Posts

Kigogo Escrow aruhusiwa kwenda kutibiwa

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeamuru Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Seth, aende kutibiwa kutokana na matatizo ya kiafya yanayomsumbua. Amri hiyo imekuja baada ya Seth kusimama mbele ya mahakama hiyo jana wakati shauri lake likiendelea na kudai kuwa ana matatizo ya kiafya na kuomba apewe kibali ili aweze kutibiwa. Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, aliitaka Serikali kumpeleka hospitali ili aweze kupatiwa matibabu kutokana na maradhi hayo. Hakimu Shahidi aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 3, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa tena. Julai 14, mwaka huu, upande wa utetezi, ukiongozwa na Wakili Alex Balomi, uliieleza mahakama hiyo kuwa mteja wao anahitaji kupewa mtaalamu wa afya kwa sababu ana uvimbe tumboni kama puto, pia anakosa usingizi. Awali, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka sita, yakiwamo kula njama, uhujumu uchumi, kujihusisha n...

ujenzi wa barabara ya kidato hadi ifakara yatiwa saini

Image
Wizara ya Fedha na Mipango imetiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara mkoani Morogoro, yenye urefu wa kilometa 67 kwa kiwango cha lami utakaojengwa kwa shilingi bilioni 101, kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza. Mkataba huo umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Bw. Dan Yzhak Shahn, Bw. Benjamin Arbit ambaye ni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds. Kiasi hicho cha fedha ni sawa na Euro milioni 40.4 ambapo  Euro milioni  29.6 zimetolewa kwa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Shirika la Misaada la Uingereza-UK-AID, huku  kiasi kinachobaki cha Euro milioni 10.8 kikitolewa na Shirika la Misaada la watu wa Marekani- USAID. Akizungumza mara baada ya kutiwa saini kwa kandarasi hiyo, Bi. Amina Khamis Shaaban, amesema ujenzi wa barabara hiyo utakaohusisha pia ujenzi wa daraja ka...