Papa Francis aanguka akisoma misa CZESTOSHOWA: Poland
Papa Francis aanguka akisoma misa CZESTOSHOWA: Poland Wasaidizi wake wakimwinua KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis (79) jana alianguka wakati wa ibada, kwenye madhabahu ya Jasna Gora, mjini Czestoshowa, Poland. Tukio hilo lilitokea baada ya Papa Francis kujiikwaa akiwa madhabahuni hali iliyowalazimu mapadre waliokuwa karibu naye kumsaidia kuinuka. Taarifa zinasema Papa alianguka chini karibu na ngazi za madhabahuni na aliinuliwa na mapadri waliokuwa kwenye misa hiyo. Kwa mujibu wa taarifa za utabibu, Papa Francis amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sciatica unaosababishwa na maumivu chini ya mgongo. Papa Francis , ambaye ni mzaliwa wa Argentina alionekana akitembea huku akitafakari hali iliyomfanya asigundue kuwa kulikuwa na ngazi mbele yake. B aad ya kuinuka, Papa Francis , aliendelea na taratibu za ibada kama ilivyopangwa. Alihubiri kwa muda mrefu kwenye ...