KAMATI YA BUNGE WILAYANI MASASI
Abdallah Haji, mmoja wa wajumbe wa kamati ya bunge ya Maji, Mifugo na uvuvi, akiwaongoza wajumbe wenzake kutoka katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Masasi baada ya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya hiyo. Mwenyekiti wa msafara huo, Amina Makilagi akizungumza na mmoja wa viongozi wa wilaya hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Masasi na Nachingwe (MANAWASA), Nuntufye David, akitoa maelezo ya kwa wajumbe wa kamati ya bunge walipofika ofisini kwake kufahamu hali ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa mamlaka hiyo. Mkurugenzi huyo alianza kuelezea mwanzo wa mamlaka hiyo, Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi na Nachingwea (Manawasa) ilianzishwa rasmi na Waziri mmwenye dhamana ya maji 10.5.2013 kupitia gazeti la serikali (GN No 105. kuundwa kwa mamlaka hiyo kulitokana na kuvunjwa kwa bodi na Mamlaka za Majisafi na usafi wa mazinira za masasi na Nachingwea. Bodi ya Mwanawasa kwa mujibu...