI NA MWANDISHI WA HABARI RADIO TANZANIA SASA TBC BEN KIKO AFARIKI DUNIA
Katibu wa Rais maswala ya Habari, Issa Michuzi kulia akiwa na mtangazaji wa siku nyingi, Beni Kiko wakifurahia jambo wakati wa uhai wake katika tuzo za mwandishi bora |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenela Mukangara kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko.
Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akiendelea na matibabu ya figo baada ya kuhamishiwa hapo akitokea Hospitali ya Jeshi ya Milambo Mkoani Tabora.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mwanahabari na Mtangazaji huyu Mahiri ambaye ametoa mchango mkubwa wa kihabari kwa Taifa letu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba wa Ben Hamis Kikoromo.
“Namkumbuka Marehemu Ben Kiko, enzi za uhai wake, kama Mtangazaji aliyekuwa na mvuto mkubwa kwa wasikilizaji wake kutokana na namna yake ya kipekee ya kuripoti matukio hususan katika kipindi kilichojizolea umaarufu mkubwa wakati huo cha MAJIRA kilichokuwa kikirushwa hewani na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD)”.
Wakati wa vita dhidi ya Nduli Idi Amin wa Uganda mwaka 1978, Ben Hamis Kikoromo alifanya kazi kubwa kwa Taifa kwani aliweza kuripoti matukio mbalimbali kutoka katika uwanja wenyewe wa vita, na hivyo kuliwezesha Taifa na wananchi kwa ujumla kuhabarika vilivyo na matukio yaliyokuwa yakiendelea.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, pokea salamu zangu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza mmoja wa Waandishi na Watangazaji Mahiri katika Tasnia ya Habari hapa nchini.
Vilevile kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo kwa kupoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti wa Familia. Nawaomba Wanafamilia wote, ndugu na Jamaa wa Marehemu wawe wavumilivu na wenye subira wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao huku wakitambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.
Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika muda wote wa maombolezo, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Ben Hamis Kikoromo, Amina.
Aidha Rais Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kwa Wanahabari kote nchini ambao kwa hakika msiba wa Ben Kiko utakuwa umewagusa kwa karibu.
Hata hivyo amesema kuondoka kwa Ben Kiko kusiwe chanzo cha wao kukata tamaa, bali kifo chake hakina budi kuwa chachu katika kujituma zaidi, na wawe tayari kuiga yote mazuri aliyoyafanya Marehemu enzi za uhai wake hapa duniani hususan katika Taaluma ya Uandishi wa Habari.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Oktoba, 2014.
Viongozi wa Msondo wamtembelea Rais Kikwete Ikulu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro). Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro)
AJALI MBAYA YA ARUSHA
Simanzi
zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali
iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya
mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema
ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani
-Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka
Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria)
iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na
lori hilo. Habari kamili zitawajia punde.
BREKING NEWZZZZZZZZ WATU 9 WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO LE JIONI
Watu 9 wamefariki dunia na wengine 2 wamejeruhiwa baada ya basi dogo la
abiria Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mafuta katika eneo
la makumira wilayani Arumeru kwa mujibu wa kamanda wa polisi Arusha
libaratus Sabas ametibitisha na kusema imetokea mida ya saa kumi leo
lori hilo namba ya usajili T582 ACR likitokea mkoani kilimanjari na
kwenda Arusha majeruhi wamepelekwa katika hospitali iliyokaribu ya
Tengeru na waliofariki miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya
Mount Meru RADIO ONE STEREIO TUTAWALETEA HABARI ZAIDI KATIKA MZUKA WA
FUNGO
BONDIA FADHILI MAJIHA AONESHA MAAJABU KWA KUPIGWA KWA POINT THAILAND MCHEZO WA RAUNDI 12
Bondia Fadhili Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa Thailand wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA nambari moja kwa ubora nchini Tanzania katika uzito wa bantamweight
Fadhili Majiha 'Stoper' mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa na kibarua
kizito kutoka kwa Mthailand aliyemenyana nae nyumbani kwao Thailand na
kupigwa kwa point
akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa
kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi
hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana
nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa
upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi
bondia huyo ambaye anatamba sana hapa
nchini kuwa akuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na
bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa
onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa
mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe
nimerudi nyumbani nipo fit sina ata
kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza
ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote
mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali
yangu
nae Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne
Comments
Post a Comment