MBUNGE LUFUNGIJA ALILIA MAENDELEA JIMBONI KWAKE SERIKALI YAAHIDI KUMPELEKEA
Mbunge wa jimbo la Ulyangulu CCM, Masanja Lufungija (pichani) leo akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani, ameitaka Serikali kukamilisha ujenzi wa vituo vya Polisi vilivyojengwa na wananchi kwa kujitolea imebaki umaliziaji tuu wa kuezeka mabati na sakafu. Akijibu maswal ya wabuge waliochangia bajeti hiyo Waziri wa wizara hiyo Protas Katambi amemhakikishia mbunge huyo kwamba bajeti ya mwaka huu watahakikisha maboma hayo yanamaliziwa ili kuwe na vituo hivyo . Kabla ya hapo katika maswali ya asubuhi alimuuliza Waziri wa ujenzi ni lini Barabara ya Kahama Ulyangulu Kaliua Mpanda itajengwa kwani tangu mwaka 2015 aliahidi mgombea urais pia na Mgombea Mwenza kwamba ingejengwa hadi leo haijajengwa.
Comments
Post a Comment