RAIS SAMIA AZINDUA MINARA 758 YA MAWASILIANO, ATAKA HUDUMA ZIWAFIKIE WANANCHI WOTE NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla akisaini Hati ya Makabidhiano kati ya Serikali na Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yas Tanzania Bw. Pierre Canton-Bacara (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Charles Kamoto wa kwanza (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Mtandao wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Andrew Lupembe katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 10 Aprili, 2026.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Angellah Kairuki pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 10 Aprili, 2026. Rais Dkt. Samia alipewa zawadi hiyo kutokana na kutambua mchango wake kwenye Sekta hiyo ya Mawasiliano.
Rais JDkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Yas Tanzania Bw. Pierre Canton-Bacara kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 10 Aprili, 2026.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi wa Miundombinu ya Mtandao kutoka Kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Andrew Lupembe kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 10 Aprili, 202
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Charles Kamoto kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 10 Aprili, 2026.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) CPA. Moremi Marwa kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 10 Aprili, 2026.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 10, 2026 amezindua minara 758 ya mawasiliano pamoja na maunganisho ya Mkongo wa Taifa katika wilaya 85 nchini, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wa kidijitali na kupanua huduma za mawasiliano kwa wananchi.
Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ambapo Rais Samia amesisitiza kuwa mawasiliano sasa ni nguzo muhimu ya uchumi wa kisasa, uwekezaji na utoaji wa huduma za kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Shaaban Kissu, uwekezaji huo una lengo la kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi wengi zaidi hususan walioko vijijini na mipakani.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia pia ameiagiza Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha maeneo ambayo bado hayajafikiwa na Mkongo wa Taifa yanaunganishwa kwa wakati, sambamba na kuelekeza juhudi zaidi katika ngazi za chini ili kuongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali.
Aidha, Rais amezitaka halmashauri zote nchini kuondoa urasimu katika utoaji wa vibali vya miradi ya mawasiliano ili kuharakisha utekelezaji wake, akibainisha kuwa ucheleweshaji huongeza gharama na kuchelewesha huduma kwa wananchi.
Katika taarifa hiyo, imebainishwa pia kuwa Rais Samia amesisitiza ulinzi wa miundombinu ya mawasiliano akieleza kuwa ni rasilimali ya kimkakati kwa uchumi na usalama wa taifa, pamoja na kuagiza huduma zinazotolewa kuzingatia maadili, mila na utamaduni wa Mtanzania.
Serikali imeendelea kuchukua hatua za kukuza sekta ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika ubunifu wa kidijitali na kuwawezesha vijana, hatua inayotarajiwa kuongeza ajira na ushindani wa kimataifa.
Comments
Post a Comment