WAZIRI DKT. NYANSAHO AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YAKE LEO BUNGENI JIJINI DODOMA


 Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) iliyochambua na kutoa ushauri ulioboresha Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ninaomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Aidha, ninaomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 kwa mafungu yote matatu (Fungu 57 - Wizara, Fungu 38 - NGOME na Fungu 39 - JKT). 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kuijalia Nchi yetu amani, utulivu na mshikamano na kutuwezesha kuendelea kutumikia Taifa letu kwa uaminifu na uadilifu tukiwa wenye afya njema. 3. Mheshimiwa Spika, napenda kuungana na waheshimiwa wabunge wenzangu waliotangulia, kuwapongeza viongozi wa kitaifa kwa kuchaguliwa kwenye nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kipekee nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu na Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, 1 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuiongoza Nchi yetu katika Serikali ya Awamu ya Sita. Ninamuomba mwenyezi Mungu azidi kuwapa maarifa, busara, hekima na nguvu katika kuliongoza Taifa letu. 4. Mheshimiwa Spika, vilevile, napenda kumpongeza Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kuaminiwa na wananchi kuiongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kipindi cha muhula wa pili. Pia, nampongeza Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.), Mbunge wa Iramba Magharibi kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 5. Mheshimiwa Spika, nikupongeze wewe binafsi Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuongoza Mhimili huu muhimu katika kusimamia maslahi ya Taifa letu. Vilevile, nimpongeze Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.), kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. 6. Mheshimiwa Spika, ninawapongeza Mhe. Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini; Mhe. Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum; na Mhe. Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Viti Maalum kwa kuchaguliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, 2 ninawapongeza kwa jinsi mnavyoliongoza Bunge letu Tukufu kwa weledi na maarifa. 7. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie fursa hii, kuwapongeza waheshimiwa mawaziri na naibu mawaziri walioteuliwa kuongoza wizara mbalimbali. Aidha, nawapongeza waheshimiwa wabunge waliochaguliwa na walioteuliwa kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nawatakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yao. 8. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama katika Bunge lako Tukufu kuwasilisha Hotuba hii nikiwa Waziri wa Ulinzi na JKT, kwa namna ya kipekee namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mbunge na Waziri wa Wizara hii. Ninaomba niseme kuwa, uteuzi huu ni dhamana na heshima kubwa kwangu katika kusimamia na kuendeleza sekta ya ulinzi nchini ambayo ni kichocheo cha ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi, kijamii, maendeleo ya Taifa na wananchi kwa ujumla. Kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu, na Dira 2050 ambayo msingi wake mkuu ni utawala bora, amani, usalama na utulivu, nitatekeleza majukumu yangu kwa weledi na uadilifu, kwa kushirikiana na Bunge lako Tukufu, ili kuhakikisha kuwa maono yake katika maendeleo ya Taifa yanafikiwa. 3 9. Mheshimiwa Spika, pia, nawashukuru mawaziri wenzangu na naibu mawaziri, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jenerali Jacob John Mkunda, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, na watendaji wote wa Wizara kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu yangu. 10. Mheshimiwa Spika, nampongeza Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb.), kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, na Mhe. Paschal Inyasi Chinyele (Mb.), kuwa Makamu Mwenyekiti pamoja na waheshimiwa wabunge wote walioteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati hii. Wizara inaahidi kutoa ushirikiano kwa Kamati katika kuhakikisha mipaka, mamlaka na maslahi ya Taifa letu yanaendelea kulindwa kikamilifu. 11. Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia nafasi hii kuishukuru kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kwa maoni na ushauri wa kukabiliana na changamoto katika Sekta ya Ulinzi. Vilevile, nawashukuru kwa ushauri waliotupatia katika maandalizi ya Bajeti hii. Maoni, ushauri na maelekezo ya Kamati wakati wakichambua Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, na mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, yamesaidia kuboresha makadirio ya 4 mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, ninayowasilisha leo hapa Bungeni. 12. Mheshimiwa Spika, ninaungana na wenzangu waliotangulia kutoa salamu za pole kwako, Bunge lako Tukufu, familia, ndugu, jamaa, na watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na Mhe. Jenista Joakim Mhagama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho aliyefariki tarehe 11 Desemba, 2025, Mhe. Halima Idd Nassor aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (wafanyakazi) aliyefariki tarehe 18 Januari, 2026 na Mhe. William Vangimembe Lukuvi aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Ismani aliyefariki tarehe 25 Machi, 2026. Ninamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina. B. HALI YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI 13. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26, hali ya mipaka ya Nchi yetu yenye urefu wa jumla ya kilomita 5,923.41, ambayo inahusisha eneo la Nchi kavu, anga na eneo la maji, vyombo vyetu vya ulinzi vimeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama katika mipaka hiyo. Mipaka ya Nchi kavu ni baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, 5 Uganda, Zambia na mipaka ya Bahari ya Hindi inayojumuisha Nchi za Comoros na Shelisheli. 14. Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika hapakuwa na matukio yaliyoashiria uvunjifu wa amani baina ya Nchi yetu na Nchi tunazopakana nazo. Hata hivyo, zimekuwepo changamoto kadhaa za kiulinzi na kiusalama katika baadhi ya mipaka ikiwemo uharibifu wa alama za mipakani, ukosefu wa barabara za ulinzi kwa baadhi ya mipaka na nyingine kuharibika pamoja na migogoro ya ndani katika baadhi ya Nchi tunazopakana nazo. Taarifa kwa kila Mpaka ni kama ifuatavyo: Mpaka wa Tanzania na Burundi 15. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama wa Mpaka wa Tanzania na Burundi wenye urefu wa kilomita 468.85 ni shwari. Hakuna matukio yoyote yanayoashiria kuhatarisha usalama wa Nchi yetu yaliyotokea. Mpaka unakabiliwa na changamoto za uharibifu wa alama za Mpaka na barabara za ulinzi. Hali hii inaathiri shughuli mbalimbali za ulinzi katika Mpaka. Wizara kupitia JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama imeendelea kuimarisha ulinzi katika Mpaka huu. Mpaka wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 16. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama ya Mpaka wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 6 wenye urefu wa kilomita 554 ni shwari. Hata hivyo, Mpaka unakabiliwa na changamoto za kiusalama kutokana na mapigano yanayoendelea Mashariki mwa DRC kati ya Jeshi la Nchi hiyo na makundi yenye silaha, hususan Kundi la M23. Hali hii inaathiri usalama wa Mpaka. Kundi la M23 linashikilia miji mbalimbali ya kimkakati katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini ikiwemo Goma na Bukavu na kudhibiti Mji wa Uvira. Kushikiliwa kwa miji hiyo kunaongeza changamoto za kiusalama katika Mpaka huu. Aidha, juhudi mbalimbali za kikanda na kimataifa zimeendelea kuchukuliwa kurejesha amani ya kudumu nchini DRC. Wizara kupitia JWTZ, imeendelea kufuatilia hali hiyo kwa ukaribu ikiwemo kufanya doria mara kwa mara katika Mpaka huu. Mpaka wa Tanzania na Kenya 17. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama wa Mpaka wa Tanzania na Kenya wenye urefu wa kilomita 1,187 ni shwari. Hakuna tukio lililojitokeza linaloashiria kuhatarisha usalama katika Nchi yetu. Kazi ya kuimarisha alama za Mpaka huu inayotekelezwa na Timu ya wataalam kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya inaendelea. Mpaka wa Tanzania na Malawi 18. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama ya Mpaka wa Tanzania na Malawi wenye urefu wa kilomita 394, ni shwari. Hakuna tukio lililotokea lenye viashiria vya 7 kuhatarisha usalama wa Nchi yetu. Ushirikiano mzuri wa Jeshi letu na Jeshi la Malawi umeendelea kuimarisha usalama wa Mpaka huu. Changamoto katika Mpaka ni mgogoro wa kimpaka kati ya Nchi yetu na Nchi ya Malawi katika Ziwa Nyasa. Changamoto hii, imeendelea kufanyiwa kazi kupitia Tume Maalum ya Usuluhishi (High Level Mediation Team) chini ya Mhe. Joaquim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji. Serikali yetu kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendelea kutumia njia za kidiplomasia ili kupata ufumbuzi wa changamoto hii. Aidha, Wizara kupitia JWTZ, imeendelea kuimarisha ulinzi katika Mpaka huu na kuhakikisha wananchi wanaoishi karibu na Ziwa Nyasa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Mpaka wa Tanzania na Msumbiji 19. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama wa Mpaka wa Tanzania na Msumbiji wenye urefu wa kilomita 922.76, ni shwari. Hata hivyo, Mpaka unakabiliwa na changamoto ya uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Ansar Al - Sunna Wal Jamaah (ASWJ) / Islamic State Mozambique Province kilichopo Kaskazini mwa Msumbiji, katika Jimbo la Cabo Delgado linalopakana na Mkoa wa Mtwara kwa upande wa Tanzania. Pia, unakabiliwa na changamoto ya kuharibika kwa barabara za ulinzi ambazo zinaathiri shughuli za ulinzi wa Mpaka. Wizara kupitia JWTZ imeendelea kuimarisha ulinzi katika Mpaka huu kwa kuvijengea uwezo vikundi vyake 8 kwa zana na vifaa kuhakikisha vinatekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Vilevile, Wizara imeendelea kuwasiliana na Wizara ya Ujenzi kuona namna bora ya kuimarisha barabara hizo ili kuimarisha shughuli za ulinzi katika Mpaka huu. Mpaka wa Tanzania na Rwanda 20. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama wa Mpaka wa Tanzania na Rwanda wenye urefu wa kilomita 230 ni shwari. Katika kipindi hiki, hakuna viashiria vyovyote vilivyoripotiwa vyenye kuhatarisha usalama wa Nchi yetu. Hata hivyo, unakabiliwa na changamoto ya kuharibika kwa alama za Mpaka na barabara za ulinzi. Hali hii inaathiri shughuli za ulinzi ikiwemo doria. Juhudi za pamoja za kuimarisha alama za Mpaka huu zinaendelea kufanyika kupitia Timu ya wataalam kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda. Mpaka wa Tanzania na Uganda 21. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama katika Mpaka wa Tanzania na Uganda wenye urefu wa kilomita 397.80 ni shwari. Hakuna tukio la kuhatarisha usalama wa Nchi yetu lililotokea katika kipindi hiki. Pamoja na hali hii, Mpaka unakabiliwa na changamoto inayotokana na kuharibika kwa alama za Mpaka na uingizaji haramu wa mifugo kwa ajili ya malisho hususan katika Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera. Vilevile, unakabiliwa na changamoto ya kimpaka 9 kutokana na Serikali ya Uganda kuibua hoja kuwa Mpaka wake na Tanzania unapita nyuzi moja (1°) Kusini mwa Ikweta, badala ya marundo ya mawe yaliyopo ambayo ndiyo Mpaka sahihi kihistoria. 22. Mheshimiwa Spika, changamoto hizi zimeendelea kushughulikiwa kidiplomasia na pande zote mbili kupitia Wizara zenye dhamana ya Ardhi na Mambo ya Nje . Aidha, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kuimarisha ulinzi katika Mpaka huu. Mpaka wa Tanzania na Zambia 23. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama katika Mpaka wa Tanzania na Zambia wenye urefu wa kilomita 345, ni shwari. Hakuna tukio lililojitokeza lenye kuhatarisha usalama wa Nchi yetu katika kipindi hiki. Changamoto zinazokabili Mpaka huu ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya alama za Mpaka. Kukabiliana na changamoto hiyo, uimarishaji wa alama hizo umeendelea kufanyika kupitia Timu ya wataalam kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Zambia. Ulinzi na Usalama wa Anga la Juu 24. Mheshimiwa Spika, hali ya ulinzi na usalama wa Anga la Juu ni shwari, ingawa imekuwa isiyotabirika kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa. Aidha, Wizara ya Ulinzi na JKT kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi nyingine inaendelea kujiimarisha kwa vifaa, zana, wataalam, mafunzo na semina, lengo 10 ni kuhakikisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa salama dhidi ya matishio ya Anga la Juu. Mpaka Katika Bahari ya Hindi 25. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama katika Mpaka wa Bahari ya Hindi wenye urefu wa Nautical Miles 864.376 ni shwari. Katika Mpaka huu tumepakana na Nchi za Comoros na Shelisheli. Hakuna tukio lililoashiria kuhatarisha usalama dhidi ya Nchi yetu lililotokea katika kipindi hiki. Aidha, JWTZ imeendelea kufanya doria za mara kwa mara katika eneo la Bahari ya Hindi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ili kubaini na kuzuia uharamia, wahamiaji haramu, uvuvi haramu, usafirishaji haramu wa binadamu, usafirishaji wa dawa za kulevya na matishio ya kigaidi. C. UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA 26. Mheshimiwa Spika, Wizara iliwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yaliyotolewa katika Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha 28 kilichofanyika tarehe 20 Mei, 2025 kwenye Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama. Kamati iliridhika na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa maazimio hayo. Aidha, tarehe 10 Machi, 2026, Kamati ilipokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 na tarehe 26 Machi, 2026 ilipokea na kujadili Taarifa ya 11 Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 na Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/27. Kamati ilitoa maoni, ushauri na maelekezo yaliyolenga kuboresha usimamizi wa miradi ya maendeleo. Napenda kuishukuru Kamati na kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa yamezingatiwa na kufanyiwa kazi wakati wa kuandaa na kukamilisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 ninayowasilisha leo hapa Bungeni. D. UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI YA UCHAGUZI MKUU WA 2025 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/26 27. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara imeendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambayo miongoni mwa malengo yake ni kudumisha muungano, amani, utulivu, usalama na diplomasia ya kimataifa. Kuhakikisha lengo hili linafikiwa, Wizara ya Ulinzi na JKT imeendelea kutekeleza ipasavyo masuala yaliyoainishwa kwenye Sura ya Pili Ibara ya 501 (vii-xii) na 51 (x) ya Ilani ambayo ni: a. Kuimarisha ulinzi na usalama wa ndani ya Nchi hususan maeneo ya kimkakati kama vile bandari, 1Kipengele a-e ni ibara ya 50 (vii –viii na x–xii) na f ni ibara ya 51 (x) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. 12 viwanja vya ndege, na mipakani ili kudumisha amani, utulivu na usalama wa raia na mali zao; b. Kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo makazi, vifaa, zana, mafunzo yanayoendana na teknolojia na mifumo ya intelijensia ya kisasa ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo; c. Kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya ulinzi, usalama, uzalendo wa kitaifa na umuhimu wa kushiriki katika ulinzi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kujiunga na Jeshi la Akiba na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu; d. Kuimarisha ushirikiano na jumuiya za kikanda, kimataifa, na Nchi nyingine katika nyanja za ulinzi na usalama; e. Kuimarisha kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (Tanzania Bara) na Jeshi la Kujenga Uchumi (Zanzibar) ili kuwezesha wahitimu wa Kidato cha Sita na vijana wanaojitolea kwa hiyari kupata fursa ya mafunzo yanayolenga kujenga uzalendo kwa Taifa, moyo wa kujitolea na stadi za kazi; na f. Kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za kulinda amani kupitia misheni za kimataifa ikiwemo za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa 13 ili kuleta utulivu katika Nchi jirani na rafiki zinazokumbwa na migogoro. E. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/26 Makusanyo ya Maduhuli 28. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara ilikadiria kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi 87,603,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu, Fungu 38 - NGOME Shilingi 22,000,000.00, Fungu 39 - JKT Shilingi 64,403,000.00 na Fungu 57 - Wizara Shilingi 1,200,000.00. 29. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mwezi Aprili 2026 Wizara imefanikiwa kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi 180,505,418.00 kutoka kwenye mafungu yake matatu, sawa na asilimia 206.05 ya makadirio. Kwa upande wa Fungu 38 - NGOME limekusanya Shilingi 22,349,954.00 ambazo zimetokana na mauzo ya nyaraka za zabuni (Sale of Tender Documents) na mapato yanayotokana na uwakala wa Bima zilizokatwa na wanajeshi kwa Shirika la Bima la Taifa. 30. Mheshimiwa Spika, Fungu 39 - JKT limekusanya Shilingi 65,603,000.00 zilizotokana na mauzo ya nyaraka za zabuni na mauzo ya mazao ya kilimo, na Fungu 57 - Wizara, limekusanya jumla ya 14 Shilingi 92,552,464.00 zilizotokana na deni la ukodishaji wa simu za ZTE na ukodishaji wa minara ya mawasiliano kwa TTCL. Mchanganuo wa maduhuli kwa kila Fungu umeoneshwa kwenye Jedwali Na. 1 Jedwali Na. 1: Makadirio na Makusanyo ya Maduhuli kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026. Fungu Makadirio ya Maduhuli 2025/26 (Shs) Makusanyo Julai 2025 hadi Aprili 2026 (Shs) 38 – Asilimia ya Makusanyo NGOME 39 – JKT 22,000,000.00 64,403,000.00 22,349,954.00 65,603,000.00 101.59 57 – Wizara 101.86 1,200,000.00 92,552,464.00 Jumla 7,712.71 87,603,000.00 180,505,418.00 Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo Bajeti iliyoidhinishwa 206.05 31. Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliidhinishiwa 3,645,912,947,000.00. jumla Kati ya ya fedha Shilingi hizo, Shilingi 3,327,115,385,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 318,797,562,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo kwa mafungu yake matatu ambayo ni Fungu 57 - Wizara, Fungu 38 - NGOME na Fungu 39 - JKT. Mchanganuo wa Bajeti kwa kila fungu umeainishwa katika Jedwali Na. 2. 15 Jedwali Na. 2: Bajeti Iliyoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Na Fungu Matumizi ya Kawaida (Shs) Matumizi ya Maendeleo (Shs) 1. 38 - NGOME 2,733,729,204,000.00 Jumla (Shs) 2. 39 - JKT 48,867,636,000.00 2,782,596,840,000.00 567,023,845,000.00 9,929,926,000.00 3. 57 - Wizara 576,953,771,000.00 26,362,336,000.00 260,000,000,000.00 Jumla Kuu 286,362,336,000.00 3,327,115,385,000.00 318,797,562,000.00 3,645,912,947,000.00 Fedha zilizopokelewa kuanzia Mwezi Julai 2025 hadi Aprili 2026 32. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2026 fedha zilizopokelewa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo ni Shilingi 3,122,326,357,215.44 sawa na asilimia 85.64 ya Bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 3,011,737,307,354.91 sawa na asilimia 90.52 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 110,589,049,860.53 sawa na asilimia 34.69 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. 33. Mheshimiwa Spika, kati ya Fedha hizo, Fungu 38: NGOME limepokea fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 2,516,758,703,569.18 sawa 92.06, na asilimia na Matumizi ya Maendeleo Shilingi 9,309,160,031.00 sawa na asilimia 19.05; Fungu 39: JKT limepokea fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 470,874,925,482.33 sawa na asilimia 83.04, na Matumizi ya Maendeleo Shilingi 9,929,926,000.00 sawa na asilimia 100; na Fungu 57: Wizara limepokea fedha za Matumizi ya Kawaida 16 17 Shilingi 24,103,678,303.40 sawa na asilimia 91.44, na Matumizi ya Maendeleo Shilingi 91,349,963,829.53 sawa na asilimia 35.13. Muhtasari wa mchanganuo wa mapokezi ya fedha kwa mafungu yote umeainishwa katika Jedwali Na. 3. Jedwali Na. 3: Mapokezi ya Fedha kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026 Fungu Aina ya Matumizi Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Mapokezi ya Fedha kuanzia Julai 2025 Aprili 2026 Asilimia Bajeti vs Mapokezi (Shs) (Shs) 38 - NGOME Mishahara 2,201,453,296,000.00 1,959,480,540,054.58 89.01 Chakula 297,424,825,000.00 253,587,020,749.31 85.26 Posho msamaha wa kodi 97,200,000,000.00 72,900,000,000.00 75.00 Matumizi Mengineyo 137,651,083,000.00 230,791,142,765.29 167.66 Maendeleo 48,867,636,000.00 9,309,160,031.00 19.05 Jumla ya Fungu 2,782,596,840,000.00 2,526,067,863,600.18 90.78 39 - JKT Mishahara 406,799,724,000.00 347,418,712,149.00 85.40 Chakula 76,175,580,000.00 51,758,762,500.00 67.95 Posho msamaha wa kodi 12,015,600,000.00 8,100,000,000.00 67.41 Matumizi Mengineyo 51,032,941,000.00 42,597,450,833.33 83.47 Mafunzo ya Vijana Mujibu 21,000,000,000.00 21,000,000,000.00 100.00 Maendeleo 9,929,926,000.00 9,929,926,000.00 100.00 Jumla ya Fungu 576,953,771,000.00 480,804,851,482.33 83.34 57 - WIZARA Mishahara 10,782,457,000.00 9,963,772,420.00 92.41 Matumizi Mengineyo 15,579,000,000.00 14,139,905,883.40 90.76 Maendeleo 260,000,000,000.00 91,349,963,829.53 35.13 Jumla ya Fungu 286,361,457,000.00 115,453,642,132.93 40.32 JUMLA KUU 3,645,912,068,000.00 3,122,326,357,215.44 85.64 Uhamisho wa Fedha za Matumizi Mengineyo na Maendeleo Fungu 57 - Wizara 34. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026, Fungu 57 - Wizara limepokea uhamisho wa fedha za maendeleo kiasi cha Shilingi 1,331,467,213,231.82 kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,210,974,680,107.34 zimetolewa kugharamia mikataba ya ununuzi wa zana na vifaa kwa matumizi ya JWTZ kutoka kwa wazabuni mbalimbali. Vilevile, Shilingi 117,692,467,011.00 kwa ajili ya kugharamia malipo ya deni la kimkataba na Shilingi 2,980,066,113.12 zimepokelewa miundombinu wezeshi. kugharamia 35. Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara imepokea uhamisho wa fedha kiasi cha Shilingi 7,000,000,000.00 katika Bajeti ya Matumizi Mengineyo kwa ajili ya kugharamia malipo ya madeni ya huduma za matibabu kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, Muhimbili Orthopaedic Institute na Jakaya Kikwete Cardiac Institute Jijini Dar es Salaam. Fungu 38 - NGOME 36. Mheshimiwa Spika, Fungu 38 - NGOME limepokea uhamisho wa fedha za maendeleo wenye jumla ya Shilingi 20,272,046,086.54 kugharamia 18 ununuzi wa vifaa vya mawasiliano vya JWTZ na kugharamia Mradi wa ujenzi wa Jengo la mahafali, Mlango Mkuu na Uzio katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College - NDC Tanzania). Vilevile, limepokea uhamisho wa fedha wenye jumla ya Shilingi 56,132,873,378.00 za Matumizi Mengineyo. Fedha hizo zimetumika kugharamia Operesheni maalumu. Shughuli zilizotekelezwa kwa Fedha za Matumizi ya Kawaida 35. Mheshimiwa Spika, fedha zilizotolewa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kawaida katika Mwaka wa Fedha 2025/26, zimetumika katika maeneo yafuatayo: Mafunzo na Mazoezi ya Kijeshi 36. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu na kusimamia mafunzo mbalimbali ya kijeshi kwa maafisa na askari katika shule na vyuo vya kijeshi ndani na nje ya Nchi. Katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kufanya mazoezi na Nchi rafiki. Mwaka wa Fedha 2025/26 Jeshi lilifanya zoezi lililoshirikisha kamandi za anga za majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Aidha, JWTZ ilifanya Zoezi la Ushirikiano Imara lililoshirikisha majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Mazoezi hayo yameimarisha ushirikiano, mshikamano na utayari kwa majeshi ya 19 Nchi wanachama katika kukabiliana na changamoto za kiusalama ikiwemo ugaidi, uharamia na kukabiliana na majanga. 37. Mheshimiwa Spika, Mafunzo mbalimbali yanaendelea kutolewa kwa maafisa na askari ndani na nje ya Nchi, ili kuiwezesha JWTZ kutekeleza majukumu yake ya kulinda Nchi na mipaka yake kwa ufanisi, kulingana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Askari wa JWTZ wakiwa katika mazoezi ya Kijeshi. Matengenezo na Matunzo ya Zana na Vifaa vya Kijeshi 38. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendelea na programu za kuhakikisha mitambo, magari, zana na vifaa vya kijeshi vinakuwa katika hali 20 nzuri ya kiutendaji, hii ni pamoja na kuvifanyia matengenezo pale inapohitajika. Aidha, kupitia TATC, kituo hicho kinaendelea na tafiti ambazo zimetumika kuwezesha kufanya maboresho ya mitambo, magari, zana na vifaa vilivyopo nchini. Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa 39. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) imeendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya awali ya Kijeshi na stadi za kazi kwa ajili ya kuwajengea uzalendo, umoja wa kitaifa, na uwezo wa kujitegemea. Mafunzo haya hufanyika katika makundi mawili ambayo ni Kundi la Kujitolea na Kundi la Lazima kwa vijana wanaohitimu Kidato cha Sita kwenye kambi mbalimbali za JKT. 40. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha 2025/26 mafunzo yamefanyika kupitia Operesheni Nishati Safi, ambapo jumla ya vijana 34,000 wa Kundi la Lazima walipatiwa mafunzo. Kati yao wavulana ni 25,469 na wasichana ni 8,531. Vilevile, katika Mwaka wa Fedha 2024/25 yamefanyika mafunzo kwa Kundi la Kujitolea kupitia Operesheni Miaka 60 ya Muungano ambapo jumla ya vijana 12,000 wamepatiwa mafunzo. Kati yao wavulana ni 8,536 na wasichana ni 3,464. Aidha, katika mwaka wa fedha 2025/26 jumla ya vijana 12,000 wa kujitolea Operesheni Nishati Safi wanaendelea na mafunzo ambapo kati yao wavulani ni 7,972 na wasichana ni 4,028. 21 41. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha wahitimu wote wa Kidato cha Sita wanapata fursa ya kujiunga na mafunzo ya JKT, miundombinu ya kambi imeendelea kuboreshwa, ambapo hadi kufikia Mwaka wa Fedha 2025/26 ina uwezo wa kuchukua vijana zaidi ya 60,000. Mpango uliopo ni kuendelea kuboresha miundombinu na kufungua kambi mpya, ili kuiwezesha JKT kuchukua vijana 140,000 ifikapo Mwaka 2031, na hatimaye kuwezesha wahitimu wote wa Kidato cha Sita kupata fursa ya kujiunga na mafunzo ya JKT. 42. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kulitaarifu Bunge lako Tukufu pamoja na umma wa Tanzania kwamba, mafunzo yanayotolewa kwa vijana wa JKT yameendelea kuwajengea uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, kuwapatia stadi za kazi katika nyanja mbalimbali na stadi za maisha, ili wakimaliza mafunzo ya JKT waweze kurejea katika jamii wakiwa raia wema wenye uwezo wa kujitegemea na kulilinda Taifa. Nitoe rai kwa vijana wote wanaopata fursa ya mafunzo hayo, kuwa raia wema na kuzitumia stadi walizozipata kujiajiri na kujitegemea. 22 Vijana wa JKT wakiwa kwenye mafunzo ya ukakamavu wakati wa kujiandaa na gwaride la kumaliza mafunzo ya JKT katika Kikosi cha Bulombora JKT mkoani Kigoma. Vijana wa JKT wakiwa kwenye mafunzo ya stadi za kazi ya ufugaji wa kuku wa mayai katika Kikosi cha Ruvu JKT kilichopo mkoani Pwani. 23 Kilimo cha Kimkakati 43. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JKT imeendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa Mageuzi ya Kilimo Ndani ya JKT (2019/20 – 2027/28) unaolenga kuongeza uzalishaji wa mazao na kujitosheleza kwa chakula, ili kuipunguzia Serikali gharama za kulisha vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT na kuchangia katika usalama wa chakula kwa Taifa. Kupitia Mpango huo, JKT imeendeleza ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Chita ambapo hadi sasa ekari 2,500 kati ya 12,000 zimejengewa miundombinu ya umwagiliaji. Aidha, katika Msimu wa Kilimo 2024/25, zimezalishwa tani 1,962.2 za Mpunga, tani 5,864 za Mahindi, tani 6.52 za Maharage na tani 48 za Alizeti. Mafunzo kwa Jeshi la Akiba 44. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kutoa mafunzo kwa Jeshi la Akiba katika mikoa yote ya Tanzania. Mafunzo haya husimamiwa na ofisi za washauri wa Jeshi la Akiba katika mikoa yote kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI. Lengo ni kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa masuala ya Ulinzi, na kuwajengea uwezo katika kulitumikia Taifa lao. Katika Mwaka wa Fedha 2025/26 jumla ya wananchi 14,899 walihitimu mafunzo, ambapo kati yao wanaume ni 12,280 na wanawake ni 2,619. Niwapongeze wahitimu wote na kuwataka waendelee kuviishi viapo vyao vya kulinda raia, kutetea uhuru na 24 uchumi wa Nchi, pamoja na kutii sheria. Nitoe shukrani kwa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI kwa ushirikiano wanaotupatia katika kuratibu mafunzo haya muhimu. Kikundi cha Wanafunzi wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba kikiwa katika Mafunzo ya kujenga utimamu wa mwili wilayani Magu mkoani Mwanza Mwaka 2025. Huduma za Afya na Tiba 45. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi husika, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kutoa huduma za matibabu kwa maafisa, askari, watumishi wa umma, na familia zao pamoja na wananchi. Katika kuboresha huduma za afya, juhudi mbalimbali zimefanyika ikiwemo ujenzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Jeshi Dodoma unaoendelea kwa awamu, ambapo Awamu ya Kwanza hadi ya Nne zimekamilika. Kwa sasa, Awamu ya Tano inaendelea 25 kwa ujenzi wa Diagnostic Radiology Centre na ununuzi wa vifaa tiba ili Hospitali ianze kutoa huduma. 46. Mheshimwa Spika, JWTZ imeboresha upatikanaji wa huduma muhimu katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, zikiwemo za usafishaji wa figo, uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo. Hospitali zote za kanda za Jeshi zina vifaa vya kisasa vya kutolea huduma za kibingwa vikiwemo vya kuhudumia wagonjwa mahututi. Pia, zinatoa huduma ya vipimo vya Advanced Ultrasound na Digitalized X – Ray. Vilevile, huduma katika vituo vya tiba vikosini zinaendelea kuboreshwa, kwa vituo hivyo kupatiwa vifaa tiba, kuongezewa madaktari na kutumia mifumo ya TEHAMA. Stahiki kwa Wanajeshi na Watumishi wa Umma 47. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa stahiki mbalimbali kwa wanajeshi na watumishi wa umma, ikiwemo mishahara na malipo ya likizo. Vilevile, imeendelea kugharamia mafunzo mbalimbali ya kitaalam kuwawezesha watumishi kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. Ushirikiano na Mamlaka za Kiraia katika shughuli mbalimbali 48. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia, kupitia huduma za moja kwa moja na miradi ya maendeleo. 26 Mbali na jukumu la msingi la ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JWTZ ina jukumu la kisheria la kusaidia Mamlaka za Kiraia wakati wa majanga au uhitaji wa dharura. Katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Jeshi limeimarisha utayari wa kukabiliana na dharura na limeshiriki katika usafirishaji wa chakula wakati wa mafuriko katika Nchi ya Msumbiji kuanzia tarehe 17 hadi 24 Machi, 2026. Vilevile, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushiriki katika ulinzi wa miradi ya kimkakati ikiwemo Reli ya kisasa (SGR), Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP), Mgodi wa Tanzanite, Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Daraja la Kigongo - Busisi, Bandari, Mkongo wa Taifa, na maeneo ya viwanja vya ndege. Jeshi lipo tayari kushirikiana na Mamlaka za Kiraia muda wote litakapohitajika. Ushiriki katika Michezo Kitaifa na Kimataifa 49. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ulinzi na JKT inatambua vema mchango wa michezo kwa ustawi wa Wanajeshi wetu. Hivyo, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara imeiwezesha JWTZ kushiriki kwa mafanikio katika michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, Riadha, Ngumi, Pool table na Kuogelea. Aidha, naomba kulijulisha Bunge lako Tukufu japo kwa uchache baadhi ya mafanikio ambayo Wizara kupitia JWTZ imeyapata katika michezo hiyo. 27 50. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mpira wa miguu, Wizara ina timu mbili za wanaume zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Timu hizo ni Mashujaa FC na JKT Tanzania ambazo zinamilikiwa na JWTZ na JKT mtawalia. Vilevile, JWTZ ina timu nne zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship). Timu hizo ni TMA Stars, Mbuni Football Club, Transit Camp na Gunners, ambazo zinafanya vizuri katika Ligi hiyo, na ni matumaini yangu zitapanda daraja na hivyo kuongeza timu za Jeshi zinazoshiriki Ligi Kuu. 51. Mheshimiwa Spika, Wizara ina timu mbili za mpira wa miguu wa wanawake ambazo zinashiriki katika mashindano ya ligi kuu ya kitaifa. Timu hizo ni JKT Queens na Mashujaa Queens ambazo zinamilikiwa na JKT na JWTZ mtawalia. Aidha, nina furaha kuwajulisha kuwa JKT Queens ni mabingwa wa Council for East and Central Africa Football Associations (CECAFA) kwa mwaka 2025, ilitwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo uliofanyika tarehe 16 Septemba, 2025. Ushindi huu uliiwezesha Timu hiyo kufuzu kuuwakilisha Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Klabu Bingwa ya Afrika Mwaka 2025. 52. Mheshimiwa Spika, Wizara katika mwaka wa Fedha 2025/26, imeshiriki katika mashindano ya Mei Mosi yaliyofanyika mkoani Njombe na kuwa mshindi wa kwanza wa jumla katika michezo mbalimbali. Aidha, Shirika la Mzinga limeshiriki katika Mashindano ya 28 Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 06 Desemba, 2025 na limeweza kushika nafasi ya kwanza kwa mshindi wa jumla katika michezo hiyo. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu akimkabidhi Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kombe la Ushindi wa Jumla la Michezo ya Mei Mosi mkoani Njombe tarehe 01 Mei, 2026. 53. Mheshimiwa Spika, katika mchezo wa riadha, Sajini Taji Alphonce Felix Simbu amekuwa Bingwa wa Dunia wa mashindano ya Riadha ya Dunia (World Athletics Championship 2025) Tokyo Japan yaliyofanyika tarehe 15 Septemba, 2025 na kuwa Mtanzania wa kwanza kupata Medali ya Dhahabu katika 29 mashindano hayo. Vilevile, katika mashindano ya Boston Mararthon yaliyofanyika nchini Marekani tarehe 20 Aprili, 2026 alishika nafasi ya pili na kupewa Medali ya Fedha. Aidha, wanariadha wengine walioshinda ni pamoja na Sajini Secilia Ginoka Panga mshindi wa kwanza katika mbio za kimataifa za Sao Silvester zilizofanyika nchini Brazil tarehe 31 Desemba, 2025 na kufanikiwa kupata Medali ya Dhahabu, Koplo Magdalena Crispin Shauri mshindi wa kwanza katika mbio za kimataifa za AI Shargiyal (Shargiyal International Half Marathon) zilizofanyika nchini Saudi Arabia tarehe 21 Januari, 2026 na kupata Medali ya Dhahabu, na Praiveti Sinda Godfrey Sinda mshindi wa pili katika mbio za kimataifa za CPC Loop Den Haag zilizofanyika nchini Uholanzi tarehe 15 Machi, 2026 na kufanikiwa kupata Medali ya Fedha. 30 Sajini Taji Alphonce Felix Simbu Bingwa wa Dunia wa mashindano ya Riadha katika World Athletics Championship 2025 yaliyofanyika Tokyo Japan tarehe 15 Septemba, 2025 na kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kupata Medali ya Dhahabu. 54. Mheshimiwa Spika, katika mashindano ya Pool table Barani Afrika yaliyofanyika Durban nchini Afrika Kusini, Mwezi Februari 2026 Mtumishi wa Umma Bi. Rosemary Deus Kazaura alishiriki na kuwa mchezaji bora na kupata Medali ya Dhahabu. Aidha, ushiriki wa JWTZ katika mashindano mbalimbali umekuwa na mafanikio kutokana na maandalizi mazuri ya timu pamoja na uwezeshwaji unaofanywa na Wizara kupitia 31 JWTZ. Mbali na kujenga ukakamavu kimwili kwa wanajeshi, michezo inasaidia kujenga mahusiano mazuri kwa wananchi na majeshi mengine. 55. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mchezo wa ngumi, mabondia wa JWTZ wanaume na wanawake wameendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya Nchi. Katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Nchi ya Comoros yaliyofanyika tarehe 06 Julai, 2025, mabondia Koplo Ezra Mwanjwango na Praiveti Kassim Mbundikwa walishinda Medali ya Dhahabu. 56. Mheshimiwa Spika, pia Wizara imeshiriki katika michezo mingine ndani na nje ya nchi ikiwemo mpira wa magongo, vishale (darts), mpira wa wavu (volleyball), mpira wa pete (netball), mpira wa kikapu (Basketball) na Golf. Katika michezo hiyo, timu zetu zilifanya vizuri. Ushiriki na ushindi wa wanamichezo wetu katika mashindano haya, umeweza kuIiIetea Taifa Ietu medaIi, heshima pamoja na kuimarisha mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki. Napenda kutumia fursa hii, kuwapongeza washindi wote. 57. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutunukiwa Nishani ya juu ya heshima ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) ijulikanayo kama THE GRAND CORDON tarehe 14 Agosti, 2025 kwa mchango 32 mkubwa wa kufikia malengo ya CISM. Vilevile, nawapongeza viongozi wote wa JWTZ kwa kutoa uzito katika michezo na kuunga mkono maono ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuimarisha miundombinu ya michezo. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu akipokea Nishani ya juu ya heshima ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) ijulikanayo kama THE GRAND CORDON tarehe 14 Agosti, 2025 Ikulu Chamwino Dodoma. 33 58. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, kupitia Bunge lako Tukufu napenda kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa mchango wake uliowezesha wanamichezo wetu kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Nchi na kuliletea sifa na heshima Taifa letu. 59. Mheshimiwa Spika, napenda pia, kutoa taarifa kuwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Baraza la Michezo Tanzania 2026 iliyofanyika tarehe 09 Mei, 2026, Sajini Taji Alphonce Felix Simbu alitangazwa kuwa Mwanamichezo Bora wa Kiume, Praiveti Stumai Abdallah Mwanamichezo Bora wa Kike ambaye ni mchezaji wa JKT Queens na Timu ya Taifa ya Wanawake, Mteule Daraja la Kwanza Anthony Mwingereza (Mstaafu) Kocha Bora kwa upande wa wanaume na Klabu ya JKT Queens ilitangazwa kuwa Klabu Bora kwa upande wa wanawake kutokana na mafanikio makubwa iliyoyapata katika mashindano mbalimbali. Masuala Mtambuka 60. Mheshimiwa Spika, Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake imeendelea kuzingatia masuala mtambuka katika utekelezaji wa shughuli zake kwa kutumia Bajeti ya Matumizi ya Kawaida. Masuala hayo yanajumuisha mapambano dhidi ya magonjwa ambukizi na sugu yasiyoambukiza, utawala bora na mazingira. 34 Mapambano dhidi ya magonjwa ambukizi na sugu yasiyoambukiza 61. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara imeendelea kutekeleza mikakati ya kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI na Magonjwa Sugu yasiyoambukiza. Mikakati hiyo inajumuisha kuhamasisha watumishi kupima ili kufahamu hali za afya zao. Aidha, Wizara imeendelea kutoa huduma ya lishe kwa watumishi wanaoishi na Virusi vinavyosababisha Upungufu wa Kinga Mwilini. Hatua hizi zinachukuliwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Udhibiti VVU na UKIMWI mahali pa kazi. Utawala Bora 62. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha Utawala Bora kwa kuzingatia miongozo ya kupambana na rushwa, sheria za matumizi ya fedha na ununuzi, ambapo taarifa za ukaguzi na ununuzi zimekuwa zikiandaliwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka husika. 63. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26 Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake imeendelea na jitihada mbalimbali ili kuimarisha Utawala Bora kwa kuzingatia sheria za matumizi ya fedha na ununuzi, kuhakikisha matumizi ya fedha na ununuzi yanafanyika kwa ufanisi, kuzingatia thamani ya fedha na kaguzi kufanyika ipasavyo. Katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya 35 Mwaka wa Fedha 2024/25, Wizara na taasisi zilizo chini yake imeendelea kupata Hati Inayoridhisha (Safi) ya Ukaguzi. 64. Mheshimiwa Spika, taarifa za kila Robo Mwaka huwasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Vilevile, semina mbalimbali kuhusu jinsi ya kupambana na kuzuia rushwa mahala pa kazi zimeendelea kutolewa kwa watumishi. Wizara imekuwa ikishirikisha watumishi katika kutoa maoni na ushauri kupitia vikao mbalimbali, hususan Baraza la Wafanyakazi, Kamati ya Maadili na Kamati ya Ajira. Pia, Wizara inaendelea kutoa huduma bora kwa wateja kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali. Utunzaji wa Mazingira 65. Mheshimiwa Spika, Wizara imechukua hatua mahususi ili kutimiza Azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi. Katika kipindi husika kupitia taasisi zilizo chini yake, imeendelea na utunzaji wa mazingira katika maeneo yake yenye miti ya asili, kwa kulinda maeneo hayo yasivamiwe kwa shughuli za kijamii, na kuendelea kupanda miti mipya. Katika Mwaka wa Fedha 2025/26 Wizara na taasisi zake imeweza kupanda miti mipya 209,794 katika kambi mbalimbali za Jeshi. Vilevile, Wizara imeendelea na upimaji na uwekaji wa alama za mipaka katika maeneo ya Jeshi yakiwemo yenye misitu na ardhi oevu. Hatua 36 hii imepunguza uvamizi, uharibifu wa mazingira na migogoro ya ardhi inayotokana na shughuli za kibinadamu zikiwemo uchomaji mkaa, ukataji miti, uchimbaji madini, kilimo na ufugaji. 66. Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi ya nishati safi JWTZ na kambi zake zinazolisha zaidi ya watu 100 yamefikia asilimia 92 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, JKT imefikia asilimia 100, Shirika la Mzinga asilimia 98, na Shirika la Tanzania Automotive Technology Center (TATC) asilimia 98. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kambi zote za JKT. Vilevile, shughuli zilizotekelezwa hadi hivi sasa ni kutengeneza mashine za kuzalisha mkaa mbadala, utengenezaji wa miundombinu ya mitambo ya gesivunde (biogas plant) katika baadhi ya vikosi vya JKT na kufundisha vijana kutengeneza mkaa banifu katika kambi zote za JKT. 37 Majiko ya kisasa ya kupikia kwa kutumia nishati safi ya Gesi katika Kikosi cha Msange JKT kilichopo mkoani Tabora. Shughuli zilizotekelezwa kwa kutumia Fedha za Maendeleo 67. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Fungu 57 - Wizara imetumia fedha za maendeleo kutekeleza shughuli mbalimbali zifuatazo: a. Kugharamia malipo ya mikataba mbalimbali ya ununuzi wa zana na vifaa kwa matumizi ya JWTZ; b. Utafiti wa uhuishaji wa silaha, zana na vifaa kwa matumizi ya Jeshi; c. Ununuzi wa mitambo na malighafi za kuzalisha mazao ya msingi kwa Shirika la Mzinga; d. Kufanya maboresho ya vifaa vya ulinzi wa anga; e. Kutekeleza shughuli za utafiti na uhawilishaji wa teknolojia katika Shirika la TATC; 38 39 f. Kugharamia maboresho, huduma ya ulinzi na malipo ya huduma ya umeme kwenye minara ya Mawasiliano Salama Jeshini; g. Kugharamia ufuatiliaji na tathmini wa miradi na shughuli mbalimbali za Wizara; na h. Kulipa fidia ya ardhi katika maeneo yaliyofanyiwa uthamini, kama inavyoonekana katika Jedwali Na 4. Jedwali Na. 4: Maeneo Yaliyolipwa Fidia ya Ardhi kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026 Na Eneo Mkoa Kiasi kilicholipwa (Shs) 1. Fidia kwa wananchi 989 eneo la Mboghwe - Nzega. Tabora 4,869,631,375.08 2. Fidia ya wananchi 121 eneo la Pongwekiona – Chalinze. Pwani 4,180,632,171.00 3. Fidia ya wananchi 34 eneo la Buhale – Musoma. Mara 278,427,710.83 4. Fidia ya mwananchi mmoja eneo la Buhongwa - Nyamagana. Mwanza 18,639,400.00 5. Fidia ya wananchi 10 eneo la Rasi Nondwa - Kasulu. Kigoma 733,602,415.00 6. Fidia ya wananchi wawili eneo la Chungu – Ikungi. Singida 10,840,767.00 7. Fidia ya mwananchi mmoja eneo la Bweni - Pangani Tanga 2,000,000,000.00 Jumla 12,091,773,838.91 68. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Fungu 38: NGOME limetumia fedha za maendeleo kutekeleza shughuli mbalimbali zifuatazo: a. Kugharamia ununuzi wa risasi, mabomu na milipuko kwa ajili ya mafunzo, oparesheni na mazoezi; b. Kuendeleza ujenzi wa Shule ya Polisi Jeshi Mafinga mkoani Iringa; c. Kuendeleza ujenzi wa Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Anga; d. Umaliziaji wa Ujenzi wa Ukumbi SKUA – Tanga; e. Ujenzi wa Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Akiba; na f. Kugharamia uboreshaji wa miundombinu ya vyuo, shule na vikosi. 69. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Fungu 39: JKT limetumia fedha za maendeleo kutekeleza miradi ifuatayo: a. Kuendeleza ujenzi wa Kikosi kipya cha Tanganyika; b. Kumalizia ujenzi wa majengo ya Makao Makuu ya JKT; c. Ujenzi wa mahanga katika Kiteule cha Chenene - Kikosi cha Makutupora JKT; na d. Kuendeleza ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji Chita, Morogoro na kuanzisha ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji katika Kiteule cha Chenene - Kikosi cha Makutupora JKT- Dodoma. 40 Ujenzi wa Majengo ya Utawala katika Kikosi kipya cha Tanganyika kilichopo Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi. 70. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia mashirika yake ya Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), Mzinga, na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) imeendelea kutekeleza majukumu yake ifuatavyo: Tanzania Automotive Technology Centre 71. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) liliidhinishiwa fedha kiasi cha Shilingi 15,000,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Hadi kufikia Mwezi Aprili 2026, limepokea Shilingi 5,500,000,000.00 sawa na asilimia 36.67. Fedha hizo zimetumika kugharamia: ukamilishaji wa miundombinu ya Jengo, ununuzi wa mashine na mitambo kwa ajili ya Karakana ya Grey and 41 ductile Iron; ununuzi wa malighafi na mitambo kwa ajili ya kukamilisha Mradi wa Cupola Furnace; ukarabati wa miundombinu ya milki; na kuendeleza tafiti za teknolojia ya magari na bidhaa za viwandani. 72. Mheshimiwa Spika, aidha, Shirika la TATC limekamilisha taratibu za kuingia ubia kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari na kampuni ya STREIT Group kutoka Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE). Manufaa yatakayopatikana kutokana na ubia huu ni kuongeza mtaji, kuongeza ajira, kupata teknolojia na kuimarisha uwezo wa kuunda magari ya Deraya na kiraia. Shirika la Mzinga 73. Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/26, Shirika la Mzinga liliidhinishiwa fedha kiasi cha Shilingi 6,000,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili 2026, Shirika limepokea Shilingi 4,674,582,595.94 sawa na asilimia 77.91. Fedha hizo zimetumika kugharamia ununuzi wa mashine na malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya msingi. Aidha Shirika katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya msingi kwa ajili ya JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi na usalama lipo katika mchakato wa kuanzisha kiwanda kipya (Mzinga II) ambapo hatua iliyofikiwa sasa ni kuandaliwa kwa Mkataba kati Shirika na Mzabuni. 42 Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), akiwa na Wajumbe wa Kamati walipotembelea miradi ya maendeleo katika Shirika la Mzinga mkoani Morogoro tarehe 17 Machi, 2026. Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa 74. Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/26, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) liliidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,000,000,000.00 kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa mitambo. Hadi kufikia mwezi Aprili 2026 Shirika limepokea kiasi kilichoidhinishwa, ambacho kimetumika kugharamia ununuzi wa mitambo na zana za kilimo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali. 43 Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT akipewa maelezo ya ushonaji wa Sare za vijana wa JKT katika kiwanda cha ushonaji nguo cha SUMAJKT Garment. CO. Ltd kilichopo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea shughuli zinazofanywa na SUMAJKT tarehe 12 Mei, 2026. 75. Mheshimiwa Spika, kwa kutumia vyanzo vya ndani vya mapato, Shirika limeendelea na shughuli za uzalishaji mali kupitia kampuni tanzu na viwanda vyake, ili kuchangia katika uchumi wa Nchi na kuipunguzia Serikali gharama za malezi ya vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT. Shughuli hizo zinatekelezwa kupitia sekta za ujenzi, viwanda, biashara na huduma, kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na elimu. 44 F. USHIRIKIANO WA KIULINZI KIKANDA NA KIMATAIFA Ushirikiano na Nchi nyingine 76. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kwa kushiriki vikao vya kikanda na kimataifa katika kuimarisha ulinzi na usalama duniani. 77. Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushirikiana na Nchi rafiki katika masuala ya ulinzi na usalama kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo mafunzo, mazoezi na misaada ya kitaalamu. Pia, tumeendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mafunzo, mazoezi, ubadilishanaji wataalamu na taarifa, na kufanya operesheni mbalimbali. Nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini, Angola, Algeria, Brazil, Bangladesh, Botswana, Burundi, Canada, Comoros, China, Cuba, DRC, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Finland, Ghana, Hispania, India, Indonesia, Israel, Jamhuri ya Czech, Jordan, Kenya, Malawi, Marekani, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Oman, Kuwait, Pakistan, Rwanda, Sri Lanka, Sweden, Ufaransa, Uganda, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Uturuki, Uswisi, Zambia na Zimbabwe. 45 Mhe. Dkt. Rhimo S. Nyansaho (Mb.), Waziri wa Ulinzi na JKT na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Zambia ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Ulinzi, Mhe. Jackob Jack Mwiimbu, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Ushirikiano wa Kamisheni ya Kudumu ya masuala ya Ulinzi na Usalama baina ya Tanzania na Zambia, tarehe 27 Februari, 2026 Jijini Arusha. Mafunzo ya Usalama na Stratejia 78. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Chuo cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania (NDC - Tanzania) imeendelea kutoa mafunzo ya Usalama na Stratejia kwa maafisa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Utumishi wa Umma. Mafunzo yanayotolewa na Chuo hiki ni ya uongozi katika ngazi ya Kisera na Kistratejia. Katika mafunzo hayo tunashirikiana na Nchi mbalimbali ambazo ni pamoja na Afrika Kusini, Bangladeshi, 46 Botswana, Burundi, China, Ethiopia, India, Kenya, Malawi, Misri, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, Uganda, Zambia na Zimbabwe. 79. Mheshimiwa Spika, Nchi rafiki zinazoleta viongozi wake kupata Mafunzo Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania inaonesha ubora na viwango vya kimataifa vya Mtaala, uhusiano mzuri na mataifa hayo, na mchango wa Tanzania katika kuandaa viongozi katika Usalama na Stratejia kitaifa, kikanda na kimataifa. Kupitia Mafunzo haya, Wizara inashiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa Diplomasia ya Ulinzi na ujenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Nchi rafiki; masuala ambayo yanaendelea kuimarishwa na Serikali ya Awamu ya Sita. 80. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2025/26, Chuo kimeendesha mafunzo kwa viongozi waandamizi wa Serikali na Sekta Binafsi kuanzia tarehe 09 - 13 Machi, 2026. Mada kuu ya Kozi hii ilikuwa “Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Kuchochea Maendeleo Endelevu ya Taifa,” (Public Private Partnership (PPP) for Sustainable National Development). Washiriki wa Kozi hii walikuwa ni baadhi ya makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wa wizara, watendaji wakuu wa taasisi za umma, watendaji wakuu wa taasisi za binafsi, viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na maafisa kutoka vyombo vya ulinzi na usalama. 47 Dkt. Natu El - Maamry Mwamba Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, akitoa mhadhara kuhusu ustawi wa uchumi na umuhimu wa usalama Tanzania kwa washiriki wa kozi ya NDC kundi la kumi na nne tarehe 30 Aprili, 2026. 81. Mheshimiwa Spika, pia, Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Arusha vimeendelea kuendesha mafunzo kwa kushirikiana na Nchi mbalimbali. Mafunzo hayo yameendelea kuimarisha uhusiano na diplomasia ya ulinzi. Ushiriki wa JWTZ katika Ulinzi wa Amani 82. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushirikiana na Jumuiya za Kimataifa na Kikanda katika operesheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Kwa sasa JWTZ ina vikundi vya ulinzi wa Amani katika Nchi za DRC (MONUSCO), Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) na Lebanon (UNIFIL). Kwa ujumla hali ya usalama wa 48 vikundi hivyo vinavyoshiriki Ulinzi wa Amani ni shwari na vinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuboresha hali ya zana na vifaa kwa JWTZ na katika vikundi vinavyoshiriki katika majukumu ya Ulinzi wa Amani ili kuimarisha zaidi utendaji kazi. G. MPANGO NA MWELEKEO WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2026/27 83. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2026/27, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imelenga kutekeleza Mpango na Bajeti kwa kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2026/27 – 2030/31), Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Mpango Mkakati wa Wizara (2026/27 – 2030/31) na Taasisi zake na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27. 84. Mheshimiwa Spika, naomba uniruhusu kuwasilisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 ifuatavyo: Makadirio ya Makusanyo ya Maduhuli 85. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2026/27, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi 90,603,000.00 kutoka katika mafungu 49 yake matatu. Fungu 38 - NGOME linatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 22,000,000.00, Fungu 39 - JKT linatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 67,403,000.00 na Fungu 57 - Wizara inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 1,200,000.00 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 5. Jedwali Na. 5: Makadirio ya Makusanyo ya Maduhuli kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 Na. Fungu Makadirio ya Maduhuli 2026/27 (Shs) 1. 38 – NGOME 2. 39 – JKT 22,000,000.00 67,403,000.00 3. 57 – Wizara Jumla 1,200,000.00 90,603,000.00 Matumizi ya Kawaida na Maendeleo 86. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2026/27, Serikali inatarajia kutenga fedha kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo jumla ya Shilingi 4,286,489,324,427.00 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 3,859,955,671,427.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, na Shilingi 426,533,653,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. 87. Mheshimiwa Spika, kati ya Fedha hizo, Fungu 38 - NGOME linatarajia kutengewa Shilingi 3,198,126,934,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 54,867,636,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Fungu 39 - JKT linatarajia kutengewa Shilingi 626,273,760,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya 50 51 Kawaida na Shilingi 19,929,926,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Fungu 57 - Wizara linatarajia kutengewa Shilingi 35,554,768,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 351,736,091,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Mchanganuo kwa kila Fungu ni kama ilivyoainishwa katika Jedwali Na. 6. Jedwali Na. 6: Mchanganuo wa Bajeti kwa kila Fungu kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 Na Fungu Matumizi ya Kawaida (Shs) Matumizi ya Maendeleo (Shs) Jumla ya Fedha zitakazotengwa (Shs) 1. 38 - NGOME 3,198,126,934,000.00 54,867,636,000.00 3,252,994,570,000.0 0 2. 39 - JKT 626,273,760,000.00 19,929,926,000.00 646,203,686,000.00 3. 57 - Wizara 35,554,768,000.00 351,736,091,000.0 0 387,290,859,000.00 Jumla 3,859,955,462,000.00 426,533,653,000.00 4,286,489,115,000.00 88. Mheshimiwa Spika, shughuli zinazokusudiwa kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2026/27 zitazingatia maeneo ya kipaumbele yafuatayo: a. Kuliimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, kiteknolojia, mawasiliano na rasilimali watu; b. Kuendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa wanajeshi ikiwemo kutunza vifaa na zana, mazoezi, mafunzo, maslahi, huduma za afya na makazi; c. Kuendelea kuimarisha uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuboresha miundombinu, ili liweze kuchukua vijana wengi zaidi watakaopata mafunzo ya awali ya kijeshi na stadi za kazi; d. Kuendelea kuliimarisha Jeshi la Akiba; e. Kuendeleza na kulinda miradi ya kimkakati kwa maslahi mapana ya Taifa; f. Kuimarisha mashirika na taasisi za utafiti wa masuala ya kijeshi, kuanzisha viwanda vipya katika Sekta ya Ulinzi (Defence industries) vitakavyozalisha bidhaa kwa matumizi ya Kijeshi na Kiraia. Pia, kuanzisha viwanda vipya kwa kushirikiana na Sekta Binafsi; g. Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na kati ya Nchi na Nchi katika masuala ya ulinzi; na h. Kuendelea kushirikiana na Mamlaka za kiraia katika kukabiliana na majanga na dharura inapohitajika. H. SHUKRANI 89. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha Hotuba yangu, napenda kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi na watendaji wa Wizara ninayoiongoza na taasisi zake kwa ushirikiano wanayoifanya, na wanaonipatia, michango kazi yao kubwa madhubuti iliyowezesha kutekeleza Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/26 kwa mafanikio na ushirikiano mkubwa katika kutayarisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 ninayoyawasilisha. Napenda kumshukuru Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na 52 Jeshi la Kujenga Taifa, Jenerali Jacob John Mkunda, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi na JKT, Wakuu wa Mashirika, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Vyuo, Shule na Vikosi vya Jeshi. Vilevile, nawashukuru maafisa, askari na watumishi wa umma kwa ushirikiano wanaonipatia. Mafanikio tuliyopata ni kutokana na bidii, nidhamu, uhodari na kujituma kwao. 90. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii, kwa niaba ya Serikali kutoa shukrani kwa washirika wa maendeleo na serikali za Nchi mbalimbali kwa ushirikiano wanaoendelea kuipatia Wizara ninayoiongoza. Washirika hao ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Pia, tunazishukuru Nchi rafiki katika shughuli zetu za ulinzi ambazo ni pamoja na Afrika Kusini, Algeria, Angola, Bangladesh, Burundi, Jamhuri ya Watu wa China, Cuba, Jamhuri ya Czech, Ethiopia, Finland, Ghana, Hispania, India, Indonesia, Israel, Jordan, Kenya, Msumbiji, Kuwait, Malawi, Marekani, Misri, Morocco, Nigeria, Oman, Pakistan, Rwanda, Serbia, Sri Lanka, Sweden, Uganda, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Uingereza, Umoja wa 53 Falme za Kiarabu, Urusi, Uswisi, Uturuki, Zambia na Zimbabwe. 91. Mheshimiwa Spika, naomba pia kuzishukuru wizara na taasisi zote, na wananchi wote kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Wizara ya Ulinzi na JKT na taasisi zake katika ulinzi wa Nchi yetu. Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana zaidi kwa manufaa ya Taifa letu. 92. Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru familia yangu kwa uvumilivu na upendo wao mkubwa kwangu unaoniwezesha kutekeleza majukumu yangu kwa utulivu. 93. Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe binafsi, Mawaziri wenzangu na Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii, inapatikana pia katika tovuti ya Wizara ya Ulinzi na JKT ambayo ni www.modans.go.tz I. HITIMISHO 94. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, Wizara ya Ulinzi na JKT na taasisi zilizo chini yake inaliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 4,286,489,115, 000.00 kati ya fedha hizo, Shilingi 3,859,955,462,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 426,533,653,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. 95. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja. 

Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mabeyo akiwasili bungeni kusikiliza bajeti ya Wizara hiyo

Wakuu wa majeshi wastaafu Waitara na Mwamunyage wakiwasili nao


Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda na wasaidizi wake wakibadilishana mawazo wakati wakimsubili Waziri wa ulinzi



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Nyansaho (Kushoto), akisalimiana na Mkuu wa  Majeshi  Jenerali Mkunda baada ya kuwasili viwanja vya bunge kwa ajili ya uwasilishaji wa bajeti ya Wizara yake










 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?