UN WASHIRIKI BURUDANI TEMEKE
KITUO CHA HABARI CHA UMOJA WA MATAIFA WASHIRIKI ALHAMISI YA BURUDANI Afisa habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akitoa mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development) iliyotolewa kwa Mtandao wa vijana wa Temeke. Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jana iliandaa Alhamisi ya Burudani kwa ajili ya kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Kwa kila Alhamis ya mwisho wa mwezi Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huandaa burudani kwa makundi mbalimbali na kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Alhamisi ya mwezi wa kumi kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kilitembelea Mtandao wa Vijana wa temeke na kujadili mambo makuu ya malengo ya Milenia pamoja na kuangalia ni jinsi gani vijana wanashiriki katika shughuri za kimaendeleo katika jamii zao Mkutubi - Kituo cha Habari cha U