MAANDALIZI YA BUNGE MARATHON YAZIDI KUNOGA
Mwenyekiti wa Bunge Bonanza na Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga (katikati) amesema maandalizi ya mbio za hisani za Bunge (Bunge Marathon) msimu wa tatu mwaka 2026 yamekamilika ambapo mbio hizo zitashirikisha wananchi zaidi ya 5000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wabunge
Mbunge Sanga amesema hayo leo Aprili 14, 2026 bungeni Jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabaria mbapo amesema tayari mdhamini mkuu wa mbio hizo, kampuni ya Silent Ocean imekabidhi vitendea kazi vyote na maeneo ya mbio hizo tayari yameainishwa.
Aidha amesema kusudio la bonanza hilo ambalo litashirikisha wabunge na wananchi ni kuendelea kuunga mkoni jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha michezo ili kuimarisha afya na vile vile Bunge kujenga mahusiano ya kuwa karibu na wananchi.
Pia ametoa wito kwa wananchi wote nchini kushiriki katika mbio hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, Aprili 18, 2026 kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Sanga amesema mashindano ya mwaka huu yatakuwa na zawadi kubwa zikiwemo fedha taslimu.
Aidha, amesema mbio hizo kwa sasa zimepata ithibati ya kutambulika kimataifa, hivyo washindi wa mbio hizo kwa mwaka huu watawekwa kwenye rekodi ya dunia.Sanga akionyesha medari watakazokabidhiwa washindi na washriki wa mbio hizo
Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti huyo pamoja na wadhamini wakuu wa mbio hizoWakionyesha mavazi watakayovaa wakati wa mbio hizo

Comments
Post a Comment