Posts

KAWISHE BILIONEA MPYA WA TANZANITE NCHINI

Image
Na Mwandishi wetu, Mirerani  MCHIMBAJI wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Anselim Kawishe ametangazwa kuwa bilionea mpya wa madini ya Tanzanite. Kawishe amekuwa bilionea mpya baada ya kupata vipande viwili vya madini hayo vya thamani ya sh2.2 bilioni. Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Nduguru amemtangaza bilionea huyo leo jumamosi Agosti 27 mji mdogo wa Mirerani.  Nduguru amemtangaza bilionea huyo mpya katika hafla ya ununuzi wa madini ya Tanzanite kuwa ni Anselim Kawishe. Amesema Kawishe amepata vipande viwili vya madini ya Tanzanite vyenye uzito wa kilogramu 3.74 na kilogramu 1.48. “Kati ya madini hayo mawili, yenye uzito wa kilogramu 1.48 ina thamani ya sh713.8 milioni na ya uzito wa kilogramu 3.74 yenye thamani ya sh1.5 bilioni jumla ni sh2.245 bilioni, amesema Nduguru. Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka amempongeza Kawishe kwa kufanikiwa kupata madini hayo. “Hata mimi nisipokuwa bilionea...

NAIBU SPIKA AFUNGUA MAFUNZO YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA KAMATI ZA USIMAMIZI BUNGE (PAC, LAAC NA PIC) NA KAMATI YA BAJETI

Image
  Naibu Spika wa Bunge,  Mussa Azzan Zungu akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU Institute of Public Accountability, Ludovick Utouh kabla ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika  Agosti 7,2022 Jijini Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akifungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika  Agosti 27,2022 Jijini Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU  Institute of Public Accountability, Ndg. Ludovick Utouh  akitoa neno la ukaribisho wakati   wa   mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika  Agosti 27,2022 Jijini Dodoma. Baadhi ya Wajumbe wa kamati za usimamizi wa Bunge (PAC, LAAC na PAC) pamoja na kamati ya Bajeti wakishir...

MKUTANO WA WADAU WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAKUTANA JIJINI DODOMA

Image
Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Raphael Chibunda, akitoa mada katika mkutano wa Wadau wa kupokea Maoni Kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi cha Uratibu wa Ubunifu nchini, mkutano huo wa siku mbili unafanyika jijini Dodoma Wadau wa mkutano huo wakisikiliza kwa umakini watoa mada Wadau wakiwa katika mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Stanlaus Nyongo, akizungumza katika hafla hiyo  

MKUU WA MKOA WA DODOMA ROSEMARY SITAKI SENYAMULE AWATAKIA SAFARI NJEMA AKINAMAMA WAKIANGLIKANA WANAOENDA KUTALII NGORONGORO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, RoseMary Staki, amewapongeza wanawake wa dhehebu la Kianglikana  kwa kitendo chao cha kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza utalii nchini, Mkuu huyo aliyasema hayo wakati akiagana na waumini hao wa kike 100 wanaoenda Ngorongoro kutalii  utalii wa ndani Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Centraly Tanganyika Kanisa la Anglikan, Dickson Chilongani, akizungumza katika hafla hiyo ya kuagwa wake wa wachungaji wa kanisa hilo wapatao 100 wanaoenda kutalii Ngorongoro kwa awamu ya kwanza, alisema kutakuwa na awamu tatu yawanawake na wanaume ambapo itachukuwa waumini 600 hadi kukamilika kwenda kutalii utalii wa ndani. Askofu alisema  yawapasa wananchi wa Tanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kitendo chake hiki alichokifanya sasa dunia yote inaiangazia Tanzania. Waumini wengi wanyama waliopo mbugani wanawaona katika picha tangu kuzaliwa kwao hawajawahi kuwaona kwa macho sasa ni muda sasa wa kujionea maajabu yaliyopo nchini, aliwaomba Chilo...

TEMBOCARD YAJA NA KAMPENI YA WATEJA WAKE WANNE KUPELEKWA NCHINI QATAR KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA

Image
      Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (watatu kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Kadi, Farid Seif (wapili kulia), Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Badru Idd (wapili kulia) na Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa Benki hiyo, Erica Mwaipopo, wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya ...