RIDHIWANI AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YAKE NA YAPITA BIRA KUPINGWA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete leo, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo mbele ya wabunge jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema Serikali kupitia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeimarisha maadili ya viongozi wa umma ambapo asilimia 85 ya viongozi wamewasilisha matamko ya mali na madeni yao.

Amebainisha kwamba  hatua hiyo inaonyesha kuimarika kwa uwajibikaji wa viongozi na uaminifu wa wananchi kwa taasisi za umma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kujenga Serikali inayowajibika, yenye uwazi na inayoaminika kwao.
Pia Ridhiwani amesema wananchi 34,334 wamepatiwa elimu ya maadili, hatua inayochangia kukuza utamaduni wa uadilifu na uwajibikaji katika jamii.
Aidha Waziri Ridhiwani amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kusimamia maadili kwa vitendo kwa sababu uadilifu wa viongozi ndio msingi wa haki, maendeleo na imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Amebainisha na kusema kwamba Serikali itaendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kuwa mtumishi bora ndiye msingi wa huduma bora kwa mwananchi na jumla ya viongozi 4,867 walisaini Hati ya Ahadi ya Uadilifu ambapo viongozi wanaume ni asilimia 69 na wanawake ni asilimia 31.

Waziri Ridhiwani amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Bajeti hiyo ilipitishwa na wabunge wakitoa michano yao walimtaka akachape kazi bilakuwaonea woga  wanaotaka kukwamisha juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge wengi waliipongeza TAKUKURU kwa usimamizi wake mzuri wa kujenga ofisi zake kwa umakini mikoani.

Wabunge hao waliwamiminia sifa Waziri na Naibu wake Regina Qwaray,  kwa uchapa kazi wao huku wakiwa wanyenyekevu kwa kila mtu.


Wakuu wa  Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo wakifatilia  kwa umakini mkubwa


Wageni waliotembelea bunge nao wakishuhudia










Waziri  Ridhiwani na Naibu wake  Regina wakibadilishana mawzo na Mbunge wa Misungwi,Silvery  Ruboja Salvatory Rutaba  katika viwanja vya bunge





Wakiandaa nondo au majibu ya kuja kuwajibu wabunge waliochangia bajeti yao











 Naibu Waziri, Regina akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya michango ya wabuge leo

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?